SAKATA la Kuuawa kwa Faru John Lachukua Sura Mpya.......Watumishi Watano Watiwa Mbaroni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Maofisa watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wanaotuhumiwa kushiriki kumwondoa faru John kutoka katika Creta hiyo walikamatwa juzi kwa mahojiano ili kujua ukweli kuhusu mazingira ya kupotea kwake.

Hatua ya maofisa hao kukamatwa imekuja siku tatu baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuituhumu menejimenti, wafanyakazi wa NCAA na Baraza la Wafugaji (NPC) kuwa imejaa vitendo vya rushwa na wizi na asingeweza kuvumilia sakata la faru John ambaye alisema kuwa aliuzwa kwa Sh200 milioni kwenye Hoteli ya Grumet iliyo Hifadhi ya Serengeti na kuwa walipokea fedha za awali Sh100 milioni.

Waziri Mkuu alisema anataka kumwona faru huyo, nyaraka za kumhamisha na kama amekufa basi apelekewe hata pembe ofisini kwa kuwa anajua pa kuzipeleka.

Alisisitiza kuwa ikibainika kuna ambao wamekiuka taratibu watawajibika.

Habari za uhakika kutoka Ngorongoro, ambazo zimethibitishwa na Jeshi la Polisi zinasema kuwa maofisa hao watano wanashikiliwa katika kituo chao cha Ngorongoro kutokana na ushiriki wao kwa njia moja au nyingine.

Wanaoshikiliwa ni pamoja na Israel Naman ambaye alikuwa Kaimu mkuu wa idara ya uhifadhi wakati faru huyo akiondolewa.

Wengine ni Cuthbert Lemanya, ambaye alikuwa Mkuu wa Kanda ya Creta, Dk Athanas Nyaki ambaye anadaiwa kumdunga sindano ya usingizi ili aweze kubebwa.

Maofisa wengine waliokamatwa ni aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka ya Ngorongoro, Kuya Sayaleli na aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Ikolojia, Patrice Mattey.

Ofisa mmoja wa NCAA, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake jana alisema maofisa hao walikamatwa juzi jioni na jana walikuwa wanaendelea kuhojiwa.

“Tuiache serikali ifanye kazi kwani ni muhimu sana kujulikana ukweli wa tukio hili,” alisema ofisa huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo hakupatikana jana kuelezea tukio la kukamatwa maofisa hao, baada ya simu yake kupokelewa na msaidizi wake ambaye alieleza yupo kwenye kikao.

Lakini, ofisa wa mmoja wa polisi, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina kwa kuwa si msemaji alikiri kukamatwa maofisa hao kwa mahojiano.

Chanzo cha sakata
Akiwa katika ziara ya kikazi Ngorongoro, Waziri Majaliwa aliibua sakata la kuhamishwa kinyemela faru huyo na kudaiwa kupelekwa Grumet.

Waziri mkuu alitaka ukweli kuhusu upotevu wa John aliyeondolewa Creta na kupelekwa Grumet na kudaiwa kufa huku taarifa za kifo hicho zikifanywa siri.

Waziri Mkuu alitaka kupewa nyaraka zote zilizotumika kujadili kumuondoa faru na kuamua kumpeleka Grumet.

Waziri Mkuu alitoa hadi Desemba 8 (jana) awe amepata taarifa zote, ikiwamo ya daktari inayothibitisha kifo hicho na kwamba pembe za faru huyo zifikishwe ofisini kwake. Pia, Majaliwa alisema ikibainika wapo waliokiuka taratibu watawajibika.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwanini wasimuweke zoo
    Wote kuanzia mkurugenzi na watendaji Kama bado wizarani
    Vitu vinawekwa kwenye zoo vizaliane itafika siku tutauziwa tembo, simba nk toka ulaya dunia nature imekwisha tubadilike hata Safari za wanyama kwenda Kenya tuzibadishe tuwajengee madaraja ili wasiliwe na mamba au kufa maji hii tufanye uamuzi wetu kwani watalamu wa kizungu wengi wao wana makampuni ya utalii ili waje kuona wanyama wetu wakiuwana
    Utapeli Upo dunia mzima
    Waziri litazame hili

    ReplyDelete
  2. Kwanini wasimuweke zoo
    Wote kuanzia mkurugenzi na watendaji Kama bado wizarani
    Vitu vinawekwa kwenye zoo vizaliane itafika siku tutauziwa tembo, simba nk toka ulaya dunia nature imekwisha tubadilike hata Safari za wanyama kwenda Kenya tuzibadishe tuwajengee madaraja ili wasiliwe na mamba au kufa maji hii tufanye uamuzi wetu kwani watalamu wa kizungu wengi wao wana makampuni ya utalii ili waje kuona wanyama wetu wakiuwana
    Utapeli Upo dunia mzima
    Waziri litazame hili

