Rais Magufuli Atoa ONYO Kali....."Mimi sijaribiwi, wasije kunijaribu. Atakayeleta vurugu atashughulikiwa bila huruma!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Julai, 2016 ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo amezungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana  na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.

Akiwa Mkoani Singida, Rais Magufuli aliyeongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli amewasihi watanzania kufanya kazi kwa juhudi na kujiepusha na vitendo vya vurugu vinavyohamasishwa na baadhi ya wanasiasa huku akionya kuwa serikali yake haitamvumilia mtu yeyote ambaye atathubutu kuchochea vurugu ikiwemo maandamano kinyume cha sheria.

“Sitaki nchi hii iwe ya vurugu, watakaoleta vurugu mimi nitawashughulikia kikamilifu bila huruma, na wasije wakanijaribu, mimi ni tofauti sana na kama wapo watu wanaowatumia wakawaeleze vizuri, mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa.

“Wananchi hawa wana shida, na siasa nzuri ni wananchi washibe, siasa nzuri ni wananchi wetu wapate dawa” Amesema Rais Magufuli.

Kuhusu hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali yake ya awamu ya tano tangu aingie madarakani Rais Magufuli ametaja baadhi ya  hatua hizo kuwa ni kufuta ada kwa shule za msingi na sekondari, kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu zaidi ya laki moja na kuongeza fedha za miradi ya maendeleo katika bajeti ya serikali kutoka asilimia 26 ya mwaka 2015/2016 hadi kufikia asilimia 40 katika bajeti ya mwaka huu 2016/2017.

Hatua nyingine ni kuondoa wafanyakazi hewa 12,500 katika orodha ya waliokuwa wanalipwa mshahara na serikali, kudhibiti upotevu wa mapato serikalini, kutenga shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani Standard gauge na pia akazungumzia hatua zilizochukuliwa dhidi ya wala rushwa na wanaojihusisha na ufisadi kwa kuunda mahakama ya mafisadi huku akiapa kuwa katika kipindi chake hakuna fisadi atakayeendelea kutamba.

Akiwa njiani Rais Magufuli amewasalimu wananchi wa Ikungi na baadaye amefanya mkutano wa hadhara Singida Mjini ambako amesisitiza kuwa serikali yake haiko tayari kumvumilia mtu yeyote atakayekwamisha utekelezaji wa Ahadi na Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Singida

29 Julai, 2016

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndugu Raisi, Mbona hata ukawa wamechaguliwa na Wananchi hawahawa. Ndugu Raisi wamechagulia pia kuwatumikia Wananchi hawahwa. Wamechaguliwa na Wananchi kwa mujubu wa sheria za nchi sasa tatizo liko wapi? Mtu mmoja hawezi kwenda kote nchini kutatua matatizo ndio maana kuna ngazi toka chini mpaka juu. Wewe ni kiongozi wa ngazi ya juu sana. Kwa nini uwe ni wewe tu badala ya kuhakiki viongozi waliochaguliwa na vyama vyote wanauhuru wa kutekeleza kazi zao kama wewe. Sasa kama ni hivi usizuie kazi zao.Sasa hili tatizo mbona sio tatizo.Inashangaza Kwa kweli. Watu wengi wasomi na Wasiosoma wanalishangaa Taifa kufikia hapa tulipo.Ni siasa chafu bado inatembea Tanzania badala ya kuwaachia huru Watanzania watende kazi zao. Mbona Wageni hamuwabani na ni wao wanaofaidi nchi.Ulianza vizuri, tulifiri mambo safi. Sasa ukali niachieni, hii nchi ya mamilioni Watanzania kila mtu inampasa awajibike vizuri kwa nguvu kwa pamoja. Si mtu mmoja. Sitaki kutumia neno baya, lakini inafikia wakati inabidi Watanzania tujiulize haya mambo. Ningependekeza kukaa chini na Wapinzani na Wanaheria kutatua hili jambo kufuatana na sheria za nchi. Tuache kuendesha Taifa kama nyumba binafsi. kila nyumba kunatofauti. Kila kabila kuna shearia zao. Lakini kitaifa wote tunaongozwa na sheria moja. Ukali haulipi. Kusikilizana , kuelewana, ndio kutatupeleka mbele. Watu wanashtuka sasa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Waende kwenye majimbo yao wakahimize maendeleo hakuna atakaewasemesha,maandamano ya nn nchi nzima?? wacheni watu wapige kazi wacheni uchochezi bana.

      Delete
  2. Sawa sawa Raisi wetu mpendwa, wamekaa kimaslahi hawana lolote hao bali longo longo nyingi za kutaka kukukwamisha wapoteze tu na uwashughulikie kiupasavyo haswa mueshimiwa. Wanakuona uko kimya ndio wanataka wakujaribu

    ReplyDelete
  3. Sawa sawa Raisi wetu mpendwa, wamekaa kimaslahi hawana lolote hao bali longo longo nyingi za kutaka kukukwamisha wapoteze tu na uwashughulikie kiupasavyo haswa mueshimiwa. Wanakuona uko kimya ndio wanataka wakujaribu

    ReplyDelete
  4. Misingi ya utawala ni sheria za nchi, kwa hiyo pande zote mbili zingatie hayo na utulivu utakuepo tu.

    ReplyDelete
  5. Misingi ya utawala ni sheria za nchi, kwa hiyo pande zote mbili zingatie hayo na utulivu utakuepo tu.

    ReplyDelete
  6. Shida kufikiri.vilaza.

    ReplyDelete
  7. Alimkataza Lowasa kutoa ahsante mikoani. Umesahau.kauli hazoeleweki.unaminya kila uhuru. Watanzania wenye amili hawaongei.wanangojea lipi tena uraliibua.

    ReplyDelete
    Replies

    1. Lowasa atoe asante kwa lipi kama sio vurugu?kwani yeye kachaguliwa na wananchi kuwa rais?

      Delete

Top Post Ad