20 Percent 50 cent Abbas Kandoro Abdu Kiba ACT Act Tanzania ACT- Wazalendo Act-Wazalendo Adam Juma Adamu Juma Adamu mchomvu Afande Sele Africa AFRICAN BEAUTY PRODUCTS Afrika Kusini Afrimma 2015 Afumaniwa Afya Afya ya mama Diamond Agnes Masogange Agness Masogange AGP Mangu Aika Air France flight No 463 Air Tanzania Ajabu Ajali Ajali ya Basi Ajali ya Moto Ajali ya Ndege Ajira ajira za walimu AK47 AKA Akon awajibu wakenya Al shabaab Al Shabab Al-Shabaab terror Alale Alazimishwa Alberto Msando Ali Kiba Alikiba Alikiba Atazidi Kupitwa kila Siku Ally Kiba Aloe Vera Alshabaab Amanda Poshy amani Amatus Liyumba Amber Lulu Amber Rose Andrew Chenge Angry Kenyans Blast Davido for being Drunk and Rude at Concert Anna Makinda Anna Tibaijuka Anne Kansiime Anne Kilango Anne Kilango Malecela Anti-Foreigners Attacks Arusha Asha Baraka Ashanti Askari Askofu Gwajima Askofu Gwajima Azimia Ghafla Askofu Mokiwa Askofu Pendo Askofu Pengo Asma Platnumz AT ATCL Augustine Mrema Aunt ezekiel Aunty Ezekiel Aunty Lulu Awaacha njia panda Ay Azam fc Azam TV Baba Diamond Baba Haji Baba Kanumba Baba Levo Babu Loliondo Babu Seya Babu Tale baby madaha Baby_ake Badra Bagamoyo Bakheresa Bakita Bakwata Balozi Mwapachu Ban Kin Moon Bandari Bang Magazine Bangi Banza Stone Baraka Da Prince Baraza la Mawaziri Baraza la waislam Barnaba Basata Bashe Bastola Bastola iliyokamatwa Juzi Gwajima Anaimiliki Kihalali Batuli BAWACHA Zanzibar Bayo BayPort BBC Beautiful Onyinye wa Bongo belle 9 Ben Pol Benard Membe Benjamin Mkapa Benki ya CRDB imepanga kumjengea ukuta wa fensi wa nyumba ya Daimond Platnumz Benzema Besigye BET Betty Mbereko Beyonce Biashara Big Brother Africa Bikira wa Kisukuma Bilali Bilionea Binslum Tyres Bishop Piusi Erasto Ikongo Bob Junior Bob Marley Bobbi Kristina Boda Boda Bodi ya Mikopo Boko Haram Bomoa Bomoa Bomu mkononi Bond Bondia Mohamed Matumla Bongo Fleva Bongo Fuse Bongo Movies Bongo Star Search Bongo5 BOT Breaking News Bukoba Bulembo Bunduki Bunge Bungeni Burudani Busu la Wema Sepetu BVR Caitlyn Jenner Calisah Cannavaro Captain John Komba Cassim Mganga CCM CCM-B chadema Chagga Barbie Chama cha Mapinduzi Charles Kitwanga Chato Chege Chege Chigunda Chekecha Chekechua Chelsea Chemical Chibok Girls Chid Benz Chris Brown Chris Brown Kuwahamishia Mwanae na Mama Christian Bella Christiano Ronaldo Christopher Mtikila chuchu Hans Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Chuo kikuu cha Garissa Clouds FM Clouds TV CNN Coco Beach Colonel Mustapha confirmed 152 were killed including the four alleged terrorists. Cookie Copyright Society of Kenya Corazon Cosota court Crazy Photos Crazy Video CRDB Cristiano Ronaldo CUF CvpeopleAfrica D'banj Daftari la Wapiga Kura Daktari Feki Dallas Dangote Dar es salaam Dar Live Daraja la Kigamboni Darasa Dating Daudi Balali David Mataka Davido Davido Apost Picha Akiwa na Diamond Studio