Trafiki Wakusanya Milioni 320 Kwa Siku Nne DSM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam limekusanya shilingi milioni 320.2 ambapo fedha hizo ni kutokana na tozo za makosa ya usalama barabarani.

Askari wa kikosi cha usalama barabarani Jijini Dar es salaam akiwa kazini.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Kamanda wa wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema fedha hizo ni kutokana na makosa 10,676 ambayo yamefanywa na watumiaji wa vyombo vya moto.

‘’Toka tarehe 25 hadi tarehe 28 tumefanikiwa kukusanya kiasi nilichotaja ambapo makosa mengi ya madereva wa bodaboda tumeanza kuona kwamb tunapowatoza faini ya elfu 30 au 60 haiwapi fundisho lolote ndiyo maana tumekuwa tumekuwa tukiwapeleka mahakamani ili kupunguza matukio ya uvunjifu wa sheria barabarani’’ Amesema Kamanda Sirro

Aidha Kamishna Sirro ametumia wasaa huo kuwataka watanzania kutii sheria bila shurti wanapokuwa wanatumia vyombo vya moto barabarani na katika maeneo yao ya kuishi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wananchi tunaomba trafiki wapewe mashine za tra zile za electronic maana wengi wao wanachukua hizo faini ukidai risiti anakwambia twende kituoni nikakuandikie hapa sina risiti. Mchezo huu wanao zaidi trafiki WA Dodoma.

    ReplyDelete
  2. Hii maana yake nini?? Tunazuia ajali au kukamata huku na kupiga faini ni imekuwa chanzo cha kipato kwa jeshi la Polisi??? Mi nilidhani mnafanya jitihada kuzuia matumizi hatarishi ya barabara ila kwa mwelekeo huu ni kama vile kwenu ninyi polisi ni dili!

    ReplyDelete
  3. TRA nyingine

    ReplyDelete

Top Post Ad