Vijana 29 Huambukizwa UKIMWI Kila Saa Moja

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linasema vijana 29 huambukizwa virusi vya ukimwi, VVU kila saa moja.

Katika ripoti yake mpya iliyotolewa leo, UNICEF inasema maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa vijana yanakadiriwa kuongezeka kutoka 250,000 mwaka 2015 hadi kufikia 400,000 ifikapo mwaka 2030.

Ripoti hiyo inapendekeza mikakati ya kuongeza kasi katika kuzuia VVU miongoni mwa vijana na kutibu wale ambao tayari wameambukizwa kama vile kuwekeza katika uvumbuzi ikiwemo wa kitaifa, kuimarisha ukusanyaji wa takwimu, kutokomeza ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia na elimu kwa vijana.

Wakati huo huo, kumefanyika kongamano la kimataifa jijini Durban, Afrika Kusini kuhusu Ukimwi ambalo limewaleta pamoja UNICEF, wanaharakati na vijana kutoka kutoka sehemu mbalimbali Afrika kupata maoni yao.

UNICEF inasema mbali na mafanikio mengi yaliyopatikana, ufadhili wa fedha kwa ajili ya kukabiliana na Ukimwi umepungua tangu mwaka 2014.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sasa wataachaje kuambukizana wakati watu wenyewe ndio hivyo tena. Mara leo Jokate na Alikiba mara kesho na Domo. Mara leo sijui Gigy Money na Idrissa Sultani kesho sijui na Ney wa Mitego, achili mbali ya Wema Sepenga na Kajala Masanja sijui na Ya Shishi Baby duh................na wataukwa sana mwaka huuuuuu

    ReplyDelete

Top Post Ad