Kajala Aenda Kumlilia Mumewe Gerezani!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ hivi karibuni amekwenda kumlilia mumewe, Faraji Chambo anayetumikia kifungo cha miaka kumi na mbili gerezani.

Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Kajala, mwanamama huyo alitinga kwenye Gereza la Ukonga, Dar alikofungwa mumewe ambapo alipata nafasi ya kumjulia hali kisha kumwaga machozi akimuonea huruma anavyosota gerezani hasa akikumbuka walivyokuwa wakiishi kabla ya msala huo.

Katika safari hiyo, Kajala aliongozana na mwanaye, Paula Paul na mdogo wake Kajala ambao ndiyo waliokuwa wakimtuliza staa huyo ambaye alisababisha mumewe naye kutokwa machozi.
Akizungumzia ishu hiyo, Kajala ambaye wiki iliyopita alizindua filamu yake kali ya Sikitu alisema kuwa ni utaratibu wake wa mara kwa mara kwenda kumjulia hali mumewe huyo ila mara zote huwa anakwenda kimyakimya.

“Huwa nakwenda mara nyingi tu sema ndiyo hivyo huwa sipendi kuongozana na msururu mrefu, namshukuru Mungu anaendelea vizuri,” alisema Kajala. Machi 2013, Kajala na Faraji walihukumiwa ambapo Kajala alitakiwa kwenda jela miaka mitano au faini ya shilingi milioni kumi na tatu na mumewe miaka kumi na mbili au faini ya shilingi milioni mia mbili kwa kosa la kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar.

KajalacropHarusiHata hivyo, Faraji alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ gerezani huku Wema Sepetu ‘Madam’ akimlipia Kajala faini ya shilingi milioni kumi na tatu, iliyomnusuru kwenda jela.

Chanzo:Global Publishers
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. nyie wadaku kuweni na fact kabla ya kuandika uongo inajulikana mume wa kajala alienda jela miaka saba sio miaka kumi na mbili ndiyo mara ya kwanza nasikia miaka kumi na mbili wala si kweli, inajulikana Kajala angeenda jela miaka mitano na mume Wake miaka saba

    ReplyDelete
  2. Mdau wa hapo juu hujui ndiyo maana inaitwa"UDAKU"?Wanatitinganya habari hawazichunguzi kabla ya kuziandika wao ili mradi bora liende wasomaji na wahusika watajaza wao wenyewe

    ReplyDelete
  3. Ustaa wa kibongo ni shida tu,unakosaje shilingi million miambili??

    ReplyDelete

Top Post Ad