Sakata la Lema na Gumbo Arusha Lamuibua Dr Slaa Mafichoni..

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dr Slaa anaandika!

Mrisho Gumbo,
Naamini hii ID ni ya kwako na hasa kwakuwa kwenye post unaonekana ukizungumza, napata uhakika kuwa ni wewe.

1) Mkuu wa Mkoa, nakuheshimu kwa kuwa cheo chako ni kikubwa sana. Hata hivyo, ulichokifanya leo na " propaganda unazopiga zimenifanya nikudharau na kukupuuza. Ningeliweza kuishia katika kukudharau na kukupuuza, lakini

2) Aibu uliyoiletea Taifa letu leo, inanifanya " nipige kelele" kuwa " siasa za maji taka siyo wakati wake huu.
a) Mhe.Mrisho Gumbo, wewe kama Mkuu wa Mkoa unayo au mamlaka au vyombo vya dola kukusaidia kufanya utafiti wa maana kuliko aibu kubwa uliyoiletea Taifa letu mbele ya Wahisani/ Wafadhili wetu kupitia Maternity Africa. Hukufanya hivyo, umeamini propaganda kuliko busara na hekima. Kwa hilo siwezi kukusamehe wala kukuheshimu pamoja na cheo au vyeo vyote ulivyonavyo.

b) Mrisho Gumbo, ungelikuwa wa busara iwapo ungelimwomba kiongozi au mwakilishi wa ADF ( ulikuwa na uwezo wa kujua ADF ni nani na historiaya yake ni ipi- kwa kupenda propaganda hukufanya hivyo) au Mwakilishi wa Maternity Africa hasa Happy ( ambaye alisaini pia barua ya kukualika kuwa mgeni rasmi, au hata Mhe. Mbunge Lema ambaye kimsingi ndiye chimbuko la upatikanaji wa Ardhi hiyo kutoka kwa Marehemu Advocate Mawala ( Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi), na pia chimbuko la Upatikanaji mradi kutoka kwa wafadhili wetu. Kutokupenda kushauriwa na hao wenye kujua mradi imekufanya "kuonekana ****" na " mwongo" kwa kuwa historia haifutwi kwa " propaganda za jukwaani". Lakini kwa bahati mbaya athari ya propaganda imeenda mpaka kuichafua Taifa letu kwa wahisani. Ujenzi ndiyo kwanza unaanza. Umeombwa kufanya "Ground Breaking ceremony", unadhani wawakilishi wa wahisani na hasa kule kwenye chimbuko la fedha wanapata picha gani ya Taifa letu.

c) Mrisho Gumbo, busara na hekima ya kawaida ingelikuwezesha kuelewa barua ya mwaliko ambayo imesisitiza mara mbili hivi, kuwa wahusika ni taasisi isiyojihusisha na siasa. Wakasema mradi kwa muda sasa umekumbwa na matatizo yenye sura ya kisiasa. Ulipaswa kutafakari, kutafiti na kutafiti njia makini zaidi ya kuona wakina mama wajawazito, wenye fistula na watoto wachanga hawakosei au hata hawacheleweshewi kupata huduma hiyo kwa sababu za kipuuzi tu. Eti unasoma historia! Unsijua historia au unaota ndoto! Nimepiga kelele kwa kuwa ninaijua vizuri hiyo historia A to Z. Sikuambii ungeliniuliza, lakini wapo kwenye kikao hicho ambao wasingelihitaji kuisoma bali kuitoa kichwani historia hiyo, tangu kupatikana kwa Ardhi, mchakato wa kuchora ramani, kuisajili na kupata vibali vyote vya Kituo hicho cha Afya( japo kwa kweli ni hospitali ( inaitwa kituo cha Afya tu kwa. Sababu za kisheria).

