Diamond Ajisifia Baada ya Familia yake Kupata Deal la Vodacom..."Mimi, Tiffah na Zari ni Brand"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Familia ya Diamond Platnumz yote ni brand, kwa mujibu wake mwenyewe.
Yuko sahihi kwasababu si yeye tu anayenufaika na ubalozi wa mabilioni ya shilingi wa Vodacom Tanzania. Mchumba wake Zari, mtoto wao Tiffah na mama yake Sandra, wote wamepiga mpunga kutokana na ubalozi huo unaoshuhudia familia nzima ikishiriki kwenye tangazo la promotion mpya ya mtandao huo, Ongea Deilee.

Ni mtu mmoja tu muhimu aliyekosekana – Abdul, baba yake Diamond ambaye kwa wengi anaonekana kuwa ‘mcharuko’ kiaina kiasi cha mwanae kutopenda kujihusisha naye. Bila shaka itamchukua miaka mingi Diamond kumtengeneza naye kuwa brand.

“The Most Powerful and Impactful Family in Africa!!!… Bibi Brand, Baba Brand, Mama Brand Mtoto ndio Usiseme!!…. thanks for the Big Love our People… and get ready for another Big Thing,” ameandika Diamond kwenye Instagram.
Kweli hela huenda kwa wenye nazo tayari!
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wataingia nazo kaburini??

    ReplyDelete
  2. KIPOFU KAONA MWEZI.

    ReplyDelete
  3. Fala sana domo
    Na hao Vodacom
    Tuwa tumbulie jipu
    Boycott Vodacom
    Tuone atatamba Na lipi

    ReplyDelete
    Replies
    1. unafikiri riziki anatoa shangazi yako,yaani unaroho mbaya kama shetani.Basi na mi naomba mungu achukue mikono yako tuone utatamba na nini

      Delete
  4. Ushauri WA bure kwa Diamond Je wewe umefanya kitu gani kwa jamii yako je umeweka angalau kisima kwenye Primary school yako au umepaka rangi ukuta WA shule yako uliyisoma please Do something at leas

    ReplyDelete
  5. Big it up diamond family Zari ndio kaupatia harudi kwao tena anatafuta chakula cha wanae Good Girl

    ReplyDelete
  6. tatizo la Dai akisha chukua pesa anazopewa haangali kama kampuni ni figisufifisu gani. ili mradi yake yanamuendea. ni kama yale ya doct Mwaka. halafu sifa za kijinga sasa. utafikiri kaona pesa jana.

    ReplyDelete
  7. ILE STATE HOUSE ALISEMA KILA KITU NI DHAHABU. KUMBE NI RANGI YA KAWAIDA. SASA VODA ATASEMA WAMEMPA DHAHABU ZA TIFAA.

    ReplyDelete
  8. Dai anaangaika sana kujionyesha kwa watu hakuna kama yeye tz. kumbe siri ya mtungi ajuae kata.

    ReplyDelete
  9. siyo kupaka ranga nyumba muulize huyo Almasi kawasaidia yatima wangapi kama kweli anapaa mkwanja mwingi. msidanganyike na picha za kiki. DNA ndo imekuwa jiiiiiiiiiiiiiii mpaka leo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyie wote mnaotaka apime DNA mnafikiri domo atakubali?? yeye sio mjinga kiasi hicho, mnadhani hayo 'madili' alopata kupitia huyo mtoto yatakuwaje ikibainika mtoto si'wake?? PRESHA INAPANDA PRESHA INASHUKA

      Delete
  10. rizki hatoi shangazi wala jini. cha kushangaza urine tulionyeshwa mimba tukatangaziwa. ila DNA kimyaaaaaaaaaaaa! na mambo ya kiki kila saa. fikiri kabla hujajibu pumbavuuuuuuuuuu Anony 6.25 PM

    ReplyDelete
  11. Mhh huyu kaka anajiona kayapatia maisha. katoka kwenye umaskini mkubwa sana. sasa kila afanyacho ni kiki tuu. ohh Tifaa anamillion 200. ohh vitu vikubwa vinakuja wakati wenye pesa huwasikiii hata wakikohoa.

    ReplyDelete
  12. DNA ajuae bi Zari lkn akumbuke msaada kwa jamii Ni muhimu Sana hata ajenge visima,Na msaada kwa watoto wenye matatizo Hospitalini sio sifa tuu kila SK Mara nimelipwa Na MTV Mara nimeuza sn jee hao wapenzi wk wachache umewaonyesha nini kipya

    ReplyDelete
    Replies
    1. NIMEKUSTUKIA MTU MMOJA UNACOMMENT TOKA SAA 6:20 MPAKA 6:40. KWELI UNA CHUKI NAE. HAYA KAZANA LABDA NA WEWE UTAPATA SIKU MOJA ILA KWA CHUKI HIZO SIJUI?

      Delete
    2. Kweli nakuunga mkono Kuna mtu anatumia 20minutes cucoment So

      Delete
  13. kumbe zari na Tiffa ni bidhaa haaah zikichuja? kweli akili ni nywele kila mtu anazo zake , na huyu Zari anashindwa hata na ndege vitoto vyote kwenye kiota kimoja

    ReplyDelete
  14. Duh watanzania mna chuki Mbaya Sana yani kupata kwa mwenzenu mimeno inawatika hivyo😡 kisha mna kesha mkilia umasikini kwa mwendo huu Na roho zenu za kutu mtakufa hata kuku Tu wa kwako wakufuga huta pata. Shenzi zenu mfyuuu Dai Yuko juu Tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad