Cheyo Awataka Watanzania Waungane Kuyakataa Maandamano ya Chadema

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo amewataka Watanzania kupaza sauti na kukataa maandamano ya Septemba Mosi mwaka huu ambayo yameandaliwa na Chama cha Demokrasia (CHADEMA).

Cheyo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu msimamo wake juu ya maandamano hayo.

“Watanzania wenzangu jambo la kuwaacha watoto wetu kwenda kupambana na Polisi si jambo zuri, wote tupaze sauti zetu na kusema hapana kwa maandamano ya Septemba Mosi,” alisisitiza Cheyo.

Alisema kuwa, ziko njia mbalimbali ambazo Chadema wanaweza kuzitumia kutatua migogoro, kama vile meza ya mazungumzo na kuachana na maandamano ambayo yanachochea vurugu na hata kutishia amani ya nchi.

Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi linapotoa katazo la maandamano ni lazima utii uwepo, kwani Polisi wapo kwa mujibu wa Sheria na Katiba. Ikiwa Chama hicho hakikuridhika na katazo hilo basi wanatakiwa kuonana na Waziri anayehusika na Jeshi la Polisi.

Akifafanua zaidi alisema kuwa Rais Magufuli amekuwa akichukua hatua za makusudi za kutatua matatizo mbalimbali kama vile kupambana na ufisadi, ambapo viongozi wengi wa Serikali wamesimamishwa kazi au kufukuzwa kutokana na kujihusisha na masuala ya rushwa.

Mwenyekiti huyo wa UDP amewataka watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli ili aweze kutimiza ndoto zake na yale ambayo ameyaahidi kwa ajili ya nchi ya Tanzania.

Aidha Cheyo aliwasifu viongozi wa Dini ambao walikaa na Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kukubali kurudi bungeni bila pingamizi lolote.

Amewataka viongozi hao wa dini kuendelea kuzungumzia suala la amani kwa Watanzania na Viongozi wa kiasa ili kudumisha amani ya nchi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watu wanafuata mkumbo tu hawajui nini walisemalo au walitendalo kwani hawajui nini madhara ya vita vya wenyewe kwa wenyewe(civil war)huwa wanasikiaga au kuona news katika luninga kuhusu nchi zenye kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe wakati huo wa zamani nilishuhudia mwenyewe kwa macho yangu siyo kwa kuambiwa au kusikia mgogoro kama huo ulipotokeaga nchini Msumbiji(Moçambique)kuanzia miaka ya mwishoni mwa 1970 vita vilivyodumu takribani miaka 13 hivi kati ya FRELIMO(Enzi hizo chini ya uongozi wa hayati"SAMORA MOSES MACHEL"kuna baadhi yenu mlikuwa bado wadogo sana kuelewa na baadhi yenu mlikuwa bado hamjazaliwa wakati huo sisi tulikuwa tuna-cross toka bongo kupitia Mtwara tunauvuka mto wa Ruvuma kuingia Msumbuji kuelekea Maputo kuzifuata meli na huku ile nchi ipo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mambo tuliyokuwa unyama ukatili uliokuwa unatendeka watu kupoteza maisha watu kuwa vilema njaa hakuna madawa hospitalini yaani Mungu apishie mbali balaa kama hilo lisije kutokea Tanzania kwani vita vya wenyewe kwa wenyewe mvisikie hivyo hivyo tu ndugu zangu tamaa za wachache kwa kutaka madaraka zitakuja kuwaponza mamilioni ya watanzania wasiokuwa na hatia hasa wanawake na watoto jaribuni kulitafakari suala hili kwa kina na siyo tu kijuu juu gharama yake ni kubwa sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa hiyo hatutaki mtu tuliye mchaguwa ageuke mungu mtu
      Kila alisemalo , atakacho aminicho nasi tuabudu
      Lazima tuishi kwenye misingi ya kushauliana na kukusoana
      Mtu hashauriki hata na wale waliomtia madarakani
      Fyuuuuu

      Delete

Top Post Ad