Makonda Asema hataki kuwaona wasanii nyumbani kwake.......Ni Baada ya Kumtosa kwenye uzinduzi wa kampeni ya usafi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema hataki kuwaona nyumbani kwake wasanii ambao wamekacha kuhudhuria kampeni yake ya usafi ambayo imezinduliwa Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.


Akizungumza katika uzinduzi huo, Paul Makonda ameonesha kusikitishwa na idadi ndogo ya wasanii waliojitokeza kuunga mkogo kampeni hiyo.


“Lakini nashukuru wasanii wote ambao wamejumuika nasi, na kwa kweli hiki ni kipimo cha kuwatambua marafiki zangu wa kweli ni wapi. Na mimi niwaambie tu, sitaki kuona msanii yoyote nyumbani kwangu ambaye hawezi kuniunga mkono kwenye mambo yangu ya maendeleo,”alisema Makonda.


“Sitaki hiyo tabia, nimemuona Steve Nyerere hapa amekuja akiwa amechelewa hilo ni onyo, ukirudia tena nakushughulikia. Huwezi kuwa rafiki yangu alafu kwenye mambo kama haya huhangaiki, wengine wanataka waombwe, eti mbona hujanipigia simu kuniomba nipost, we nani?. Swala la usafi siyo la serikali ni swala la kila mtu,”aliongeza Makonda.


Wasanii ambao walihudhuria uzinduzi huo ni, Mchizi Mox, Yamoto Band, Diamond na team ya Wasafi, Mwasiti, Queen Darleen, Salam TMK pamoja na Steve Nyerere wa bongo movies.h


Katika hatua nyingine Makonda amevitaka vyombo vya usafiri jijini Dar es salaam kuwa na vifaa vya kuwekea uchafu.


Pia wamewataka wafanyabiashara siku ya jumamosi, kufungua maduka yao saa 3 asubuhi ili muda wa asubuhi wautumie kwa ajili ya kufanya usafi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wanakuja kwako ? kuna nni?

    ReplyDelete
  2. Hahahaaa huyu mjinga kweli,kwani ukuu wa mkoa ndo Nini !!!?mbona anajishauwa sanaa!!!mxiuuu!!!elimu yenyewe zero

    ReplyDelete
  3. Makonda Ni Kijana Mchapa Kazi... Wito wake ni kwa Ajili ya Jiji Letu na Nchi Yetu.. Je wewe uliyekuwa haukuhudhuria Umejulikana? Lakini wasaaani kawataja kwa Ajili ya kuwa wao ni Vioo vya Jamii... kuhudhuria kwao kwa wingi kungekuwa ni Gumzo mitaani na kungeweza kumuhamasisha Kila mwana jiji na effect yake ingekuwa ni ya muda mrefu... Cha muhimu ni kwamba Usafi ni Imani ni huluka na ni mazoea.. Ninaamini Makonda na mimi wewe yule na wale wote tunawajibika kuona Usafi ni kipaumbele kwa jamii na kaya zetu popote tulipo ila Daresalama ni mji unafikiwa na wageni wengi KWA HIYO SURA YA JIJI NA USAFI WA JIJI NI MUHIMU IKIWEPO PIA USAIDIAJI WA SISI WENYEWE KWA WENYEWE NA UPENDO KATI YETU... HII INACHUKULIWA KAMA KIGEZO... KWA HIYO NDUGU ZANGU SHIME SHIME NA MAKONDA ILI TUSIANGUSHANE NA BABA JPJM...TUMUUNGE MKONO KWA HALI NA NGUVU ZETU... USAFI KATIKA MAZINGIRA NA JAMMI NI MUHIMU WAKATI WOTE....MOKONDA TUKO BEGA KWA BEGA ENDELEA NA KAMPENI ZAKO ZOTE ZA MAENDELEO NA SURA YA MJI WETU... HONGERA INARIDHISHA NA TUNARIDHIKA...WE NI MCHAPA KAZI...HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  4. Makonda Ni Kijana Mchapa Kazi... Wito wake ni kwa Ajili ya Jiji Letu na Nchi Yetu.. Je wewe uliyekuwa haukuhudhuria Umejulikana? Lakini wasaaani kawataja kwa Ajili ya kuwa wao ni Vioo vya Jamii... kuhudhuria kwao kwa wingi kungekuwa ni Gumzo mitaani na kungeweza kumuhamasisha Kila mwana jiji na effect yake ingekuwa ni ya muda mrefu... Cha muhimu ni kwamba Usafi ni Imani ni huluka na ni mazoea.. Ninaamini Makonda na mimi wewe yule na wale wote tunawajibika kuona Usafi ni kipaumbele kwa jamii na kaya zetu popote tulipo ila Daresalama ni mji unafikiwa na wageni wengi KWA HIYO SURA YA JIJI NA USAFI WA JIJI NI MUHIMU IKIWEPO PIA USAIDIAJI WA SISI WENYEWE KWA WENYEWE NA UPENDO KATI YETU... HII INACHUKULIWA KAMA KIGEZO... KWA HIYO NDUGU ZANGU SHIME SHIME NA MAKONDA ILI TUSIANGUSHANE NA BABA JPJM...TUMUUNGE MKONO KWA HALI NA NGUVU ZETU... USAFI KATIKA MAZINGIRA NA JAMMI NI MUHIMU WAKATI WOTE....MOKONDA TUKO BEGA KWA BEGA ENDELEA NA KAMPENI ZAKO ZOTE ZA MAENDELEO NA SURA YA MJI WETU... HONGERA INARIDHISHA NA TUNARIDHIKA...WE NI MCHAPA KAZI...HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  5. Wape mgongo watakuja wengi
    Dogo ana mtalimbo hujakutosha

    ReplyDelete

Top Post Ad