Zitto Kabwe afunguka haya baada ya Rais Magufuli kukabidhiwa uenyekiti wa CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Leo July 23 2016  Rais John Pombe Magufuli amekabidhiwa rasmi nafasi ya uenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM   baada ya kupigiwa kura za ndio 2398  kutoka kwa wanachama wa chama hicho ambapo hakuna kura hata moja ya hapana wala iliyoharibika

Baadhi ya viongozi wakiwemo wa vyama vya upinzania walishiri akiwemo mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema, lakini wapo pia waliotamani kufikisha hisia zao kuhusu tukio hilo na mmojawapo ni mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe kupitia account yake ya facebook aliandika maneno haya…

>>’Napenda kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa Chama chake cha CCM akiwa Mwenyekiti wa Tano chama hicho. CCM imeendelea kudumisha utamaduni wa kukabidhiana Uongozi kila baada ya muda‘

‘Jambo ambalo ni la kujifunza hasa kwa vyama vya Siasa nchini na barani Afrika. Nataraji kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona umuhimu wa Vyama vya Siasa kuendelea kufanya Siasa bila vikwazo na kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.’ –Zitto Kabwe

‘Demokrasia inaimarisha Amani kwa kupaza sauti za HAKI. Karibu kwenye changamoto za kuongoza Vyama vya Siasa ndugu Rais.‘ –Zitto Kabwe
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Upinzani c kubeza au kulaumu kila kitu. Penye kuhitaji pongezi msisite, penye kuhitaji kukosoa karibuni, hii ndiyo siasa yenye afya kwa mustakabali wa demokrasia nchini kwetu. Nakupongeza sana Kiongozi Mkuu kwa comment na salaam zako kwa CCM nadhani unawapa funzo wale wenye mawazo hasi kutoka upinzani.

    ReplyDelete
  2. Pengine atakupangia kazi, zidi kujikommba!!

    ReplyDelete

Top Post Ad