Kimenuka..Mbowe Awekwa Katika Orodha ya Wadaiwa Sugu wa NHC, Mwenyewe Adai ni Njama

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nimepata taarifa ya mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Waandishi wa habari kuhusu kilichoitwa “wadaiwa sugu” wa NHC ambapo katika orodha hiyo kampuni ambayo nina hisa ya Mbowe Hotels Co.Ltd imeorodheshwa kama mdaiwa anayedaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni moja.

Nakiri kuwepo kwa mgogoro wa kibiashara wa miaka mingi baina ya Kampuni hii na NHC. Aidha kampuni hii imekuwa ikilipa kodi stahiki kwa NHC kwa mujibu wa makubaliano yetu ya kibiashara.

Kumekuwepo na ukakasi wa muda mrefu kuhusiana na mkataba wetu wa umiliki, uendelezaji na uendeshaji wa jengo hili unaochagizwa na msimamo wangu wa kisiasa.

Haki na Uhuru wetu wa kufanya biashara kama raia wengine umekuwa ukiingiliwa mara kwa mara katika mazingira yanayoambatana na Vitisho kiasi ambacho Maamuzi kadhaa hayafanyiki kwa hofu ya kisiasa kwamba “Itakuwa kumwongezea nguvu Mpinzani”. Hivyo, ningependa umma wa Watanzania uelewe kuwa sidaiwi na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC). Kufuatia utata huu wanasheria wa Kampuni wanashughulikia jambo hili kwa taratibu za kibiashara na kisheria.

Naomba kuweka wazi kwa yeyote anayehusika. Sitafungwa fikra, sitafungwa mdomo na sitaacha kuutetea Ukweli, Haki na Demokrasia katika nchi hii kwa misingi ya “kulinda kinachodhaniwa ni maslahi yangu ya kibiashara”. Wafanyabiashara wengi wanafungwa fikra na midomo ndani ya nchi hii kwa kuogopa hila na ghiliba za watawala.

Ni heri kufa masikini nikiwa nimesimamia ukweli, kuliko kuishi tajiri niliyetawaliwa na ubinafsi, woga, hofu na ubatili.

Natambua kuna jitihada za kutumia kila silaha na kila hila dhidi yetu katika Kipindi hiki.

Mwisho, Natoa rai kwa wanachama na wapenzi wa Haki katika Taifa hili, wasiogope. Haki itaweza kucheleweshwa kwa muda tu, lakini kamwe haiwezi kuzuiwa. Binadamu akikufungia mlango Mungu wa Haki atakufungulia dirisha.

Ubatili ni wa mpito lakini Haki ni ya milele.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

24 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watatapatapa sana
    Tatizo lao ni vilaza wa kufikiri
    Wamezoea vijembe, umbea, uzushi, uchochezi
    Ndo hadi Leo hawajiamini
    Lowassa na Sumaye wanatesa sana
    Yote wivu tu Mbowe mwenyekiti wetu
    Usiwe a Shaka

    ReplyDelete
    Replies
    1. kilaza mkubwa kama anadaiwa si akalipe, vijembe na umbea viko wapi hapo wakati anatakiwa akalipe deni la NHC? na bado zile alizoficha China nazo mpaka zirudi, na huyo lowassa na mr. o wanatesa nini wakati wanakaa kwa wasi wasi ya kutufilisiwa?

      Delete
    2. Koma wewe huna Kazi
      Kazi kujitia kada wa CCM
      Kusifia walipewa madaraka
      Unafiki Magu atakupa cheo sahau mtabaki hivyo hivyo kuninyinia mitandaoni kujibu
      Upunbavu na u
      Umbea na kuhack wana CCM wenzenu waonekane wabaya

      Delete
  2. Wasikunyime usingizi
    Wenyewe kwa wenyewe hawaelewani
    Leo wanaponda awamu ya nne ilyowaweka madarakani
    Naaza kupata picha kwanini wametawala miaka zaidi ya 50 Tanzania
    Hakuna maendeleo
    Chama kimejaa wezi, waongo, wambea,
    Wazuchi
    Wameiba Mali zote za watanzania na kujitisisha lakini bado omba omba

    Ukiwa mfanya biashara Upo upinzani shida Tanzania
    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  3. Wanasiasa wetu bhana ni kiboko sasa Mbowe uachwe kushughulikiwa na kudaiwa kisa mwanasiasa ukidaiwa unasema njama kwa hiyo Mbowe tuthibitishie kuwa madai hayo ni ya uongo na hudaiwi sio blah blah

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mungu ni mwema,na jee wangepewa nchi si tungenyonywa mpaka kope?wangegundua wafanyakazi hewa hawa kweli?wangelipa kodi?
      Wanakera na hawajiongezi.

