TAARIFA ya Kifo Cha faru John yakabidhiwa Kwa Waziri Mkuu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea taarifa inayoelezea utaratibu uliotumika kumhamisha faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti.

Akizungumza katika kikao kilichofanyika nyumbani kwake Oysterbay leo mchana na kuhudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na baadhi ya watendaji wa wizara yake, Waziri Mkuu amesema taarifa hiyo itafanyiwa kazi na wataalamu wa ofisi yake.

“Nilipokea taarifa yenu jana saa 7 usiku lakini nikaahidi kuwa leo tukimaliza sherehe za maadhimisho ya Uhuru tukutane na kujadiliana kuhusu taarifa yenu,” amesema.

Akisoma taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Prof. Maghembe alisema hadi kufikia Desemba 2015 wakati faru John anahamishwa alikuwa na watoto 26 (sawa na asilimia 70.2) ya faru wote waliokuwepo ndani ya kreta.

“Kati ya faru 37 waliokuwepo ndani ya kreta, watoto wake walikuwa 26 sawa na asilimia 70.2. Uamuzi wa kumuondoa John ulikuwa ni muhimu ili kuwezesha kuongezeka kwa faru weusi na kupunguza tatizo la ‘inbreeding’ ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro,” alisema Waziri Maghembe.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili Robert Mande (Kushoto) na Mkuu wa Pori la Akiba la Ikorongo/Grumeti, Bw. Nollasco Ngowe.

Baada ya kuhamishiwa Sasakwa, Waziri Maghembe alisema Julai 10, 2016 afya ya faru John ilianza kudorora na alikufa tarehe 18 Agosti, mwaka huu. Taarifa hiyo iliandaliwa na Kamati ya Taifa ya Kuwalinda Tembo na Faru. Kamati hiyo inaundwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Mkurugenzi Mkuu wa NCAA na Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro.

Akikabidhi pembe za faru huyo mbele ya Waziri Mkuu, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Bw. Robert Mande alimweleza kwamba pembe kubwa ya faru John ilikuwa na uzito wa kilo 3.6 na pembe ndogo ilikuwa na uzito wa kilo 2.3.

Desemba 6, mwaka huu, akiwa ziarani mkoani Arusha, Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha faru maarufu kwa jina la ‘John’ kutoka kwenye hifadhi hiyo ifikapo Alhamisi, Desemba 8.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania mnachezewa n.a. wazungu bila kufikiri.viongozi wote po kama watoto w asio n.a. akili.hii ni mbinu za ujanja zinazotumika n.a. wamiliki wa nurumenti kujiogezea umarufu n.a. kujiogezea kipato kifedha. Ni lini viongozi wa Africa mtatumia elimu Zen kwa manufaa ya nchi na wananchi badala ya kutumiwa n.a. wazungu. No kama hawajaelimika bado. Mnaendeshwa n.a. wazungu kama wako nchini kwao. Me Taifa ya elimu z enu ni nini.mnawatii wstu hawa bila kufikiri. No aibu kwa Taifa. Waadhibiwe n.a. Ngurumeti iafhibiwe kwa kupotosha watu. Hui ni aina mmojawapo ya bingo n.a. upotoshaji n.a. udanganyifu mkubwa.

    ReplyDelete
  2. Hao ni waongo wakubwa. Kama ni kweli Faru John alikufa tunataka watuonyeshe pia ni wapi walipomzika ili afukuliwe na ichukuliwe DNA. Hizo pembe ni za Kifaru mwingine na sasa wanazuga eti ni za yule Kifaru John.Wakati ukweli wa mambo ni kwamba yule Kifaru John walimuuza kwa Waarabu kwa $90,000.

    ReplyDelete
  3. Hii Nchi yetu sijui itafikia wapi kwa huuu aina ya utapeli na wizi uliokithiri.

    ReplyDelete
  4. Changa la macho ilo kwanin report isitolewe mapema tangu mwezi wa nane mpaka leo ni miez minne ndo report itolewe baada ya mheshimiwa waziri kutoa amri kwamba anahtaji vielelezo

    ReplyDelete

Top Post Ad