Weka Picha za Utupu Mtandaoni Uende Miaka 20 jela – TCRA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Unataka kwenda jela? Ni rahisi, weka picha za ngono mtandaoni, na utakuwa mkazi wa huko kwa kipindi cha miaka 20.

Kwa mara nyingine tena, mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA imewakumbusha watanzania kutozichezea sharubu za sheria ya makosa ya mtandaoni, lasivyo wataishia pabaya.

“Ni vyema wananchi wakatambua kwamba uchochezi kwenye mitandao kwa kusambaza ujumbe wenye viashiria vya uvunjifu wa amani au kuweka picha zisizofaa kwenye mitandao sheria ipo wazi na watu watajikuta wanaishia pabaya, hivyo ni vyema kuchukua tahadhari mapema,” alisema Mhandisi wa Mawasiliano wa Victoria Rulakara wakati akizungumza kwenye kipindi cha Hotmix cha EATV.

Wakati huo huo, mamlaka hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ikiwa ni pamoja na kuwaonya watu wanaonzisha blog zenye majina ya uongo kutukana watu wengine.

Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ilipitishwa mwaka jana na rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SAFI SANA!INAPENDEZA NCHI KUWA NA SHERIA ZAKE NA SIO KILA KITU KUIGA.
    JE SERIKALI HAPO IMEKOSEA NA KUMNYIMA MTU UHURU WAKE?KARIBUNI JAMVINI MNAOJUA NA KUTETEA HAKI ZA BINADAMU.

    ReplyDelete

Top Post Ad