Unasoma Hadi PHD Hujawahi Kufanya Kazi, Una Matatizo – Mwijage

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewachana vijana wanaotumia miaka mingi kuwa chuoni wakisoma hadi kufika kiwango cha PHD bila kupitia ujuzi wa kazi yoyote.

Ameyasema hayo Jumatatu hii katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV akidai kuwa vijana wengi wanapenda elimu aliyooita ya ‘mseleleko’ akimaanisha elimu ya moja moja kwa moja bila ya kujaribu kufanya kazi yoyote au bila kupitia ujuzi mbalimbali wa kazi.

“Tatizo moja tulilonalo tunapenda elimu mseleleko,” alisema. “Sipendi kuizungumzia elimu lakini nataka niseme tunapenda elimu mseleleko, yaani unaanza leo miaka 6 unaanza darasa la kwanza, unakwenda moja kwa moja mpaka unamaliza PHD,hujawahi kufanya kazi. Mimi sikusoma elimu mseleleko na ndiyo maana mimi watu wengine kama ntalisema hili wengine litawaudhi shauri yao,” alisisitiza.

“Watu wengine wanapenda kujua mimi nimesoma shule gani, kimsingi mimi elimu ya darasani ni ndogo, niliyonayo ni elimu ya mtaani nimefanya kazi nyingi, mi nimevua samaki, nimefanya kazi gereji, ukiniuliza naweza nikakuuliza ukasema na hili Mwijage unalijua. Mimi nilikuwa hata Dj nilikuwa MC, nimefanya kazi nyingi sana kwenye field,nimepiga debe mimi, kwahiyo mimi vitabu vya darasani sina,” alieleza.

“Lakini hii elimu mseleleko hii hujawahi kufanya kazi yoyote unakuwa injinia hujawahi kusimamia hata jengo moja ina matatizo. Kwahiyo vijana mkikwama tafuta namna ya unavyoweza kuanza. Mi nawafahamu watu ambao waliokwenda kusoma kutokana na vipato walivyojitafutia,mi nawafahamu watu waliofanya vibarua kujilipia karo.”

“Sasa mtu anasoma kuanzia darasa kwanza moja kwa moja mpaka PHD bila kufanya kazi yoyote, hata vijana wa Ulaya mbona wanafanya kazi wanajilipia karo, so we have problem kwasababu ni maskini tunapenda kwasababu ya kupenda haya ya mseleleko. Mtu akianza wenzake wakimtangulia aliokuwa anasoma nao anajisikia vibaya. Mi mbona kuna watu tulimaliza nao form six wakaenda chuo kikuu na mimi sikuenda nilikuwa nafanya mambo mengine!
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Analosema waziri ni sawa sawa,huku nchi za ulaya ,marekani MTU anasoma na kazi amefanya kipindi cha zikizo,wengine wanapajua hata bure ili apate uzoefu,ila tz hakuna utaratibu huo,lazima tubadilike

    ReplyDelete
  2. Analosema waziri ni sawa sawa,huku nchi za ulaya ,marekani MTU anasoma na kazi amefanya kipindi cha zikizo,wengine wanapajua hata bure ili apate uzoefu,ila tz hakuna utaratibu huo,lazima tubadilike

    ReplyDelete
  3. Hongera msema kweli mpenzi wa mungu. uchaulinwako ni mzuri sana kwa vijana wa leo. elimu na ujuzi safi sana. wengi wana elimu alakini field awazijui

    ReplyDelete
  4. Serikali ya mwendo Kasi katika ubora wake jitu zima linaongea bila kushirimisha kichwa

    ReplyDelete
  5. MTAMKUMBUKA KIKWETE!!!!!! UKWELI NDIO HUO,,,,,,,

    ReplyDelete
  6. Hapo waziri umechemsha. Elimu kwanza mambo mengine ya ubabaishaji kama kuvua samaki,mc, kupiga debe hayo baadae. Elimu kwanza.

    ReplyDelete
  7. Point Kama hamjamueluwa mwaziri ni kwamba.
    Kusoma bila kufanyakazi hata part time sio nzuri.
    Pili, kusoma bila kufanya kazi in between unakuwa hung experience yeyote ya kazi kwenye fani unayosomea. Bali phD ya shule ya kufundishwa.

    Ulaya na America masters na PhD ni professional degrees. Maana take lazima ukimaliza degree ya kwanza ukafanye kazi, kisha ndio urudishule na ujuzi fulani wa kazi. Abao utaweza kuleta Kwa wenzio na kubadilishana mawazo, na kutatua changamoto ulizoziona wakati ukifanyakazi

    ReplyDelete
  8. we kaa na elimu yako alaf naulu unaombankwa alieishia form 4 mpiga debe au salooner

    ReplyDelete
  9. Mheshimiwa ameongea ukwel.....

    ReplyDelete

Top Post Ad