Baada ya Bilicanas na Shamba, Serikali ‘Yakamata’ Hoteli ya Mbowe Arusha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


 Ikiwa ni takribani miezi mitano sasa tangu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe alipoondolewa katika jengo la Bilicanas lililokuwa pia na ofisi za Free Media na siku moja tangu serikali imzuie kuendeleza shughuli za kilimo kwenye shamba lake, kiongozi huyo amepata pigo jingine katika hoteli yake anayoimiliki.

Mbowe ambaye ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amepewa siku 14 na serikali awe amelipa kodi ya hoteli yake ya Aishi takribani TZS milioni 13.5 vingine vyo hoteli hiyo itafungwa.

Hoteli ya Aishi inayomilikiwa na Freeman Mbowe iliyopo Machame wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.


Uamuzi huu wa serikali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro umekuja siku moja tangu Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa alipotangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe kwa madai kuwa lipo katika eneo la chanzo cha maji cha Mto Weruweru.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa mujibu wa taarifa alizozipata kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Freeman Mbowe amekuwa akikwepa kulipa kodi kwa miaka mitano na kusababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji mapato.

Kwa miaka mitano imeelezwa kuwa Mbowe hakupeleka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hali ya mauzo yake ambayo inapaswa kutumika kujua ni kodi kiasi gani anatakiwa kulipa.

Kuhusu shamba lake, DC alisema kuwa shughuli za kilimo katika eneo hilo limepeleka uharibifu wa mazingira huku kiongozi huyo akivuna miti ya asili bila kibali cha Mkuu wa Wilaya kinachotolewa baada ya uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuwaleta waturuki na kuwadharalisha wawekezaji wa kitanzania wazalendo ni kumkatisha nguvu mwananchi.kumbana mtanzania na kumwacha mchina, nturuki, mwingereza, mmarekani, mfaransa kuihujumu Tanzania kwenye nguzo kuu za uchumi umiliki arrfhi, uuaji tembo, utorodhsji madini, kutolipa kodi ni kumrudisha mtanzania nyuma enxi za kikoloni.
    Ubabe unsotumika na viongozi wa chama tawsla, kama watanzania mnaufurshia bado hamjaelimika na kujua madhara yake.mmeona wanawske Amerika walivyoungana kwa maandamano na nchi nyingi duniani zikiwaunga mkono, hapa tanzania wangeweka makombola kuwashsmbulia. Narufia nikisema, hawa watu eote wawekezaji toka nje ni wezi wakuu.wsjanja. wamekaa kimya wakijua na kuchukua fsida wakiona wazi seriksli inawakuza kuwapa mianya na kuwanyanyasa wstanzania wanaojaribu. Wanajua wazi ESCROW iliiba sababu ni hao wslikuwa wabia wso.wameachwa huru ingawa wameiba na ni mafisadi wskuu wakitanzania wakishirikiana na viongoxi waliopita wa ngazi za juu.hawadhikiki. wsliofilidi mabilioni wspo huru bafo wanatamba nchini.sasa kinachotumbuliwa hspa ni nini ksma si kuwsfumbs macho wajinga wadioweza kufikiri na ta
    nzania wamejaa kibao.
    Ukisikia mtu anasifiwa kwelikweli na wstu wa nje, kidhawekwa mkononi naye hajijui.sifa zaua nchi yetu.mtu snayejiamini, shujaa, mwenye hekma hatsuzwa kwa sifa. Atakaa kimya na kujitathmini mwenyewe.
    Ukitaka kutumbua kiukweli, kuna viongozi wa juu maraisi , mawaziri, na baafhi ya washauri wao ambao ndio chsnzo cha matatizo yote makuu nchini mbona wapo huru, hata kuwagusa hujawagusa. Sasa tamtumbuaje aliyepewa kibarua na dingi ili atekeleze na dingi anasauti kuu serikalini bado.mfumo wa utawsla kuogopana wakuu ndio tatizo na janga linalokabiri nchi yetu. Mpska mfumo huu ubadilishe kupitia katiba mpya. Watanzania watakuwa na nguvu na sheria.kwa sasa serikali hsifuati sheria.

    ReplyDelete
  2. Umelichokoza balaa mwenyewe wewe unajijua kuwa ni bomu halafu kila kukicha unajifanya unapigania haki ya mtanzania masikini wakati rohoni mwako unajijua fika kuwa uyasemayo siku kweli sasa done blew u shit

    ReplyDelete
  3. Bla bla bla hatutaki kizisikia hapa ni kazi na haki ya ukweli kwa kila mtanzania kwani nchi hii si ya kwenu peke yenu enyi nyote akina Mr and Mrs Bla bla bla.....zisizokuwa na mpango enough is enough

    ReplyDelete

Top Post Ad