RC Mrisho Gambo apigiwa simu Rais Magufuli. Soma walichozungumza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema kuwa Rais Dkt John Pombe Magufuli amempigia simu  na kumwambia kuwa ana imani naye na kuwa hajafikiria kutengua uteuzi wake labda kumpandisha cheo.

Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  baada ya taarifa kuhusu Rais kutengua uteuzi wake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Mkuu wa mkoa alisema kuwa alipigiwa simu nyingi na watu wengi lakini kabla hajawajibu Rais Magufuli akampigia simu na kumueleza kuwa ana imani naye na kuwa ahakikishe anawatumikia wananchi wa Arusha kwani yeye sio bosi wao bali ni mtumishi wao.

Pia mkuu wa mkoa alieleza kuwa Rais amempa maagizo ya kuhakikisha anasimamia wananchi wa mkoa wa Arusha walipe kodi kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo na nchi kwa ujumla.

Aidha, ili kuthibitisha kuwa ni Rais Magufuli ndiye aliyempigia simu, Rais aliomba kuongea na yeyote aliyekuwa karibu ndipo mkuu wa mkoa akampa mmoja wa waliokuwa katika mkutano huo kuthibitisha kuwa ni Rais Magufuli.

Habari ya kutenguliwa kwa mkuu wa mkoa wa Arusha imekuja ikiwa ni siku moja baada ya kuibuka mvutano mkali kati ya mkuu huyo wa mkoa na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuhusu mradi wa ujenzi wa hospitali itakayotoa huduma kwa mama na mtoto mkoani humo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Arusha ni shidaaaaaaaaaaaa,sijui huyo Rais atawatengua wangapi.
    Piga kazi kaka.HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete
  2. hatumbuliwi bibi
    chakula cha bwana hamuachi
    dar na arusha tangu macho yao haloooooooooooooooooooo
    cccmmmmmmmmmmmmmmm
    hiyo
    wanasme ya wenzao lakini wanapeana ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa
    raha gani ukiwa shoga awamu ya tano jamaniiiiiiiiiiiiiii
    tuacheni mashoga awamu tano tunatesa kitu

    ReplyDelete
  3. tumikia sawa, ila siyo tumika!!

    ReplyDelete
  4. Jamani mimi sio mwanachama wa chama chchote, sishabikii chama ata siku moja.
    Ila ndugu zangu nina swali moja: Niliangalia kwa makini kabisa ile video alipo kuwa akilalamika yule mbunge. Siwezi kuongelea sana alichokuwa akilalamika,kila mtu anamajibu yake. Katika kulalamika kwake alisema" Kila ninao gombana nao rais uwapandisha vyeo" Mwisho wa kunukuu. Leo mkuu wa mkoa amesema "Rais haja fikiria kutengua uteuzi wake labda kumpandisha cheo!!" Mwisho wa kunukuu. Jamani naomba jibu. Je mbunge alichokisema kinaukweli?? Au nini kinacho endelea kwenye nchi yetu. Mungu ibairiki Tanzania na Afrika. Wenu JB. USA

    ReplyDelete

Top Post Ad