EFM Yamburuza Paul James Mahakamani Kwa Kuvunja Mkataba, Yadai Fidia ya Shilingi Milioni 200

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtangazaji wa Clouds FM, Paul James aka PJ ameshtakiwa mahakamani na kituo cha redio cha EFM kwa kuvunja mkataba kinyemela
Mtangazaji huyo aliondoka EFM mwanzoni mwa mwezi huu na kurejea kwenye kituo chake cha zamani, Clouds FM, alichoondoka pamoja na mwenzake Gerald Hando. EFM imefungua mashtaka katika mahakama ya kazi jijini Dar es Salaam kwa madai ya kukiuka mkataba wa kazi wa kituo hicho.

Kufuatia mashtaka hayo, EFM inadai fidia ya shilingi milioni 200 kutoka kwa mtangazaji huyo.
Inadai PJ alikatisha mkataba kiholela na kurudi tena Clouds FM bila kufuata makubaliano pamoja na sheria alizokubaliana nazo katika mkataba wake pale alipojiunga nacho.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa November 23, 2016 katika mahakama ya kazi jijini Dar es Salaam.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad