Maskini Baba Diamond Platnumz, Azidiwa Ghafla!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Maskini wee! Baba wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma ‘Baba D’ anaumwa sana! Ndivyo Risasi Mchanganyiko linavyoweza kukuhabarisha baada ya mzazi huyo kuzidiwa ghafla na kukimbizwa hospitalini kutibiwa kwa msaada kutokana na kukosa fedha, twende hatua kwa hatua.

NI JUMAPILI ILIYOPITA
Tukio hilo la kusikitisha la baba mzazi wa msanii ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wa kutosha Bongo, lilijiri Jumapili iliyopita ambapo kwa msaada wa Dk. Fadhili Emily wa Kituo cha Tiba cha Fadhaget Sanitarium kilichopo Mbezi Beach-Africana, Dar, baba Diamond alifikishwa kutoka nyumbani kwake Magomeni-Kagera hadi hospitalini hapo na kupatiwa matibabu.

CHANZO CHAVUJISHA
Awali, Risasi Mchanganyiko lilipokea taarifa za mzee Abdul kuzidiwa nyumbani kwake lakini ikaelezwa kwamba, hakuwa na msaada wowote hadi majirani walipopata mawasiliano ya daktari huyo na kumuomba amsaidie.

“Jamani baba D (baba Diamond) yupo hoi hapa nyumbani kwake Magomeni. Miguu inamuuma, anashindwa kutembea na ukizingatia hana kipato, anashindwa pia kwenda hospitali. Na bahati mbaya kwa muda mrefu hata majirani wamekuwa wakimsaidia lakini bado hajapata tiba sahihi.”

AUNGANISHWA NA DK. FADHILI
“Leo (Jumapili) kuna jirani yake mmoja hapa ndiyo amepata wazo baada ya kusoma Gazeti la Risasi Jumamosi (ndugu na hili), amepata namba za Dk. Fadhili katika makala anazoandika gazetini kuhusu afya. Akampigia na kumuomba msaada na bahati nzuri dokta huyo ameguswa na tatizo la mzazi huyu, amemtumia nauli ya teksi ili akimbizwe  hospitalini kwake, sasa hivi ndiyo wanaelekea huko,” kilisema chanzo hicho.

MAKACHERO WAUNGA TELA
Licha ya kuwa muda huo ulikuwa umeyoyoma (saa 1 usiku), makachero wetu waliingia mzigoni kuelekea moja kwa moja Mbezi kwenye hospitali hiyo na kumkuta baba D akiwa anaingia mapokezi katika kliniki hiyo.


ASAIDIWA NA WAHUDUMU
Akiwa mapokezi, makachero wetu walimshuhudia baba Diamond akisaidiwa na vijana wawili ambao ni wahudumu wa hospitali hiyo, walimkalisha kwenye kochi kisha wakaanza kumpa huduma ya dharura ambapo walimpima presha na kumuita Dk. Fadhili atazame miguu yake.

KUHUSU MIGUU
Dk. Fadhili alipofika, alimvua soksi baba huyo na kuikagua vizuri miguu hiyo kabla ya kuingia naye ndani katika chumba maalumu cha vipimo na matibabu.

VIPIMO VINGINE
Ilibainika kuwa, miongoni mwa vipimo alivyopimwa baba D ni pamoja na kile cha Quantum Magnetic Analyzer ‘QMA’ ambacho kazi yake ni kutambua magonjwa mbalimbali ndani ya mwili wa binadamu. Hata hivyo, Risasi Mchanganyiko halikufanikiwa kujua kipimo hicho kilitambua nini!

BABA DIAMOND AFUNGUKA
Baada ya kupimwa na kupatiwa dawa za kutumia, baba Diamond aliliambia gazeti hili kuwa, anamshukuru daktari huyo kwani ameweza kugundua tatizo linalomsumbua na kwamba anaamini dawa alizopewa zitamsaidia.
“Kwa kweli ni Mungu tu, hali yangu ni mbaya, miguu inanisumbua kwa zaidi ya miaka nane sasa. Inauma, imevimba na inabadilika rangi kuwa myeupe. Inakuwa kama inatoka mabakamabaka. Kiuchumi siko vizuri kabisa.”

NGOZI IMEATHIRIKA
“Dk. Fadhili amenipima, amebaini ngozi yangu imeathirika vibaya. Amenitajia tatizo langu kitaalamu na amenipa dawa za kutumia, lakini pia amenielekeza mazoezi maalum ambayo natakiwa kuyafanya,” alisema baba Diamond huku uso wake ukijaa simanzi.


AMWAGA SHUKRANI
Baba Diamond alipoulizwa kama alimueleza mwanaye Diamond kuhusu suala hilo wakati alipozidiwa, alisema hakuona na haoni sababu ya kumwambia kwani analijua na hapendi kuendeleza malumbano na mwanaye lakini anamshukuru Dk. Fadhili kwa kujitolea kumsaidia bila malipo yoyote.