3) Mrisho Gumbo, kwa hili Watanzania wa Arusha na wote wenye kujua ukweli hatutakusamehe kwa aibu uliyotupatia, na kujenga misingi ya kutufungia miradi mingine kwa wahisani wetu. Kama una chembe dogo la busara:

a) Utakaa chini na kutafakari umekosea wapi. Ikiwa lazima

b) uwe na unyenyekevu uwaite wahusika wote ofisini kwako waombe wakupe " historia kamili" na wakupe mchakato mzima mpaka kufikia siku hii muhimu ya " Ground Breaking ceremony( uzinduzi wa Kazi ya ujenzi).

c) Ukipata Taarifa kamili, uwe na unyenyekevu, acha kiburi. Kiburi hakikusaidii wala haitasaidia jamii unayopaswa kuwatumikia ( unless una malengo tofauti). Kwa unyenyekevu mkubwa Waombe msamaha Wahisani wetu kwa kuwaingiza katika " siasa ya Arusha" ambayo hawahusiki nayo; awaombe msamaha wakina mama, watoto na jamii ya Wananchi wa Arusha wapenda maendeleo kwa kuwachafua na kuwaletea vurugu kiasi cha kuifanya Arusha ionekane kila leo ni mahali pa vurugu, kumbu vurugu husababishwa na viongozi wasiotumia busara na hekima. Uongozi ni busara na hekima siyo mabavu wala nguvu ya mamlaka.

Nimeyasema haya kuuchungu mkubwa. Mimi siko kwenye siasa, na wala sina interest na siasa. Siangalii uso w a mtu. Kama ambavyo niliaga kuwa " Nastaafu Party Politics, lakini nitapiga kelele pale maslahi ya Taifa langu yanavyokanyagwa" nitakuwa mwendawazimu kunyamaza wakati mradi wa Tshs Takriban 9 Billioni unahatarishwa na upuuzi na uzembe wa kiongozi mnoja mwenye kuendekeza propaganda zisizo na msingi.

Nawaomba sana Radhi wahisani wetu. Mtuvumilie siyo kwa ajili yetu bali kwa ajili ya kina mama na watoto walengwa wa huduma itakayotolewa na " Kituo cha Mama na Mtoto" ( propaganda ya Hospitali ya mke wa Lema zipuuzeni). Happy, umevumilia mengi katika miradi mingi uliyofadhili na kuisimamia. Usirudi nyuma. Timiza ndoto yako iliyoanza katika umri mdogo sana. Matunda yanaonekana pamoja na vikwazo vya mara kwa mara vya wapinga maendeleo. Viongozi, " Tenganisheni siasa na Maendeleo" Watumikieni Watanzania bila kuangalia nyuso zao, mrengo wao. Siasa ni sayansi na siasa sayansi ni utumishi.

By Dr Slaa
Source:Chingaone/Jamii Forums
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi huu muswaada wa uandishi utaanza lini watuondolee waandishi uchwara kama huyo hapo juu tumechoke stori za kutunga za kinafiki mara fulani kasema hivi mara fulani sijui kafufukia wapi kamchana fulani kuweni waungwana sio kutumikiwa waandishi kisiasa tunataka maendeleo ya nchi kwa ujumla sio blah blah blah

    ReplyDelete
    Replies
    1. yaani huyo mwandishi ni bomu sana na unaweza kuta hayo maneno hata DR Silaa hayajui, waandishi kuweni makini wakati mnapoandika isiwe mnatuletea maneno ya shobo ya kuvunja amani

      Delete
  2. Kila pahala na kila kukicha fujo, sijui tunaelekea wapi

    ReplyDelete
  3. Respect Mh. Slaa...........Well said. Thank you Sir

    ReplyDelete
  4. Respect Mh. Slaa...........Well said. Thank you Sir

    ReplyDelete
  5. Yaani nilikerekaaaaaaaaaaa,mnafanya ujinga mbele ya wageni!

    ReplyDelete
  6. NAANZA KUAMINI MKUUUUUUUU ANAPENDA MASHOGA AU ANYE ANAKULA AU ALIWA
    GUMBO NA MAKONDA WAMEFANANANANNANANANA
    MAHARAGE YA BWANA YAKO JIKONI

    ReplyDelete

Top Post Ad