MTV MAMA: Ushindi wa Kishindo wa Wizkid Utuamshe Kuhusu Tunavyozichukulia Tuzo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ushindi wa kishindo wa Wizkid kwenye tuzo za MTV MAMA mwaka huu, unanikumbusha wale wanafunzi wa kiume ambao huwa hawana time kabisa na wasichana wa darasani, lakini bado watamnasa kila demu mkali.

Wanafunzi wa aina hii ni wale ambao huwa na akili sana darasani au kwao mambo safi (wana mkwanja) – vitu viwili muhimu vinavyowadatisha madenti wa kike! Warembo hujipeleka wenyewe!

Tangu kutangazwa kwa majina ya wasanii watakaowania tuzo hizo mwaka huu, Wizkid hakuwahi kusema chochote. Alikuwa kimya tu utadhani hakuna kinachoendelea licha ya kuwepo kwenye vipengele vingi.

Hakuwa na muda wa kusema ‘thanks for the nomation.’ Hakuwa na hata muda wa kusema ‘jama eeh, mwenzenu nimetajwa kwenye MTV MAMA hebu nipigieni kura.’ He didn’t give a damn! Si ajabu lakini kwasababu ni kawaida yake bwa’mdogo huyu. Yeye tuzo huziona kitu cha kawaida, mpe sawa, mnyime, fresh tu!

Ehh! Jumamosi kaibuka na tuzo nne, kawa ‘man of the night.’ Unadhani ni kura ndizo zimempa ushindi wa tuzo zote hizo? Napata tabu kuamini. Msanii mmoja mkubwa sana ameniambia, namnukuu: Sometimes KURA zinapotosha. Watu wamepiga kazi nzuri ila kura zinapick wengine.”

Anachomanisha kuwa, msimamo wa Wizkid kutojishughulisha na kusema lolote kuhusu tuzo, kunaweza kukawa kulimfanya asipate kura nyingi kihivyo, lakini ukweli ni kwamba, hakuna msanii Afrika aliyefanya makubwa kumzidi Wizkid mwaka huu.

Alishirikishwa kwenye wimbo ‘One Dance’ wa Drake ambao umeweka rekodi kibao ikiwemo ya kusikilizwa mara bilioni 1 kwenye mtandao wa Spotify na kuwa wa kwanza kuwahi kuvutia namba hizo. Wizkid amefanya kazi na Chris Brown, Trey Songz, French Montana na wasanii wengine wakubwa. Ndio msanii anayefanyia kazi Afrika anayefahamika zaidi kwa sasa Marekani. Hata kama hakuonesha kuzitilia maanani tuzo hizo, ilikuwa ngumu kumkwepa.

Fundisho hapa ni kwamba, wingi wa kura unaweza usiwe na maana yoyote katika kumpata mshindi. Haiko sawa kwa namna yake ndio maana Eddy Kenzo amelalamika. Kwamba kama waandaji wanasisitiza watu wapige kura, lakini waliopigiwa kura nyingi hawapewi ushindi, ya nini kuwaambia watu wapige kura? Ni sawa na kampuni kutangaza ajira na kuwafanyia usaili baadhi ya waombaji huku ikiwa na watu wengine itakaowapa kazi.

Hatuna ulazima wa kujilaumu au kuumia sana au kuushusha muziki wetu. Wasanii waliotuwakilisha wamefanya kazi kubwa na ngumu kuipeperusha bendera ya Tanzania. Tusiwabeze, tuwape moyo na kuwaunga mkono bila kuchoka. Katika kipindi wanachohitaji zaidi support yetu, basi ni hiki.

Bongo5
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad