WATUMISHI Waliosoma Vyuo Vikuu Bila Sifa Kufukuzwa Kazi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baada ya matamko kadhaa kadhaa ya serikali kuhusu Sekta ya Elimu nchini hatimaye leo limeibuka jingine la kutimua watumishi wote wa umma waliojiunga na vyuo vikuu na kutunukiwa "degree" bila kuwa na sifa.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako wakati akifungua maonesho ya vyuo vya elimu ya juu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo vikuu nchini (TCU) yanayofanyika viwanja vya Karimjee, jijini Dar.

Maonesho hayo yanashirikisha vyuo 61 ambapo 12 kati ya hivyo ni kutoka nje ya nchi.
Katika taarifa yake Ndalichako amesema Wizara yake inawasiliana na idara ya Utumishi ili kuwabaini watumishi wote waliojiunga vyuo vikuu bila sifa na wafukuzwe kazi. "Kama wewe ni mfanyakazi uliyesoma moja ya vyuo vikuu ukafaulu lakini hukuwa na sifa ya kujiunga na chuo kikuu, tutakunyofoa hukohuko kwenye ajira yako" Alisema Ndalichako.

Kufuatia agizo hilo la Ndalichako, watumishi wote waliosoma vyuo vikuu kwa kupitia foundation courses kama Pre Entry/Remidial/Certificates, etc,wataondolewa kazini. Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa ya kusoma degree. Amesema kuwa kama mtu hakupata points za kumuwezesha kujiunga chuo kikuu hata asome foundation course bado hatapata sifa, namna pekee ya kupata sifa ni kurudia mtihani wa kidato cha sita.

Agizo hilo pia litawagusa watumishi waliojiunga na elimu ya juu kwa ufaulu linganishi (equivalent pass) ambapo kwa wale waliotoka diploma na wakasoma degree bila kufikisha GPA iliyowekwa na NACTE watatimuliwa. Pia waliotoka kidato cha sita na kupata nafasi vyuo vikuu moja kwa moja lakini hawakufikisha "cut off points" zilizowekwa na TCU wataondolewa katika ajira zao.

Prof.Ndalichako amesema zoezi hilo litaanza baada ya kumaliza zoezi la uhakiki wa sifa kwa wanafunzi wanaopata mikopo. "Tukimaliza hawa wanaopata mikopo, tutahamia wasiopata mikopo kuona kama wana sifa za kusoma vyuo vikuu, baadae kwa wafanyakazi. Hata kama hukupata mkopo, lakini ulisoma chuo kikuu bila sifa hauko salama" Alisisitiza Ndalichako.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hacha ufala wewe Joyce kwani huo utaratibu si muliuweka wenyewe na wewe ulikuwepo kabla hujawa waziri wa elimu, cha kufanya huo mpangilio muubadilishe sasa sio kuwafukuza watu kazini unataka wakale wapi, au kwa sababu wewe unayo ajira hujari za wenzio

    ReplyDelete
  2. Huyu bibi ndio hao mawaziri wakurupukaji wanaotaka kumtia dosari rais wetu. Kama mtu ametokea foundation na akaweza kusoma degree na kupass sasa tatizo ni nini? Si aliisomea his degree sawasawa na hao wengine waliokuwa maliza vidato vya juu? Umataka kuwa dhuluma watu kazi zao bure kwa kuwaonea kama umeshindwa kuzalisha ajira mpya useme ukweli. Sio kila mtoto anafunguka akili mapema wengine huchelewa na ndio ukaona hao waliochelewa kufunguka huachwa nyuma kimasomo. Na wakifunguka inabidi waanzie foundation ili wafike juu. Sasa wewe Hata hilo linakuudhi kwa wao kujiendeleza. Nchi nyingi zilizoendelea watoto wanasema mpaka form 4 ni elimu ya lazima sisi Tanzania Ati mtu kafeli darasa la 7 haruhusiwi tena labda mzazi ampeleke private. Hivyo kweli hii nchi mnataka iendelee? Wakati mnapinga kila jambo la raia wenu kujiendeleza. Sasa ndio tuna wafundisha watoto wetu nini soma halafu vyeti vyako havina maana. Nchi zote ulimwenguni wanazikubali degree unazo achieve kwa kupitia foundation.

