Bob Junior AmchanaJose Chameleone Kuhusu Video yao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Producer na muimbaji tokea Sharobaro Records, Bob Junior amemchana mkali tokea pande za Uganda, Jose Chameleone baaa ya kufanya wimbo pamoja ambao video yake haijatoka, wimbo unaofahamika kwa jina la "Siachani Naye" mwanzoni mwa mwaka huu.

Bob Junior alidai kuwa alikuwa na nia ya kufanya video ya wimbo huo lakini kila alipokuwa anapanga ratiba za ku'shoot, Chameleone
alikuwa akikwepa.

Akipiga story na eNewz Bob Junior alisema "Tukipanga siku ya ku'shoot, ikifika siku hiyo nikimtafuta basi hajibu meseji zangu, sasa mimi nitafanyaje? Hata hivyo sitaki kusema mengi kwa ubaya, labda kuna vitu kweli vinamzuia".

Hata hivyo Bob Junior alisema baada ya kushindwa kufanikisha kufanya video hiyo, sasa anajipanga kwa kazi nyingine, huku akisema anatarajia kuachia wimbo alioshirikiana na Q Chief na Baraka da Prince, wimbo unaoitwa "Kidege" na kama si wimbo huo basi ataachia mwengine unaoitwa "Mpasuo"
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad