CHADEMA wataka Rais Mkapa anyang’anywe shamba kama Sumaye

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Meya wa Manispaa ya Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), Boniface Jacob amemtaka Rais Dk Magufuli kulichukuwa shamba linalomilikiwa na Rais Mstafuu Mzee Benjamin Mkapa kama alivyofanya kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.

Meya huyo alisema kuwa kiongozi huyo wa zamani na familia yake wanamiliki shamba kubwa katika wilaya ya Ubungo ambalo halijaendelezwa kwa muda mrefu sasa.

Meya huyo ambaye amekuwa Diwani wa Ubungo kwa muda mrefu ametaa shamba hilo lililopo Mbezi, Dar es Salaam lirejeshwe kwenye halmashauri ili liweze kufanyiwa shughuli nyingine.

Hoja hiyo ya Meya wa Kinondoni imekuja siku chache tangu aliyekuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya tatu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Frederick Sumaye aliponyang’anywa shamba lake eneo la Mabwepande ambalo hajaliendeleza kwa muda.

Meya alitoa maelezo hayo alipokuwa akizungumza na gazeti la mwananchi ambapo alisema kuwa watamuandikia Rais Magufuli barua wakimuomba abatilishe umiliki wa shamba hilo aipe Manispaa ya Ubungo ambayo ndiyo kwanza imeanzishwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama ni kweli huyo Mkapa analimiliki Shamba ambalo hana uwezo wa kuliendeleza na wala hajaliendeleza kwa muda mrefu ni kweli kabisa kuna kila sababu ya kimsingi ya kumnyang'anya. Itakuwa uonezu wa hali juu kuona kuwa kuna watu pamoja na matatizo yaliyojitokeza kwao lakini bado mashamba yao aidha yamefutiwa hati milki na pia hayo mashamba yametaifishwa pamoja na kwamba kuna ukweli kuwa walikuwa wanayaendeleza. Kwa hili la Mkapa la Kuwa na Shamba ambalo ameshindwa kuliendeleza ni jambo ambalo sisi Wananchi wa kawaida itatubidi tulipigie kelele ili na yeye anyang'anywe kama walivyong'anywa watu wengine.

    ReplyDelete

Top Post Ad