Mtoto wa Wilson Kabwe AGOMA Kupokea Mkono wa Pole Toka Kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Anna Kabwe, binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amegoma kumpa mkondo Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Tukio hilo la aina yake lilimfika Makonda aliposhiriki shughuli ya kuaga mwili wa Kabwe katika Viwanja vya Karimjee alipokuwa akitoa mkono wa pole kwa familia ya Kabwe.

Wakati Makonda akimpa mkono, Anna aliendelea kuchezea simu yake huku akipuuza mkono wa kiongozi huyo. Anna alifanya hivyo akiwa amekaa huku ndugu zake wengine wakiwa wamesimama wakati wakipokea mkono huo wa pole.

Kitendo hicho kimetafsirika kwamba, Anna alikumbuka tukio lililofanywa Aprili 19 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni ambapo Makonda alimtuhumu marehemu Kabwe (baba yake) kwamba amehusika na kusaini mikataba iliyoikosesha mapato serikali.

Kabwe alifariki tarehe 19 Mei mwaka huu kutokana na tatizo la ini. Mauli yalimkuta akiwa katika Hospitali ya Mama Ngoma jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Ameacha mjane na watoto watano; wanne wa kiume na mmoja wa kike.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tumbua lazima italeta chuki tu...

    ReplyDelete
  2. Hawa watoto walizoea kulelewa,sasa mtu asifanye kazi.Makonda piga kazi,na tunamuombea marehemu apumzike salama.

    ReplyDelete
  3. Hizo ni nyodo tena nyodo kubwa sana na kimsingi ni kitendo kinachopaswa kulaaniwa hasa ukizingatia Mkuu wa Mkoa licha ya yeye mwenyewe pia alikuwa anamuwakilisha Rais wa Nchi. Hili ndilo tatizo la hawa majibu, walikuwa wamezoea na kuunda matabaka makubwa sana katika Taifa hili. Lakini mwisho wa hizo dharau tutaziona.

    ReplyDelete
  4. Hacheni kujipendekeza kwa Makonda, tena tusimurahumu bure binti wa watu (Anna Kabwe)
    Sababu hatujuhi kabla baba yake ajafa nini walicho kiongea!! Mwisho uchungu wa mtoto wa kike na wakiume kuna tofauti kubwa.Mwenye kutoa huku ya kweli ni Mungu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ...hacheni, ...tena tusimurahumu bure, ... hatujuhi, we mrundi eti?

      Delete
    2. ...hacheni, ....tusimurahumu bure, ....hatujuhi, ....., we Mrundi eee?

      Delete
  5. Hangefanyiwa BABA YAKO HUSINGEPOKEA HILO KONO

    ReplyDelete
  6. dada kafanya la maana hata mimi nisingepokea mkono wake

    ReplyDelete
  7. huyo dada hana akili walitegemea andelee kutunyonya wao waendelee kuishi kifahari Makonda tumbua tu hata kama ni maiti ilihujumu uchumi ifukuliwe na itumbuliwe hadharani kwasababu nchi ilikuwa imefika mahali pabaya kumpa mkono kutompa mkono haisaidii kurudisha juhudi za serikali katika kurekebisha tabia za baadhi ya watendaji. tumeuona mkonon wa magufuli ndio ukawe wa ana aende zake nfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu wtatumbuliwa tu

    ReplyDelete
  8. anatafuta kiki huyo hana lolote akatae asikatae atatumbuliwa tu

    ReplyDelete
  9. dada kafanya poa, haikuwa lazima kumpa mkono

    ReplyDelete
  10. Amekataa kupokea mkono wa muheshimiwa.......then what???? HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  11. Hasira,chuki?marehemu hasemwi,HAPA KAZI TUUUUUUUUUUU.

    ReplyDelete

Top Post Ad