KIMENUKA Kwa Nay wa Mitego, BASATA Waufungia Wimbo wake Mpya Rasmi..Kumchukulia Hatua za Kisheria

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BASATA imetoa taarifa hiyo kwenye ukurusa wake wa twitter, na kuelezea kuwa wameamua kuufungia wimbo huo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili na uchochezi.

“BASATA limeufungia rasmi wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ ulioimbwa na msanii Nay wa Mitego kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili, uchochezi”, waliandika BASATA.

Pia BASATA imesema itamchukulia hatua za kisheria msanii huyo na kumtaka kutoutangaza wimbo huo.
“BASATA litampa karipio kali Msanii huyo na kumwagiza kuacha kuutangaza wimbo huo katika media, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa,

Pamoja na hayo BASATA imesema wasanii wengi wanatumia muda mwingi kubuni na kutengeneza kazi nzuri, lakini kuna wachache ambao wanaharibu, hivyo hawatawafumbia macho watu hao.

“Wasanii wengi wanafanya kazi zao vizuri, kwa kubuni kazi zenye ubora na zinazolipa sifa taifa, wachache wanaharibu, wanapakaa matope , BASATA halitavumilia hawa ‘wasanii’ wachache wanaotaka kuigeuza tasnia ya sanaa na wasanii genge la wahuni, wasio na staha,wa kudharaulika”, ilisema BASATA.

Kwa mujibu wa sheria kifungu cha 4 (2) cha sheria hii kinalipa Baraza nguvu ya kisheria kufanya jambo lolote lile kuliwezesha kufanya majukumu yake kwa faida na ustawi wataifa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wakishaufungia wamchunguze Na kichwa pia Na maji anywayo asije dhuru jamii haraka sana

    ReplyDelete
  2. Huo ni ubabaishaji tuu kwani Huyo Ney wa mitego katoa wimbo gani amboa hauna uchochezi, matusi, fedheha, uzalilishaji? Wangechukua tokea mwanzo but at this time, nothing will be helping at all, but it much better to hold tightly law, rules and regulations.

    ReplyDelete
  3. kabla ya yote mngemuwahisha mirembe akapate dose kamili.

    ReplyDelete
  4. Enter your comment...nawapongeza Sana basata na iwe fundisho kwa wengine

    ReplyDelete
  5. nisawa basata wako vizur

    ReplyDelete
  6. Kaa chini sumbua kichwa fanya kazi km wenzio utunge mistari sio unaleta bangi tuu swhaain

    ReplyDelete

Top Post Ad