Watanzania Mil 39 Wanakunywa Mataputapu’, Mikoa Hii yaongoza kwa Wanywaji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Gazeti hilo limechapisha utafiti uliofanywa na shirika la Afya Dunia ‘WHO’ umeonesha kuwa 87% ya watanzania wanakunywa pombe za kienyeji, huku mikoa ya Dar es salaam na Kilimanjaro ikiiongoza kwa kuwa na wanywaji wengi wa pombe hiyo.

Mkoani Kilimanjaro eneo linaloongoza kwa wanywaji wa pombe hiyo ni Moshi, kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Tanzania ilikuwa na watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 44.9, hivyo 87% ya idadi hiyo kulingana na utafiti huo ni watu milioni 39.06.

Kulingana na gazeti la Jambo Leo limeeleza kuwa utafiti huo umebaini kuwa kwa sasa vijana wengi wanatumia pombe kupita kiasi kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu hali inayosababisha wakumbwe na magonjwa ya akili na kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu.

Matokeo ya utafiti huo yalitangazwa jana katibu mkuu wa chama cha wataalam wa afya ya akili Tanzania (MEHATA), Dk. Kissah Mwambene. Alikuwa akitoa mada kwa wabunge juu ya athari za matumizi za matumizi ya pombe iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanawwake ‘TAMWA’.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni aibu sana kwa taifa letu. Nashauri kuwa mataputapu, gongo na kila aina ya uchafu huu vipigwe marufuku kwani siyo chakula useme watakufa njaa.

    ReplyDelete

Top Post Ad