    ReplyDelete
  3. Kwanini wasimuweke zoo
    Wote kuanzia mkurugenzi na watendaji Kama bado wizarani
    Vitu nyeti vinawekwa kwenye zoo vizaliane itafika siku tutauziwa tembo, simba nk toka ulaya dunia nature imekwisha tubadilike hata Safari za wanyama kwenda Kenya tuzibadishe tuwajengee madaraja ili wasiliwe na mamba au kufa maji hii tufanye uamuzi wetu kwani watalamu wa kizungu wengi wao wana makampuni ya utalii ili waje kuona wanyama wetu wakiuwana
    Utapeli Upo dunia mzima
    Waziri litazame hili

    ReplyDelete
  4. Sasa kwa nini msiwafungie kazi hawa Grumeti.serikali yenu ya Ccm kwa miaka mingi sana mmewakubali wazungu kuchukua hizi ngazi juu za raslimali huko kwenye mbinga za Taifa. Wao kazi zao no kutengeneza pesa n.a. kuzihamisha. Sababu ni wazungu mmewaachia huru wafanye watakavyo. Chini ya z Raisi Kikwete serikali imewapotosha wananchi kupitia uwekezazi. Badala ya kusema uwekezazi ni ujanja umetumika kutoka mali za nchi hii.mnawakaba ngapi mnawaachia vigogo waliohusika.hawezi kuyakomesha haya rsisi wangu kama unawskumbatia maraisi waliopita ambao nfio chanzo cha matatizo n.a. mazito wake walioiba mali za umma. Mmewaachia huru ma waziri wa ESCROW ndio hao wakutoa ardhi, kuuza nvhi n.a. mali za chi.pia unawachia Hutu watu wakuu waamuzi, n.a. watoa rushwa. Unawachia huru wachina ambao ni janga kuu n.a. kusini cha matatizo m engi nchini.
    Utawatumbuaje watu wa chini n.a. utakomeshaje rushwa, ujambazi kama wahusika wakuu unawatetea hadharani.hutaweza. n.a. UN inayotoa geresha ya vijizawadi kuwafumba watanzania macho sababu uongozi wa juu natumika kupitisha hii miradi Tata, mbo n.a. mnachezewa.Mpaka Tanzania izalishe viongozi wa kweli, vijana wa kweli si wspumbavu, mpaka iwaelimishe watoto wetu wote bure toka vijijini n.a. kusahihisha namnavya kutumwa, kilinda, mali badala ya gereshageresha iliyopo. Mpaka watanzania wenyewe waje kuthamini nvhi n.a. mali zao na kuzitetea, mpska watanzania wachukue raslimali zao wenyewe badala ya kupokonywa.mpaka watoto wetu w sjue kuchapa kazi bila kusukumwa , kuthamini kazi, kujali kazi bila kusimamiwa n.a. kufaidika wenyewe. Mpaka viongozi wawathamini watanzania kama wawekezaji wakuu wa nchi Yao n.a. si wageni.mnapowsita wawekezaji n.a. kutokuwaelimisha watanzania kwanza mnaibisha nchi. Mnapowaelimisha watanzania Ile wawsfanyie kazi makampuni ya watu wa nje badala ya kuwatayarisha kimasomo, kujiamini Ile wsjiajili n.a. muwasaidie kifedha, kissikologia, na kuwatengenezes mazingira safi n.a. kiurahisi nyumbani kwao bado mnawarufisha nyuma n.a. mnauza mali zao cheap ma hamtaheshimika hata. Mnazidi piga magoti mabepari n.a. kushirikiana n.a. mabepari karudisha maendeleo ya watanzania nyuma. Mnawafunga mkono waliosomea mambo ya uchumi ksma mtu wa CUf kwenye kuvuruga watu kupitia s iasa hawa nod wa somi wababaishaji wanajua watakula kupitia siasa, badala ya kusaidia viongozi na kuitumia elimu yao kunufsisha nchi. Umekuwa mchezo wa kisiasa kukandamiza na kdanganya Watanzania. Nchi inamhitaji raisi ajaye mwenye maono haya ya juu, msikivu, atakayechagua wstu busara ili wamsaidie kulikomboa Taifa na mwenye agenda ksmili na utekelezaji safi wa afenda hizo.sgenda na shrria safi. Tunahitaji bado katiba ili viongozi watawale kufuata katiba ya nchi na si watakavyo.

    ReplyDelete

Top Post Ad