Makonda awafungukia walionukuu kauli yake vibaya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amefafanua juu ya kauli yake aliyoitoa hivi karibuni ambayo imekuwa ikinukuliwa vibaya na vyombo vya habari ikiwemo gazeti la leo la Mwananchi.

Kwenye ukurasa wa tatu, gazeti hilo limeandika habari yenye kichwa kinachosomeka, “Makonda ataka wahalifu wagongwe, wapigwe.”

Akiongea na Clouds 360 ya Clouds FM, Makonda amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanapenda kuwagombanisha wananchi na viongozi wao kutokana na kauli wanazozinukuu kutoka kwao.

“Unajua kuna baadhi ya wenzetu wana agenda zao tofauti na agenda ya kujenga taifa, watu ambao wangependa kuwatengenezea mazingira wananchi wasielewane na viongozi wao,” amesema Makonda.

“Kwa sababu ukiangalia hii stori ilivyoandikwa kuna kitu kimewekwa ambacho hakipo kabisa lakini kimewekwa kwa tafsiri ya kumsaidia mwenye kusudi la kufikisha ujumbe tofauti na ule uliotolewa,” ameongeza.

Aidha Makonda ameendelea kwa kufafanua kauli yake hiyo iliyonukuliwa vibaya kwa kudai kuwa, “unapokuwa msituni ni sawa na mapambano lazima upambane kwa kuwalinda polisi wako, majambazi siyo watu wazuri kutokana na tukio lililotokea la kuuawa kwa polisi wanne hivi karibuni.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hahahahahaha dhaaa

    ReplyDelete
  2. Jitumbuwe mwenyewe
    Tumechoka
    Leo msaada bakwata
    Kesho mpango wa makonda hospital kubwa
    Nimeibiwa simu
    Polisi piga wahalifu
    Ili mradi kila kukicha tusome
    Habari zako tumechoka
    Fanya kazi basi
    Hata ukija hapa tunajuwa una jambo muhimu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona wewe kutwa mitandaoni,na wewe unachosha vilevile.

      Delete
    2. KWANI UMEONA MAKONDA HAFANYI KAZI?ANAKULA KWAKO?FYUUUUUUUUUUUU.

      Delete
    3. Naona ndo nyinyi mlomwibia simu shoga yenu
      Fyuuuuuiuu

      Delete
    4. Mtakalia upambe wa viongozi wa ccm mkitegemea Magu atawapa cheo wengine mlikuwa team lowassa , team membe , team Sitta
      Leo team Magu
      Fyuuuuu
      Magu siyo mjinga
      Mtatangatanga kila kona kujitia makada wa CCM
      Nyinyi nyote ni makada uchwara fyuu
      Kazi kuranda mitaandaooni kujashifu wapinzani na kuhack wana CCM wenzenu
      Mimi hambu patio ngooioiooiioo

      Delete
    5. Msitumie ma RC na DC
      Kupata connection na Magu
      Nyinyi ni mtu kitu na si makada kazi yenu kupiga mizinga kwa watanzania
      waishio nje kila kukicha kwenye mitaandao

      Delete
    6. Kujitia mnajiua sana CCM
      Eti fulani kauza viwanja vya CCM
      Kumbe viwanja vyenywe ni vya kuvamia maeneo wazi ya jiji
      Fyuuuuuh

      Delete
  3. Usijali MKUU, sisi wengine tulishakuelewa vizuri tu kwamba unazungumzia majambazi. Lakini hata mimi hao wanaharakati aka haki za binadamu sijaelewa kazi zao hasa hasa ni zipi!! wapo kisiasa zaidi

    ReplyDelete
  4. Mngekuwa mnaandika kwanza mnachokuja kuongea na wananchi ukisha edit vizuri ndiyo uje uongee maana si wote wanao weza kuitaprint!!

    ReplyDelete
  5. Juzi kuna watu walibeza askari ikaniuma sana. Jamanini uaskari ni wito. Ni ngumu sana kazi hii. Msiwadharau, msiwakejeli, msiwasute. waendeni, wasaidieni, wapeni moyo. Wameapa kufa kwa ajili yetu. Ni Mitume hawa.

    ReplyDelete

Top Post Ad