    ReplyDelete
  3. Na afukuzwe yeye kazi amesoma na mavyeti vyake lakini hana commonsense. Hao watumishi anotaka kuwafukuza kwani hizo kazi zao hawazifanyi vizuri? Na wakati kuna watu hawana vyeti wanafanya kazi vizuri kwa ajili ya experience ya ile kazi wa ifanyayo kuliko Hata walionavyo. Rais Abeid karume hakusoma na ndie rais aliefanya mengi mazuri Zanzibar kuliko Hata hao wasomi.huo usomi wako ndio tatizo lako umetumia muda mwingi ku crammed kwenye mabuku unashindwa kuuona ulimwengu halisi ulivyo.

    ReplyDelete
  4. Kila mtu anataka asikike hat a utumbo utamsimamushe mtu Nazi wakati sio mwajiri wake awe n.a. ziro au one Hilo halimuhusu wenye makosa ni hawo waliokuwepo mwanzo watch wamespendi pesa na time zao vipi Leo ukurupuke labda waseme kuanzia January mwakani lkn sio kumsimamisha mtu kazi

    ReplyDelete
  5. binafsi siusapoti huo mpango wa kufukuza kazi kwani hao waliofanya hivyo kwa wakati ule taratibu na sheria zinawaruhusu na wala hawakufanya feki. kama kuna utaratibu mwengine uanze lakini sio hauwahusu waliopita.

    ReplyDelete
  6. KWELI HAPO UTAKUWA HUJAWATENDEA HAKI HAO AMBAO WALIANZA NA FOUNDATION NA BAADAE KUPATA DEGREE ZAO KWA KUFAULU VIZURI SANA KWANIHATA SERIKALI ILIWATAMBUA NDO MAANA WAKAPEWA AJIRA.SASA UKUWAFUKUZISHA KAZI UNADHANI WATAISHIJE AU UTAWATUNZA WEWE? NADHANI HAPO KUNA WATOTO NA NDUGU ZAKO PIA WAMEPITIA CHANNEL HIZO HIZO.

    ReplyDelete
  7. Ndugu zangu watanzania mnapotoa hoja tumieni Lugha nzuri, kuna mmoja anazungumza kama yuko kilabuni anakula ulanzi. tafadhali.
    haya ni mabadiliko ya mwanzo tu, bado mengine yaliyo mazuri zaidi na kama hujui jambo ni bora kuuliza au kukaa kimya kuliko kulipuka kama bomu, utatudhuru sisi.
    mmenielewa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na wala mazuri watu hawayapingi.lakini hili la kufukuza watu kazi kwa sababu hii ni uonevu na hatutoacha kusema. Magufuli anajitahidi lakini baazi ya viongozi wake ni wakurupukaji. Na hii litaleta matatizo. Nnakumbuka aNyerere na vijiji vya u jamaa aidia ilikuwa nzuri kuwasema watu pamoja ili iwe rahisi kupata huduma zote. Ikawaje? Viongozi wakakurupuka na matokeo tukayaona. Sisi sote tunaotaka Tanzania yenyewe maendeleo na tunaotaka nchi yetu mema.

      Delete
    2. It's sad to see the minister with degree on her back ground have poor vision to this level it make me wonder what sort of education she went through? Ninge mueke wa kama angeliota introduce performance a praisals for the graduates in relation to their work probably she doesn't understand what does Apprentice mean to society as young economical as Tanzania she needs to go back for her desolation in keadership

      Delete
  8. Tulipo kuwa tumefikia palikuwa pabaya mwache waziri aiweke sawa Wizara irudi kwenye mstari


    ReplyDelete
  9. teh mtaisoma namba

    ReplyDelete

Top Post Ad