Kikwete amkabidhi Magufuli 'majipu' ndani ya CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwenyekiti mstaafu wa CCM Dkt Jakaya Kikwete, amekabidhi nafasi ya uenyekiti wa chama hicho kwa Dkt John Pombe Magufuli, huku akimtaka kushughulikia baadhi ya mapungufu yanayokitia hasara chama ikiwemo kuokoa mali za chama.

Kikwete ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Tanzania, ametoa hotuba yake ya mwisho kama mwenyekiti wa chama hicho leo katika mkutano mkuu maalum uliofanyika mjini Dodoma, na kutoa onyo kwa watu wote wanaoshikilia mali za chama kwa manufaa yao binafsi.

Akitaja baadhi ya mali hizo, Jakaya Kikwete amesema kuna wanachama ambao wamejimilikisha viwanja vya chama hicho bila utaratibu rasmi na kuwapa tahadhari ya kuvirejesha katika chama haraka.

Amemtaka mwenyekiti mpya mpya wa chama hicho kushughulikia suala la viwanja ambavyo bado havijapewa hati ili viendelezwe na kugeuzwa kuwa vitega uchumi na kuongeza wigo wa mapato ya chama.

“Mkoa wa Dar es salaam pekee una viwanja 279 lakini ni 45 pekee ndivyo vina hati angalau UVCCM wanajitahidi kujenga majengo ya vitega uchumi na kuna wazee wengine wa chama wameamua kujimilikisha viwanja vya chama, sisemi kwamba ni MAJIPU hapana, nawakumbusha ili viwanja hivyo viendelezwe, chama kipate mapato”
Aidha Kikwete amewakumbusha wakuu wa wilaya kuwa wanapaswa kutambua mojawapo ya jukumu walilonalo ni kulinda maslahi ya chama katika ngazi ya wilaya.

“Kuna wakuu wa wilaya wamesema eti wao ni wasomi na kwamba siasa haiwahusu, lakini wajue kuwa wao ni wajumbe wa kamati za siasa za wilaya, hivyo wajue kuwa wamewekwa kule kwa makusudi kama kiungo kati ya chama na serikali”
Amesisitiza kuwa ana imani kubwa kuwa Dkt Magufuli anatosha na ataweza kukisimamia vizuri chama hicho.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wizi wakubwa CCM
    Mmetuibia uwanja wetu wa uhuru Shinyanga mjini
    Mungu atawalani
    Kambarage na viwanja vingine nchini ni Mali ya watanzania

    ReplyDelete
  2. Pole
    Magu
    Majipu ya Salma
    Majipu ya Ridhiwani
    Majipu ya Kinana
    Majipu ya JK
    Majipu ya mtandao
    Kazi unayo

    ReplyDelete
  3. Balozi zote zitabaki dar
    Wamejenga ofisi mpya Leo wahame
    Fyuuu
    Wazungu si gozi gozi
    Hawahami dar ngoooooiiiii
    Si wajinga kama kwetu
    Kila ccm wasemalo ruhusa

    ReplyDelete
  4. Mila mwenye akili anaweza kueliewa safi hii kauli sababu ipo wazi kabisa.
    Iko kazi. Chama, maslahi binafsi, siasa.

    ReplyDelete

Top Post Ad