Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye Akerwa na Ving'ang'anizi wa Madaraka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye amezitaka nchi za Afrika kuhakikisha zinakubali kubadilishana madaraka pale chama kimoja kinaposhindwa kuongoza ili kuepusha nchi kuingia kwenye machafuko.

Aidha, Sumaye alisema ni vyema wataalam wakaongoza nchi kwa kubuni mbinu mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.

Sumaye aliyasema hayo jana Jijini hapa wakati akizungumza kwenye kongamano la Nafasi ya Wasomi na Wafanyabiashara Katika Kujenga na Kukuza Uchumi wa Nchi, lililoshorikisha viongozi wa vyama, wafanyabiashara na wasomi wa kada mbalimbali wa Arusha.

Sumaye alisema uongozi ni kubadilishana nafasi na katika nchi za Ulaya kwa mfano, chama kikishindwa kutawala kinakubali lakini kwa nchi za Afrika kuna uroho wa madaraka au ubinafsi.

"Tunataka kuwajengea uwezo wasomi wetu kwa kujiamini na kujipatia fursa za kujikwamua kiuchumi," alisema Sumaye ambaye alikuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 mfululizo kati ya 1995-2005, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi.

"Ubinafsi tuache, tukishindwa uchaguzi achia ngazi.Mimi niliyasema haya nikiwa CCM na leo hii nipo Chadema nasema unapoang'angania madaraka, aidha unaogopa ukiachia utasababisha machafuko au ubinafsi."

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Dk. Vincent Mashinji akifungua kongamano hilo, alisema chama chake kinataka kutengeneza mabepari wa kitanzania ambao watajiongeza wenyewe katika kujiinua kiuchumi.

Alisema Arusha ni mji wa kitalii hivyo ni vyema wafanyabiashara wakatumia fursa zilizopo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi, na inawezekana Jiji hilo kuwa na fursa nyingine za kibiashara badala ya kutegemea madini ya Tanzanite pekee.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yeye mwenyewe ndio aache uking'ang'anizi wa madaraka. Ameshindwa Chama kimoja amehamia Chama kingine na kama sio uroho wa madaraka ni nini??? Kweli nyani halioni Kundule.

    ReplyDelete
  2. Kitendo chake cha kutoka chama kimoja cha siasa kwenda chama kingine cha siasa hiyo inadhihirisha ni kwa kiasi gani alivyokuwa na uroho uliokithiri wa madaraka. Halafu leo hii na bila hata ya aibu anawasema wenzake. Huo ni ubabaishaji mkubwa aliokuwa nao huyo kiongozi.

    ReplyDelete
  3. We Magumashi, ulikuwa katika Game miaka mingapi.. na ulifanya nini? Leo unazungumza! Ndugu zangu wa TRA je mnangoja nini kufanya ziara za uhakiki. wametuletea vipele mpaka wametupa kazi ya utumbuaji baada wa kuwiva chunusi na kuwa jipu..inashangaza ni vigezo gani vilimweka Huyu ndugu yetu katika MaDalaka na bila kushtukia.ni lazima tumuangalie. Japokuwa afya ni tatizo. Hatima yake ndiyo tuko katika kila kitu HEWA..HEWA...HEWA...HEWA...HEWA...na inasemekana aliweza kukaa awamu mbili...na ukiangalia madaa na hoja anazo bwatuka bwatuka inaleta mashwali mengi bila majibu sahihi na ya kuridhisha .. afike ngazi ya alipofika ...????!!!! utumbo mtupu....What is your current status? Angalia his definitiona of Uongozi" Uongozi ni kubadilishana NAFASI" JIPU JIPU TENA LIMEJAA USAHA>>>> Litapasuka hata bila KUTUMBULIWA... JP unakazi BABA

    ReplyDelete
  4. We Magumashi, ulikuwa katika Game miaka mingapi.. na ulifanya nini? Leo unazungumza! Ndugu zangu wa TRA je mnangoja nini kufanya ziara za uhakiki. wametuletea vipele mpaka wametupa kazi ya utumbuaji baada wa kuwiva chunusi na kuwa jipu..inashangaza ni vigezo gani vilimweka Huyu ndugu yetu katika MaDalaka na bila kushtukia.ni lazima tumuangalie. Japokuwa afya ni tatizo. Hatima yake ndiyo tuko katika kila kitu HEWA..HEWA...HEWA...HEWA...HEWA...na inasemekana aliweza kukaa awamu mbili...na ukiangalia madaa na hoja anazo bwatuka bwatuka inaleta mashwali mengi bila majibu sahihi na ya kuridhisha .. afike ngazi ya alipofika ...????!!!! utumbo mtupu....What is your current status? Angalia his definitiona of Uongozi" Uongozi ni kubadilishana NAFASI" JIPU JIPU TENA LIMEJAA USAHA>>>> Litapasuka hata bila KUTUMBULIWA... JP unakazi BABA

    ReplyDelete
  5. We Magumashi, ulikuwa katika Game miaka mingapi.. na ulifanya nini? Leo unazungumza! Ndugu zangu wa TRA je mnangoja nini kufanya ziara za uhakiki. wametuletea vipele mpaka wametupa kazi ya utumbuaji baada wa kuwiva chunusi na kuwa jipu..inashangaza ni vigezo gani vilimweka Huyu ndugu yetu katika MaDalaka na bila kushtukia.ni lazima tumuangalie. Japokuwa afya ni tatizo. Hatima yake ndiyo tuko katika kila kitu HEWA..HEWA...HEWA...HEWA...HEWA...na inasemekana aliweza kukaa awamu mbili...na ukiangalia madaa na hoja anazo bwatuka bwatuka inaleta mashwali mengi bila majibu sahihi na ya kuridhisha .. afike ngazi ya alipofika ...????!!!! utumbo mtupu....What is your current status? Angalia his definitiona of Uongozi" Uongozi ni kubadilishana NAFASI" JIPU JIPU TENA LIMEJAA USAHA>>>> Litapasuka hata bila KUTUMBULIWA... JP unakazi BABA

    ReplyDelete
  6. TUTAKUPA KITI KATIKA WABUNGE ILI UWE NA WENZAKO UNAOFANANA NAO!!!

    We Magumashi, ulikuwa katika Game miaka mingapi.. na ulifanya nini? Leo unazungumza! Ndugu zangu wa TRA je mnangoja nini kufanya ziara za uhakiki. wametuletea vipele mpaka wametupa kazi ya utumbuaji baada wa kuwiva chunusi na kuwa jipu..inashangaza ni vigezo gani vilimweka Huyu ndugu yetu katika MaDalaka na bila kushtukia.ni lazima tumuangalie. Japokuwa afya ni tatizo. Hatima yake ndiyo tuko katika kila kitu HEWA..HEWA...HEWA...HEWA...HEWA...na inasemekana aliweza kukaa awamu mbili...na ukiangalia madaa na hoja anazo bwatuka bwatuka inaleta mashwali mengi bila majibu sahihi na ya kuridhisha .. afike ngazi ya alipofika ...????!!!! utumbo mtupu....What is your current status? Angalia his definitiona of Uongozi" Uongozi ni kubadilishana NAFASI" JIPU JIPU TENA LIMEJAA USAHA>>>> Litapasuka hata bila KUTUMBULIWA... JP unakazi BABA

    ReplyDelete
  7. Mr zero wewe huna akili ulikuwa madarakanin muda mrefu hatukuona chochote ulichokifanya lakini kutokana na ulafi wa madaraka ukaamua kuhama na kuamia chadema ili upate madaraka sasa unaanza kuongea vitu ambavyo havina kichwa wala miguuu wakati hayo unayoyaonge yanakugusa mwenyewe. hivi inafikiri wewe utakumbukwa kwalipi? hatuwezi kukumbuka kwa lolote lile maana wakati wewe ukiwa kiongozi ulujilimbikizia mali nyingi na kuacha watu wa chini tunateseka sasa unakurupuka na kutoa maelezo ambayo hayaeleweki kazi tunaiona kwa magufuli tu (sijui umekula maharage ya wapi weweeeeee ewe sumaye ni nani aliyekurogaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa jipime mwenyewe uone kama unafaa, hufai hata una uchu wa madaraka na hao waliokukalibisha wataisoma wataliwa kwa ni wewe mwenyewe hufai kuwa kiongozi

    ReplyDelete

Top Post Ad