Mahakama Yamsaka Meneja wa Diamond ‘Babu Tale’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa hati ya kukamatwa kwa Hamis Tale ‘Babu Tale,’ ambaye ni meneja wa mwanamuziki wa bongo fleva, Diamond Platnumz, anaandika Faki Sosi.
Mahakama imetoa hati hiyo kutokana na Babu Tale kutotii amri ya mahakama iliyomtaka amlipe Shekhe Hamis Mbonde Sh. 250 milioni.

Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.

Kutokana na Babu Tale na mwenzake Iddi Tale kushindwa kulipa fedha hizo kama ilivyoamriwa tarehe 18, Februari  mwaka huu, mahakama ilitoa hati ya kukamatwa kwa wadaiwa hao tarehe 8 Julai mwaka huu.

Katika hati hiyo, mahakama ilimuelekeza Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala kuwa, hadi leo tarehe 19 Julai mwaka huu awe amewakamata wadaiwa hao ili wafike mahakamani kueleza kwanini wasipewe adhabu kwa kukiuka amri ya mahakama.

Shauri hilo limetajwa tena leo mbele ya Juma Hassan, Kaimu Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo ametoa hati nyingine kumuelekeza Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni kuwakamata wadaiwa hao.

Msajili Juma ametoa hati hiyo baada ya Mwesigwa Muhingo, Wakili wa Shekhe Mbonde,  kuomba hati hiyo ipekwe Kinondoni kwa kuwa Babu Tale anaishi huko na si Wilaya ya Ilala kama hali ya kwanza ilivyoeleza.

Tarehe 18 Februari mwaka huu, Jaji Augustine Shangwa, aliwaamuru wadaiwa kulipa Sh. 200 milioni  kama fidia ya kuvunja haki miliki ya Shekhe Mbonde na Sh. 50 milioni kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na kuvunja makubaliano.

Katika uamuzi wake Jaji Shangwa amesema, Juni 16, 2013, Mbonde aliingia makubaliano na wadaiwa hao na wenzake ya kufanya biashara ya kurekodi mawaidha na kutengeneza nakala DVDs kwa ajili ya kuziuza nchini.

Wadaiwa hao waliahidi kumjengea nyumba, kumnunulia gari na kuitangaza kazi yake pia walimpa Sh milioni mbili na kumnunulia kanzu na kofia (baraghashia) na kurekodi DVDs zenye ujumbe Uzito wa Kifo, Fitina Juu ya Wanawake, Umuhimu wa Swala, Mwanadamu Yumo Ndani ya Hasara na Maadui wa Uislam.

Amesema, makubaliano ya awali yalikuwa kurekodi halafu baadaye wakubaliane kuhusu bei na jinsi ya kuziuza, badala yake waliziuza na kuzisambaza nakala hizo na kujipatia faida bila kumshirikisha Mbonde ambaye alitumia ujuzi wake.

Mbonde kupitia wakili wake Muhingo, Gwamaka Mwaikugile na Clement Kihoko,  alifungua kesi ya madai namba 185/2013 akiiomba mahakama iamuru wadaiwa wamlipe Sh. 700 milioni kama  fidia ya kuvunja makubaliano na Sh. 50 milioni kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na kuvunjwa kwa makubaliano.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na bado anguko kuu linakuja kwenu nyie wachafu sijui wasafi dhulma ni kitu kibaya sana...

    ReplyDelete

Top Post Ad