“Sipendi kuendeleza malumbano, ninachokiangalia kwa sasa ni miguu yangu. Nitamshukuru Mungu zaidi nitakapopona kabisa maana nimeshahangaika nayo sana. Kipekee, kutoka moyoni nimshukuru Dk. Fadhili kwa kusikia kilio changu na kunisaidia bure.
“Sikutegemea, mtu unaumwa, anakwambia anakutumia fedha ya teksi uende hospitalini kwake akakutibu bure. Ni upendo wa hali ya juu na Mungu amzidishie, pale alipotoa apabariki na apate zaidi,” alisema baba Diamond.


DIAMOND ANASEMAJE?
Gazeti hili lilifanya jitihada za kutaka kumsikia Diamond anazungumziaje suala hilo la ugonjwa hadi kufikia mzazi wake kusaidiwa na mtu baki, simu yake haikuwa hewani lakini hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia Mtandao wa WhatsApp ulioonesha ameusoma, bado hakujibu chochote.

TUMEFIKAJE HAPA?
Baba Diamond amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo wa miguu ambapo awali, mzazi huyo alisema anasumbuliwa na kansa ya ngozi lakini hata hivyo, mwanaye Diamond amekuwa mzito kumsaidia kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni mwanaume huyo kumtelekeza mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ yeye akiwa mdogo.

MAJIBU YA DK. FADHILI
Juzi Jumatatu, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu daktari huyo na kumuuliza kuhusu tatizo la baba Dimaond na namna alivyolishughulikia, ambapo alijibu:

“Ha! Jamani, ugonjwa wa mtu ni siri kati yake na daktari, labda kama ataona sawa aseme yeye mwenyewe.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

26 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kina babu tale mpo wapi msaidieni huyo mzee kama mnavyowasaidia wavuta unga kwa sifa

    ReplyDelete
  2. muacheni anakula alichopanda, ila pole mzee sana mzee lakini liwe fundisho kwa wazazi wote wanaotelekeza watoto wao kwa kisingizio cha kugombana na wenza wao. (yaani namaanisha wababa na wamama wote). diamond kama moyo wako unaridhia msaidie tu as if mtu wa kawaida ila kama nafsi inakataa basi take your time. sababu dawa ya moto ni moto.

    ReplyDelete
    Replies
    1. LAKINI KAA UKIJUA DAIMOND ALIKUJA DUNIANI KWA KUPITIA HUYU MZEE,ALIYOYAPATA NI NEEMA YA MWENYEZI MUNGU,NAOMBA USOME VITABU VYA DINI SANA.YOTE YATAPITA MANENO/MAANDIKO YA MWENYEZI MUNGU HAYATAPITA.MUNGU WETU ATUPE REHEMA.

      Delete
    2. HUNA DINI WEWE?

      Delete
    3. Bila shaka huujui msikiti wala kanisa ndugu.

      Delete
    4. Kukuleta sio ratizo, tatizo kukudumia. Watoto wangapi dunuani hawawajui baba zao. Wengine baba,Dagsavisen,wengine baba wazungu,wengine,baba wafrica hata hawajulukani walipo, walitimua. Kwa hiyo baba ukitaka ukamilike utimize yote, ya Uzazi na kulea mpka mtoto akue hapo utakuwa baba kamili duniani

      Delete
    5. Watoto wangapi Diamond wanatafuta baba zao wakiwa wakubwa Bwana leo wewe uje ujianike hivyo. Hata katika vitabu vya dini hakuna ujinga kama huo. Au ndio usanii unandika kitabu. Ila uangalie huenda ukaja ukamtafuta tayari Mungu nae keshamchukua utamani hata afufuke lakini ndio basi tena na dunia ikakucheka na kukunyooshea mkono.

      Delete

  3. Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. (Quran 17:23)

    Na pindi (wazazi) wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwat'ii. Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anaye elekea kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi, na Mimi nitakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda. (Quran 31:15)

    ReplyDelete
  4. Anayejua machungu yakutekelezwa kunyimwa kusomeshwa kunyimwa chakula mimi na mama yetu tumehangaika style hizi za domo leo baba aje hata aumwe awe anatambaa simsaidii Mungu na anisamehe tu...huyu baba muacheni aonje yale aliyoyafanya kwa mwanawe akiwa mdogo...wakati wakina domo walipomuhitaji wakiwa na shida kama hzo zake sasahv hakuonekana kipindi hicho let him feel the pain let him...aaarghh napatwa na hasira mm

    ReplyDelete
  5. namuelewa Diamond mimi mwenyewe mzazi wangu alinisaliti nikiwa mdogo bila ya hata kuniaga leo hii hata akiumwa siendi kumuona na hata akifa siendi kumzika

    ReplyDelete
  6. Hivi Daimond huwa katika mazungumzo anasema ana baba,au anasema hamjui babake?Haki labda kama unamilikiwa na shetani,lakini kama ni kwa imani tulizo nazo kwamba wote ngao/nguzo yetu ni Mungu basi hutakiwi kuwa na roho ya chuma kama ya huyu Daimond.Yuko radhi akatunze hela kwenye mambo ya kidunia kuliko kumpa huyu mzee.

