Diamond: Nimenunua nyumba SA, nimechoka kuhangaika hotelini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya kudai kuwa ana nyumba Afrika Kusini na haoni sababu ya kununua nyumba nchini Marekani , Diamond amefunguka sababu iliyomfanya anunue nyumba nchini humo.

Mapema mwezi April mwaka huu, alipohojiwa kwenye Stori Tatu ya Planet Bongo, inayoruka kupitia EA Radio, Diamond alisema, “Sina sababu ya kusema ninunue nyumba Marekani. Ninunue nyumba Marekani kwa sababu gani? Kwanza sipapendi, uongozi unajua kabisa.”

Akiongea na Times FM, hitmaker huyo wa ‘Kidogo’ amesema kuwa sababu iliyomfanya yeye kununua nyuma Afrika Kusini ni kutokana na kuchoka kuhangaika kwenye hoteli kupanga wakati anapokuwa nchini humo.

“Mimi mwenyewe kwanza nipate urahisi wa makazi nikiwa kule, nimechoka kuhangaika mahotelini,” amesema Diamond. “Lakini familia yangu ipo kule, mwanangu Tiffah na mwingine ambaye anakaribia kuja kwahiyo nawawekea mazingira bora wasije kuona kwamba baba anazalisha tu.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. YES UKO VIZURI SANA DIAMOND!!! I LIKE YOUR LIFE STYLE!!!

    ReplyDelete
  2. mama yao si anayo nyumba ????

    ReplyDelete

Top Post Ad