MAJINA ya Wadaiwa Sugu Shirika la Nyumba yatua Kwa JPM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), limewasilisha ripoti ya wadaiwa sugu wa shirika hilo, zikiwamo wizara, taasisi za Serikali na watu binafsi kwa Rais Dk. John Magufuli, huku wizara mbili zikiwa na deni kubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mikoa na Utawala wa NHC, Raymond Mndolwa, alisema uamuzi huo umekuja baada ya Rais Magufuli kuwataka kukusanya madeni hayo na kuwasilisha taarifa hiyo ofisini kwake ili aweze kuipitia.

Mndolwa alisema NHC ilitoa notisi ya siku 90 ambayo ilianza  Septemba, mwaka huu, huku wadaiwa hao wakitakiwa kulipa madeni  ndani ya muda uliopangwa.

Alisema kuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bado zinadaiwa kiasi kikubwa cha fedha, licha ya kuwapo kwa mazungumzo ya kulipa madeni yao.

“Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto inadaiwa Sh bilioni 1.4, huku wakilipa Sh milioni 300, wakati Wizara ya Habari, inadaiwa Sh bilioni 1.14, lakini imelipa Sh milioni 700,” alisema Mndolwa.

Mndolwa alisema shirika hilo hadi sasa limekusanya Sh bilioni 5.9 kati ya Sh bilioni 9.3 ambalo ni deni la Serikali kupitia wizara na taasisi mbalimbali, huku Sh bilioni 2.5 zikikusanywa kutoka kwa wadaiwa binafsi ambao awali walikuwa wanadaiwa Sh bilioni 4.

Alisema lengo la shirika hilo ni kuhakikisha madeni yanalipwa ili fedha hizo ziweze kutumika kwenye shughuli nyingine za maendeleo, ikiwamo ujenzi wa nyumba za kisasa 300 mkoani Dodoma.

Alizitaja wizara zinazodaiwa ni Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Fedha na Uchumi, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na iliyokuwa Wizara ya Ujenzi.

Wadaiwa wengine ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapa Kazi tu. Na hii ni meseji tosha kwa mchanganya siasa na deni la mjengo. Kuwa hapa ni Kazi Tu. Una deni unalipa au ..... unatoka au tunakutoa.. Tunahitaji msaada wenu katika kujiwajibisha. Tanzania itajengwa na sisis wa Tanzania tukiwa Waaminifu na Wajibikaji na Kujiwajibisha inapodidi.. Magu is a man of action... He deliveres. Hapa Kazi na Dodoma tunakujenga .

    ReplyDelete
  2. Hapa Kazi tu. Na hii ni meseji tosha kwa mchanganya siasa na deni la mjengo. Kuwa hapa ni Kazi Tu. Una deni unalipa au ..... unatoka au tunakutoa.. Tunahitaji msaada wenu katika kujiwajibisha. Tanzania itajengwa na sisis wa Tanzania tukiwa Waaminifu na Wajibikaji na Kujiwajibisha inapodidi.. Magu is a Man of Action... He Deliveres. What he has promised the People. Hato Tuangusha!!!!!!Hapa Kazi TU

    ReplyDelete

Top Post Ad