    ReplyDelete
    Replies
    1. msiwe na haraka ya kuhukumu hamjui mambo yao. huyo baba anatafuta attention. hata kama anapewa hela hazitamtosha anachotafuta ni kuchukuliwa na Diamond atunzwe nyumbani kwake. na yeye hawezi kufanya hivyo kwa sababu hakuwa kwenye maisha yake tangu utoto hivyo ni kama mgeni kwake. kuzaa sio tija watu wanazaa na wanatupa. hapo swali ni kwamba ulihusikaje na maisha ya mtoto wako. unachopanda ndio unachovuna na si vinginevyo.

      Delete
  7. Hatumhukumu Dai lakini anapaswa kuangalia hili swala la kutoelewana na mzee wake,vinginevyo kama Mungu huwa anatoa adhabu na kusamehe kwa nini yeye anashindwa kumsamehe huyu mzee pamoja na kwamba amediriki kutafuta suluhu?Na mama naona anafurahia tu,tukumbuke hii ni dunia,sisi sote tunapita tu.

    ReplyDelete
  8. Sijui ni nguvu za giza anatumia huyu star wetu au laa,mbona kuna wasanii kama wakina Q'CHILLA wamepitia hayo na wamesamehe?kwa nini yeye inakuwa ngumu,au anadhani anafundisha nini jamii yeye akiwa kama kioo cha jamii?

    ReplyDelete
  9. Inaonekana nyie mliokomet upande wa d hamna radhi za wazazi wenu na huyo d soon ataokota madebe na ulimwengu utashangaa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. HAKUNA KITU KAMA HICHO!!! DIA ANGEKUWA MACHINGA JE??? NDIO IWE FUNDISHO KWA WANAUME WANAOTELEKEZA WATOTO.

      Delete
  10. Nyie yanawahusu nini......?Acheni kuingilia maisha ya familia za watu nyie. Mtoto usiyemlea unakula ujana na mademu tu huyo sio wako aje aamue mwenyewe kukusaidia au laa atakavyoona inafaa. Fundisho kwa mnaozaa zaa tu na kukimbiza watoto kwa bibi zao......zaeni na muwaleee shenzi type.

    ReplyDelete
  11. mbona mzee hajavua soxi kuonyesha miguu yake? hapo mzee anataka kaumchafua Diamond na Diamond anaelewa hivyo ndiyo maana kanyamaza kimya mzee amepata sana msaada kwa Diamond lakini mzee hatosheki na huyo daktari ni daktari feki ndiyo yule yule daktari wa akina Wema

    ReplyDelete
  12. baba Daimond vua soxi zako tuone kweli kama una matatizo na miguu, vua soxi ama sivyo wewe baba ni muongo unataka kumchafua Diamond tu, na wewe dokta feki tumechoka kusikia habari zako kwani wewe pia unataka ujulikane huwa unasema kila kitu feki unajifanya unaelewa kila kitu kwanza hata hapo hospital alipochunguzwa baba Diamond mbona kochi ni chafu sana hospitali hakuna makochi machafu

    ReplyDelete
  13. Samee mzazi mwenyezi mungu akusamee mangapi

    ReplyDelete
  14. Samee mzazi mwenyezi mungu akusamee mangapi

    ReplyDelete
  15. Huyu mzee naye naanza kumtilia mshaka kila kukicha habari zake kwenye mitandao....kuna msemo unasema 'fainali uzeeni' kwahiyo kuwa mpole tu maana umevuna ulichopanda

    ReplyDelete
    Replies
    1. SURE FAINALI UZEENI. TENA NASIKIA MZEE ALIKUWA NA PESA SANA ENZI ZAKE. ANAWAJALI MARAFIKI ZAIDI FAMILIA AKAISHITI SASA NINI? HELA ZAKE ALIKULA NA NANI??

      Delete
    2. Kila jambo linasababu zake hasa linapofanywa na mtu timamu!... naamini kabisa DIAMOND ana sababu ambazo naona watu wenye kiherehere wanataka sana kujua, na yeye kwa busara kaamua kukaa kimya. Huyu mzee sio mzima, kwanini shida zake kila kukicha anazianika mitandaoni tu? ni kweli aliwahi kumfuata Diamond amsaidie akanyimwa msaada? mbona hayo matukio ya kutoswa na Diamond hatuyaoni? alafu ni busara ya kawaida tu huwezi kuanika kila jambo la familia hadharani hivi! huyu mdingi anakosea, na napata wasiwasi anatumika na kama hatumiki basi hajielewi kama anakata tawi alilokalia. Baba kaa chini na mwanao mmalize tofauti zenu kimya kimya hatutaki drama zako kwenye mitandao banaaaaa!!! khaaaa!!! Kama ulimtelekeza or what hatutaki kujua hilo, bahati nzuri mama mzazi yupo! usitafute kiki za kipuuzi, kubali yaishe.

      Delete
  16. Yangu macho, hujafa hujaumbika!!

    ReplyDelete
  17. NAHISI DOCTA ATAJITANGAZA KIJANJA!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad