Hali Ngumu ya Maisha, Afisa wa Polisi Ajiua Kwa Kujipiga Risasi Jomo Kenyatta (JKIA)

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Afisa wa polisi Caudencia Wausi alimejiua kwa kujipiga risasi kichwani katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) muda mfupi baada ya kuchapisha ujumbe wa kuashiria kuwa na mahangaiko maishani.

Koplo Caudencia Wausi alitumia bastola yake aina ya Jericho kujifyatulia risasi kichwani ndani ya choo dakika 13 tu baada ya kuchapisha ujumbe katika mtandao wake wa Facebook.

"Maisha ni magumu unapoishi katika ulimwengu ambapo kila mtu anapanga kukufanyia maovu.. na utafanya nini wakati ambapo huwezi kuvumilia au hauna uwezo wa nguvu za kuwatia nguvu wapendwa wachache katika maisha yako.!? hauna lingine la kufanya ila... kwa hivi nisadie Mungu "aliandika kwenye Facebook.

Kwa mujibu wa mkubwa wake, Bi Wausi alikuwa amerudi kazini kutoka mapumzikoni kabla ya kujiua baada ya kujifungia chooni, JKIA.

Inadaiwa alijifungua mkanda wake wa polisi na kuuacha katika chumba cha Control Room pamoja na fimbo yake kabla ya kujifungia chooni.

"Tulisikia tu mlio wa risasi na baadaye tukampata juu ya choo huku bastola yake ikiwa mkononi, alikuwa tayari ameaga dunia "alisema kamanda wa polisi katika uwanja wa ndege Rono Bunei.

Bwana Bunei alisema kisa hiki kimeshtua wenzake kwasababu afisa huyo hakuwa na dalili za kusongwa na mawazo.

" Alikuwa anapiga gumzo na wenzake asubuhi na nilimuona mwenye furaha, hakuonyesha dalili zozote za kuwa na mahangaiko "alisema Bw Bunei na kuongeza kuwa uchunguzi umeanza kubaini kilichosababisha afisa huyo kujiua.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mbele yake nyuma yetu.

    ReplyDelete
  2. Mungu amuurumie kwa uhamuzi alio uchukua na kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.Mwenye hukumu ya kweli na ya mwisho ni mwenyezi Mungu tu wengine ni wababaishaji, akiwemo na mimi.
    JB USA.

    ReplyDelete

Top Post Ad