Chid Benz Akanusha Kutoroka Rehab ila Ameruhusiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii Chid Benz amekanusha taarifa zilizopo kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao kuwa ametoroka rehab Bagamoyo, alikokuwa akipata tiba ya kuacha madawa ya kulevya.

Akiongea na East Africa Radio Chid Benz amesema si kweli kwamba ametoroka, isipokuwa ameruhusiwa kutoka rehab.

"Wameongea uongo hao wajinga, nimeachana nao kwa sababu hatuwezi kubishana nao, mi nimetoka niko sawa, nipo fresh na siwezi kubishana na magazeti, na sasa hivi nipo studio nataka niingie kurekodi, kwa hiyo sio kweli kama nimetoroka rehab, nimetoka kwa sababu nimeruhusiwa", alisema Chid Benz.

Hata hivyo East Africa Radio iliamua kumtafuta mtu wa karibu wa Chid Benz (Madee) ambaye naye yupo chini ya Babu Tale, na kuthibitisha taarifa hizo kuwa hajatoroka kweli.

Chid Benz alipelekwa rehab Bagamoyo mwezi wa 3 mwaka huu, baada ya meneja wa TipTop kujitolea kumsaidia kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, ambayo yalikuwa yameshamuathiri.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unajidanganya mwenyewe that is ur life who care,,,ilulipata msaada kama umeuchezea is up to u,,,ule usile maisha ni yako.

    ReplyDelete
  2. TRUE MDAU!!!

    ReplyDelete
  3. Kweli kbs wadau umechezea bahati hiyo hutaipata tena subiri cku yako ifike c tutahudhunika cku mbili Tatu bac tutakusahau kama wengine yaani umenikera kupita kiasi coarse cku niliyokuona ktk hali Ile machozi yalinitoka leo najutia chozi langu kwa hanithi wewe

    ReplyDelete

Top Post Ad