      Delete
    2. Pumbavu wewe na wote wanakusapport
      Kwa lipi kwanza mmeiba agenda za ukawa Leo mnatamba
      Na tunajuwa CCM wenyewe mnasaliti Magu
      Kwani wengi wenu ni mafisadi papa
      Namuonea huruma Magu bora angehamia ukawa ndoto yake ingefanikiwa

      Delete
  4. Wapinzani wanatumika na mataifa ya nje, tusipokuwa makini tunauana wenyewe kwa wenyewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau, umesema, Hawa wapinzani wanatumika na mataifa ya nje yaliyoendelea tena Yale mataifa wasiopenda kuona bara hili la Africa likinyanyuka kwani hawapendi Kabisaa!!!! Wanapenda kuwaona wafrica wanatabika, wanangaika wanauwana, ili waendeleee kufaidika na Mali asilia wanazozipata katika bara hili, ndio maana kutwa kuwachochea wafrica, wakishaona kuona uongozi mzuri tu hawapendi, watawachochelea wale wajinga wajinga weee mpkaaa, Nayo hii inachangia bara hili kuporomoka, Kila siku siasa tu za ujinga ujinga, baadara ya kufanya kazi kwa maendeleo na mustakabali wa Taifa Bali ndio haya Kila siku, wakati huko kwao, Kuna muda wa siasa karibu na uchaguzi, ukishaa basi, iliyobaki ni kazi, tena kwa kushirikiana siasa mpka muda wake tena wa uchaguzi ukianza, lakini huku Kwetu Kila siku ndio hayo hayo, tuna matatizo sana sisi wafrica

      Delete
    2. Any.1.33 Pitia kwa mangi ukapate juice ya ukwaju.
      Nchi imeshaanza kuwa na adabu,tunafanya kazi,tunawahi kazini,kila mtu anaogopa rushwa nk.sasa badala ya kuendelea na HAPA KAZI TU eti tuendekeze siasa na maandamano yasio na tija.WATATUCHEKA.

      Delete
  5. Toa mikataba na vielelezo vyako,uone kama utafatwafatwa.
    Kwani mbona wengi wameipata pata kutoka NHC kutokana na sera ya HAPA KAZI TU ya awamu ya 5?
    nikiwemo mimi mwenyewe sehamu yangu ya biashara?
    ACHA VIJISABABU VYA KIS....

    ReplyDelete
  6. Hahahahah!Hiyo haimo Mbowe,na uache visingizio.KAWAJIBIKE.

    ReplyDelete
  7. unadaiwa bana na NHC, Hivi mchechu ni kichaa aongee na waandishi wa habari kuwa unadaiwa???? Mbowe acha siasa zako lipa deni hili ni shirika linalojiendehsa na fedha hizo za kodi.

    Hata hivyo umevumiliwa saana, lipa deni hacha porojo mbona wengine hawajatoka povu na ni taasisi za serikali.

    acha bana kila kitu sio siasa, nyie ndio mnarudisha maendeleo ya nchi nyumba. lipa deni lako.

    ReplyDelete
  8. Ni kweli unadaiwa bhana na unatuangusha sana maana Uliapa kuwa kazi yako ni kuhuisha uzalendo,uadilifu,na awajibikaji katika uongozi wa nchi,KUIMARISHA AMANI,UMOJA NA MSHIMAMANO WA TAIFA ambao ndio msingi Mama wa kuleta maendeleo ya jamii TZ.Hapo je?kutolipa kodi ndio uadilifu?Mkuu umechemka>

    ReplyDelete
  9. HAPA KAZI TU INAHUSIKA NA SI VINGINEVYO.LIPA DENI NDIO DAWA,
    NANI AMWAGE UNGA WAKE KWA KUKULINDA WEWE NA MADENI YA MUDA MREFU?

    ReplyDelete
  10. hata kama una deni..kula..lala..kwani kuwa na deni imeanza kwa MBOWE?Serikali zenyewe zinadaiwa..hakuna news hapo..msituchoshe.

    ReplyDelete
  11. DENI SI LINAONEKANA?KAMA UMELIPA ONYESHA USHAHIDI.

    ReplyDelete
  12. Kwa fikra umefungwa babu,labda mdomo ndio hujafungwa.
    Kitendo cha kupanga maandamano 01/09/2016 alhamisi siku ya kazi ni kufungwa fikra,yaani hata kama maandamano yangekuwa kihalali.

    ReplyDelete
  13. MASKINI MBOWE!DAAAAAAAAAAAAH
    YAANI JAMANI MPAKA NAMKUMBUKA DK.SLAA.

    ReplyDelete
  14. Yeah,TZ kwanza Mbowe baadae,
    lipa deni watu tupate mikopo tutakaporudi vyuoni babangu eeh.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pumbavu nyote na ofisi za serikali nazo zifungwe
      Mbowe haami Kama mnategea kukodi pale CCM
      Mmeula na chuya kapigeni disco Msoga au Chato

      Delete
  15. Kelele zote hizo Mbowe kumbe unayako mengi uliyoyaficha. Sasa nenda tu kalipe madeni kabla ujaumbuliwa zaidi. Majipu mengi yamejificha Chadema sijui hao wanaowaunga mkono hawana macho au akili......

    ReplyDelete
  16. Kwa hii awamu ya tano dawa ni kulipa tu.Hakuna ukanjanja.

    ReplyDelete

Top Post Ad