AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Taarifa zilizoripotiwa ni kwamba Koffi Olomide kaachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha siku mbili kati ya miezi 18 aliyohukumiwa awali, BBC imeripoti kuwa kuachiwa kwa koffi Olomide kumekuja baada ya Mahakama ya Kinshasa kusema kuwa hawakuona sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa Koffi Olomide kutokana na tukio alilofanya JKIA.
Pamoja na baadhi ya vyombo vya habari Afrika kuripoti kwamba Koffi alihukumiwa kifungo cha miezi 18 jela , Promoter wake wa nchini Kenya Jules Nsana amekanusha madai hayo na kusema kesi dhidi ya Koffi ilikuwa bado iko kwenye uchunguzi na kwamba baada ya uchunguzi wamebaini hakuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Koffi Olomide.
Promoter Jules amesema Olomide alimpigia simu akamtaka aombe msamaha kwa wakenya wote kwa niaba yake…..
’Koffi alinipigia mwenyewe baada tu ya kuachiwa na akaniomba niombe msamaha kwa wakenya kwa niaba yake, tumpe siku mbili, tatu atazungumza mwenyewe’
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
Wewe mkenya mbona sikuelewi!! Umuombee msamaha kwani yeye hana mdomo. Shida sitatuhuwa wajameni.
ReplyDeleteYaani mifumo mibovu sana. Eti hakuna ushahidi!! Dooh..Hii Kali!!
Delete