WANASIASA wa Upinzani Burundi Wamkataa Mkapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mkapa amesema kuwa makubaliano yataafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka ujao.

Wanasiasa wa upinzani nchini Burundi walio uhamishoni wamepinga jitihada za aliyekuwa rais wa Tanzania za kutatua mzozo ulio nchini humo.

Hii inajiri baada ya William Mkapa kuwaambia waandishi wa habari kuwa si jambo zuri kuendelea kutilia shaka uhalali wa Raia Pierre Nkurunzia.

Nchi ya Buurndi ilitumbukia kwenye mzoo baada ya bwana Nkurunziza kutangaza kuwa angewania muhula wa tatu.

Mamia ya watu wameuawa na maelfu kukimbia nchi kulipozuka ghasia.

Bwana Mkapa alipewa jukumu la kusaidia kutatua mzozo huo, na amesema kuwa makubaliano yataafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka ujao.

Baadhi ya wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni wanatafutwa na serikali kwa kupanga maandamano ya kupinga hatua ya Rais Nkurunziza hatua ambazo serikali inazitaja kuwa za kihalifu.

Wengine waliilaumiwa wa kushiriki kwenye mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli mwezi Mei.

Source: BBC
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo Mkapa alishindwa hata kuiongoza Tanzania itakuwa kuutatua mgogoro wa Burundi kweli. Hapa Tanzania aliondoka akaiacha Nchi hoi bin taaban. Viwanda vyote viliuzwa ajira zikakosekana akabakia kujimilikisha mashamba na baadhi ya mali za serikali yeye pamoja na Sumaye. Huo mgogoro wa Burundi apatiwe msuluhishi mwingine lakini huyo Mkapa hauwezi. Tena hawezi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hawezi kweli. Yeye mwenye Mkapa ni kiongozi corrupt, atawezaje kusuisha nchi iliyo corrupt zaidi, kisiasa na kiuchumi vyote corrupt, Enzi za uongozi wake ulizaa matunda ya corruption

      Delete

Top Post Ad