google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Kwanini Sauti ya Diamond Live ni Mbaya Lakini Nzuri Kwenye Nyimbo Tofauti? | UDAKU SPECIAL

Kwanini Sauti ya Diamond Live ni Mbaya Lakini Nzuri Kwenye Nyimbo Tofauti?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jamani mi ni shabiki mkubwa na mzuri wa mziki wa bongo fleva, ila ili jambo linanipa wakati mgumu kuamini, huyu mkali wa bongo fleva diamond ana nyimbo kali sana ila kumekuwa na tofauti kubwa sana katika uwasilishwaji wa nyimbo hizo katika live performance na nyimbo tunazozisikia kwenye radio.

Diamond katika nyimbo ana sauti nzuri yenye base kidogo. Ila huyu jamaa sielewi kwanini akiimba live sauti inakua ingine kabisa yaani mbaya, mbona kina ben paul, banana, kiba king, rayvanny harmonise bela etc wakiimba live sauti inakua ile ile. au kuna ka application kwenye playstore anachokitumia kufanya sauti iwe nzuri studio.

Pia nafikiri sasa diamond aachie kina iyobo kucheza awapo jukwaani yeye afanye kazi moja tu ya kuimba, asijifanye michael jackson, na hii sasa ndo imekuwa weakness ya diamond ambapo mpinzani wake kiba anamfunikia.

Namshauri atafute mwalimu wa sauti na mziki wa live, vinginevyo hatutamuelewa . sauti ya jukwaani cjui ndo yake maana huwa mbaya, na akishindwa kabisa basi bana hata pua bwana

Kwaheri
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hahahha ukweli mweupe ni kwamba bwana mdogo ni mfanya biashara sio msanii ukizungumzia wasanii ni barnaba boy banana zoro enika jide kiba mzee wa masauti xstian bela n the few wengine ni bana pua mwanzo mwisho...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Upuuzi kabisa diamond yuko juu.hao uliotaja wako wapi sasa hivi wengine wanaimbia temeke mikoroshini acha kufananisha diamond na mfano wa wanamziki

      Delete
  2. hahaha kazi kweli semeni sana Mondi piga kazi!!!

    ReplyDelete
  3. Uumetumwa? Rudi ukawaambie Mondi kaenda South kucheki mjengo wake

    ReplyDelete
  4. Muache wivu, diamond tangia aanze kuimba hafanyagi mistake akitoa nyimbo razime iwe top, huyo habahatishi ana kipaji cha ukweli, acheni unafiki na kizuri mkisifie

    ReplyDelete

Top Post Ad