google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Clouds TV yajikuta Kwenye Kitimoto Kwa Kurusha Kipindi Kuhusu Ushoga, Makonda Awatetea | UDAKU SPECIAL

Clouds TV yajikuta Kwenye Kitimoto Kwa Kurusha Kipindi Kuhusu Ushoga, Makonda Awatetea

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Clouds TV ipo kwenye kitimoto baada ya kipindi chake cha Take One kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema kumhoji shoga maarufu jijini Dar es Salaam.


Pamoja na Zamaradi kudai kuwa na nia njema ya kumhoji mtu huyo kwa madai suala hilo limekuwa tatizo nchini na ni muda wa kulizungumzia bila kificho, Watanzania wengi wameonesha kupinga kwa madai kuwa kipindi hicho kimetumika kulitangaza zaidi tatizo hilo.

Wapo pia wanaomtetea Zamaradi na hivyo kusababisha kuwepo na mgawanyiko mkubwa wa kimsimamo kuhusiana na suala hilo kama Tanzania imefikia hatua ya kuwepo mijadala ya aina hiyo kwenye runinga za taifa, seuze kuwahoji kabisa watu hao.

Hata hivyo Jumatano hii Clouds TV imelazimika kufanya kile kinachojulikana kama ‘damage control’ kujaribu kufafanua kwa wananchi kwanini ilikuwa sawa kuwa na kipindi cha aina hiyo.

“Suala hili ukilitazama positively utapata kujifunza mengi sana, hiki ni kipindi cha toba na kuhamasishana mema na kuacha mabaya, hili ni baya na lazima tulipinge na kulikemea na tusiwaangalie mashoga pekee tuwaangalie pia wale wanaoshirikiana nao ambao tuko nao ndani ya jamii,” alisema Zamaradi kwenye kipindi cha 360 cha kituo hicho alipohojiwa kueleza kwanini aliamua kufanya mahojiano na mtu huyo.

“Tusisubiri mambo yaharibike zaidi ndio tuanze kuzungumza lazima tuchukuwe hatua sasa, kama tunavyoweza kumhoji mwathirika wa madawa ya kulevya na kuamini kwa kujua njia alizopitia tutaweza kuepuka na kuwaelimisha ndugu na jamaa zetu ndivyo hivyo tujifunze walipokosea hawa,” alisisitiza.

“Je kuna tamthilia ngapi za nje zinaonekana kwenye runinga zetu zenye maudhui yenye hulka kama hizi na utofauti wa kipindi nilichofanya na tamthilia za nje ni kwamba kipindi changu kimelenga kukemea na kufundisha,kikubwa shtuka na chukua hatua. Leo ukienda kwenye kumbi za starehe kwenye taarabu haya yamekuwa ni mambo ya kawaida na pia ukipita Instagram utakuta page zao kabisa.”

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipiga simu kwenye 360 na kutetea kurushwa kwa kipindi hicho.

“Hatuwezi kubadilika kwa kuendelea kuishi katika mazingira tuliyoyazoea, tunakaa kwenye mazingira kama vile tupo sawa na akija wa kutuambia hatupo sawa tunawakebehi na kuwashambulia,” alisema Makonda.

“Tuamke na hizi hasira tuelekeze kwenye tatizo ambalo lipo kwenye jamii yetu, wazazi na walezi tujenge tabia ya kukagua watoto wetu tukiamka pia majirani zetu. Sisi kama Serikali tumeamshwa na pia inabidi waanze kutaja wateja wao ili jamii iwafahamu kwani inawezekana wateja wao wengine ni viongozi wa serikali,” aliongeza.

Hata hivyo bado wananchi wengi wameendelea kusisitiza kuwa kipindi hicho kimekiuka misingi ya utangazaji na kuitaka TCRA ichukue hatua.

Hizi ni baadhi ya barua zilizotukwa kwenye mamlaka hiyo ya mawasiliano kulalamikia kipindi hicho.




-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mi sioni kosa la hicho kipindi kipindi kipo na ukifunza utagundua kitu ushoga ni ugonjwa hawa watu wameathirika kisaikolijia na wakipewa msaada kiakili wanaacha...hili tatizo sio kuwatenga wewe kama wanao wako kamili mshukuru Mungu hawa watu wanahitaji msaada wa kiakili kuwarudisha sawa...ukimsikiliza huyo kijana itajifunza kitu

    ReplyDelete
  2. MSIPOKUBALI KUZUNGUMZA HAMJATATUA TATIZO. HAO WATOTO MNATAKIWA KUWAAMBIA UKWELI ILI WAJUE JAMBO HILO NI BAYA. UTAMFICHA NYUMBANI AKITOKA KWENDA SHULENI ATAKUTANA NALO. NA ATAKUWA HAJAJIANDAA KUPAMBANA NALO. UNAMJENGAJE MTOTO KUFIKIRI ANAISHI MAHALI SALAMA WAKATI AKIKUA ATATOKA NA ATAYAKUTA? USIPOMWELIMISHA ATAJUAJE KUJILINDA. KUFICHA UKWELI SIO SALAMA KABISA. ACHA MAMBO YAJADILIWE ILI WAZAZI WAJUE JINSI YA KUWAANDAA WATOTO WAO KUEPUKANA NA MAMBO KAMA HAYA.

    ReplyDelete
  3. HAPO SI KUAMBIWA UKWELI NI KUTANGAZA BIASHARA YAO. SIO KILA KITU KINAWEKWA HADHARANI JAMANI NDIO MAANA KULIKUWA NA JADO NA UNYAGO !!! WAADHIBIWE KWA KURUSHA KIPINDI HICHO CLOUDS

    ReplyDelete
  4. Kuna watu inabidi wawe wananyongwa kwa masilahi ya TANZANIA na watu wake.
    Huyu Kijana ameshajulikana,sioni sababu kwa nini aendelee kuishi akifundisha ujinga vijana wetu wengine. Sio mbaya akipotezwa na kuzikwa na City kimya kimya kwa sababu hata wazazi wake sidhani kama watalia!

    ReplyDelete

Top Post Ad