Nina Furaha Toka Nitoke CCM - Edward Lowassa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lowassa kupitia ukurasa wake wa Facebook ameelezea furaha yake namna ambavyo ameimarika zaidi baada ya kujitoa ndani ya CCM hadi sasa ambapo ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

''Nina furaha kutimiza mwaka mmoja toka nilipojitoa CCM na kujiunga na CHADEMA.Uamuzi ule haukuwa rahisi,lakini kwa ushupavu, ujasiri na mwongozo wa Mungu nilifanya hivyo. Nilifanya uamuzi wa kihistoria katika nchi yetu'' Amesema Lowassa.

Ameongeza kuwa watanzania bado wanataka mabadiliko na hali hiyo imezidi kuthibitika kuwa wananchi hawawezi kuyapata ndani ya CCM .

Amesema watanzania wanataka sera na mtu mbadala wa kuongoza mabadiliko hayo na kwamba vyote hivyo watavipata ndani ya CHADEMA na UKAWA kwa jumla.

Aidha amewataka watanzania wanaomuunga mkono na ambao walihama CCM kwa ajili yake waendelee kumuunga mkono na kuiunga mkono CHADEMA.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Eti Edo anafuraha jamani gia zingine ni shida tuu, Mbona alichelewa anakumbuka shuka asubuhi angejitoa CCM pale alipo kuwa bado kijana sasa hivi mguu mmoja kaburini na mwingine dunia

    ReplyDelete
  2. HAHAHAHAH!SIASA BONGO NI MIPASHO.

    ReplyDelete
  3. Eeh mara mwaka,powaaaaa!uzuri kwa sasa wote tunaisoma namba.
    Tumeimbiwa kwamba tutaisoma namba wee na imekuwa hivyo,tukubali kwa kutoa ushirikiano sio kupingapinga tuuuuuuuuuuuuuu,haipendezi.

    ReplyDelete
  4. MABADILIKO MAGUFULI KAANZA KUYALETA MBONA?KWA SANA TU BABA NA KUNA TOFAUTI KUBWA HATA WAKATI WEWE UKIWA WAZIRI MKUU,AU PENGINE NYIE AMBAO MKO MAISHA FULANI SIO RAHISI KUGUNDUA LAKINI SISI WALALA HOI TUNAIONA TOFAUTI KUBWA NA TUNAAMINI BAADA YA MUDA HALI ITAKUWA NZURI SANA,TUVUTE SUBIRA,TUJITUME KUFANYA KAZI.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeona eeh,
      Zile sherehe za kuanzia january mpaka december Kwa maana mara birthday,get together,na nyingine huku mitaani kwishaaaaaaaaaaaaaa.CHEZEA MAGUFULI WEWE!

      Delete
    2. Ha ha haaaa, mabadiliko tunayaona bwanaaaa.... vyuoni wanafunzi wanaondolewa eti credit hazitoshi, sasa huku mtaani wakijazana tutawapeleka wapi!? wakati wanasoma kwa pesa za wazazi wao sasa serikali inawashwa na nini!!! too much kufuatiliana sasa da!!!

      Delete
    3. Kwa kweli wewe Anonymous 2:38 PM yaani umenifurahishaaaaaaaaaa, nakupe bureeeee lol hahahahahahahahahahaha....................

      Delete
  5. ---Safari ya matumaini.
    ---Operation (UKUTA)= HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete
  6. Lowassa Ni raisi ajaye

    ReplyDelete
  7. Hongera baba
    Mungu akupe maisha marefu

    ReplyDelete
  8. ICU Inawahusu,Na kwa sasa mnapumulia machine ya CUF.

    ReplyDelete
  9. ACHANA NA CCM MAANA ILISHAKUTOSA,
    HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  10. SAWA BABA,ILA SASA INABIDI 2020 ASIMAME MWINGINE SIO WEWE TENA HUKUBALIKI NA WALA HUWEZI KUSHINDANA MA MAGUFULI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asisimame yeye vepe...na ile hela yake yote alotoa ndio iende na maji hifihifi......NO, HAPANA, atasimama yeye edo hata kama atajinyea tena pouwa tu........kwani hujui kama piipooozz PPWWAAAA

      Delete
  11. Hahahaa lazima uwe na furaha lowa hasa ulovyokuwa ccm hao yote mabaya walikuwa wanakuita hao chadema yaani mwizi, fisadi na mengine unayajua mwenyewe huko sasa huitwi tena yaan mtu Safi sasa wewe hahahaha pole edo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeonaeh! Hivi sasa huko aliko yeye ni 'mtakatifu', hao hao walompachika jina la fisadi hivi sasa 'wanang'ata maneno' hawathubutu tena kulitamka hilo jina, wanakula matapishi yao......amakweli Mungu hamfichi mnafiki......

      Delete

Top Post Ad