Jerry Muro Aitwa Kamati ya Maadili TFF....Kisa Hichi Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MKUU wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanha Jerry Muro ameitwa kwenye kikao cha kamati ya maadili cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF kufuatia kitendo chake cha kupingana na kuishambulia katika kuelekea mechi yao ya Kimataifa ya kombe la Shirikisho Barani Afrika uliofanyika Juni 28.

 Hiyo inakuwa ni mara ya tatu kwa Muro kuitwa na anatakiwa kufika Julai 02 katika ofisi za TFF saa Nne asubuhi au kama atashindwa kufika basi atume mwakilishi wake au utetezi wake kwa njia ya maandishi.

Muro amethibitisha hilo na kusema kuwa amepokea barua hiyo na hii ikiwa ni mara ya tatu na katika mara zote amekuwa anashinda kwa hoja na kwa.wakati huu mkakati wao mkubwa kuona nafungiwa kujihusisha na masuala ya mpira na zaidi anashangaa ni jinsi gani wanasema amewashambulia kupitia vyombo vya habari.

Barua hiyo inamtaka Muro kujitokeza siku hiyo au hata kama hatoweza kufika basi atume utetezi wake kwa maandishi au mwakilishi wake na hata kama hatofika basi kikao cha kamati ya maadili kitaendelea kama kawaida na watatoa maamuzi kama kawaida.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mimi sio shabiki wa Muro,lakini
    TFF kuweni makini na hili na sio kutaka
    kumkomoa Muro,nawaambieni tena kuweni makini.
    NIMEMALIZA.

    ReplyDelete
  2. Wapenzi wa soka nchini kuna JIPU kubwa TFF ambalo wengi wetu tunalijua lakini sijui kwa nini viongozi wa wizara husika wanakaa kimya. Wanamuogopa au kumwonea haya MALINZI ? TFF kwa sasa haina muelekeo mzuri, kila siku matatizo wilayani, mikoani na nchi nzima. Sijui ana nia gani na soka letu, kwani hata wafadhili wamechoka na uozo wa TFF. Mheshimiwa Nape, uwezo unao na hoja zipo wazi, nakuomba ulishughulikie jipu hili otherwise litakua janga la taifa ambalo hata wewe Mheshimiwa litakukumba.......

    ReplyDelete
  3. Wapenzi wa soka nchini kuna JIPU kubwa TFF ambalo wengi wetu tunalijua lakini sijui kwa nini viongozi wa wizara husika wanakaa kimya. Wanamuogopa au kumwonea haya MALINZI ? TFF kwa sasa haina muelekeo mzuri, kila siku matatizo wilayani, mikoani na nchi nzima. Sijui ana nia gani na soka letu, kwani hata wafadhili wamechoka na uozo wa TFF. Mheshimiwa Nape, uwezo unao na hoja zipo wazi, nakuomba ulishughulikie jipu hili otherwise litakua janga la taifa ambalo hata wewe Mheshimiwa litakukumba.......

    ReplyDelete

Top Post Ad