na Kuandika Ujumbe Uliotuacha njia Panda Davina Davis Mwamunyange DAWA ZA ASILI Dawasco Deci Defao Deo Mwanambilimbi Desmond Tutu Diamond Diamond Jubilee Diamond na Zari Diamond na Zari Roho Mkononi Diamond Platnumz Diamond Platnumz Amvisha Pete ya Uchumba Zari Diamond Plutnumz Diamond sio Mwanamuziki wa Kweli Anaimba Kiunjanja Tu Didas Masaburi Didier Drogba Dillish Mathews Dina Marious Disco Toto Diva Loveness Dj Choka DJ Fetty DJ Hunter DJ Majay Dk Kigwangalla Dk Mzindakaya Dk Shein Dk. Kigwangalla Dk. Makongoro Mahanga Dkt. Hamisi Kingwangalla DNA Dodoma Dogo Asley Dogo Janja Donald Ngoma Donald Trump Dougiesmasta Dr Cheni Dr Edward Hosea Dr Kessy Dr Mwaka Dr Shein Dr Slaa Dr. Asha Rose Migiro Dr. Kamani Dr. Kigwangalla Dr. Philip Mpango Dr.Edward Hosea Drake Dudu Baya Duka la Dawa Dully Sykes Dume Jike East Africa Radio/EATV Eatv Edo Kumwembe Edward Lowassa Edwin Mtei Edzen Edzen Jumanne Efm Radio Egypt Air El Chapo Eli Chapo Eliakim Maswi Elimu Elizabeth Emelda Emmanuel Adebayor Emmanuel Mbasha Emmanuel Mbasha Afunguka sakata la Gwajima Emmanuel Nchimbi Emmanuel Saimon Sewando ‘Manecky’. Empire Empire Season 2 Endlessfame Epa Erick Omondi Escrow Esha Buheti Esma Platnumz Ester Bulaya ester Matiko Esther Bulaya Ewura Ezekiel Maige Ezylinc Facebook Faini Faisal Faiza Ally Farai Mbereko Faraja Kota Nyalandu Farid Musa Fastjet Fatma Karume Fatuma Ayubu Fatuma Karume Feki Feza Boys Fezza Kessy Fid Q Fid. Fiesta Fiesta Condoms Fifa fight got dìrty Filamu Filamu Mpya Filikunjombe Fina Mango Fitness model Flaviana Matata flora lyimo Flora Mbasha Flora Mvungi Foleni Forbes Francis Cheka Fransic Cheka Freeconic Ideas Freedwa Freeman Mbowe Freemason Funny Stories Fuse ODG G-Nako Gabo Gadner Gadner G Habash GAG Gaidi Gaidi wa Kitanzania Gari Gari la Wema Garisa attack Garissa Garissa University Gays Gazeti la Amani Gazeti la Ijumaa Geita Geita Gold Mine Gerald Hando Geryson Msigwa Gesti Getrude Rwakatare Gigy Money Godbless Lema Gofu Gondwin Gondwe Goodluck Mlinga Google GPL Grace Msalame Gwajima Aachiwa kwa Dhamana Gwajima Afunguka Gwajima Avunja ukimywa H-baba Habari za Magazeti Habari za Nje Habib Mchange Hackers Haji Duni Haji Manara Haki Elimu Hali ya Hewa Halima Kimwana Halima Mdee Hamisa Mobeto Hanscana Harmonize Harusi Hasheem Hasheem Thabeet Hasna Ait Boulahcen Hassan Kessy Hawa Hawa Ghasia Haya Ndio Maelezo ya JB Kuhusu Watu Wanaotaka Kuigiza Naye Hemedy Henry kilewo High School Girls Hips HIV Status Hollywood Movies Home Shopping Hot Mix Hotel ama Restaurant House Girl Hoyce Temu Huddah Monroe Husna Hussein Machozi ICC Idara ya Uhamiaji idd Azzan Idris Idris Sultan Ikulu Ikulu.Sakata la Escrow IMF IMTU India Infosys IPS Instagram Instagram Parties Irene Paul Irene Uwoya Iringa is Fastjet is a Low-cost Airline or Not? Isabelah Mpanda Isha Mashauz ISIS Issaya Mwita Charles ITV Ivan Semwanga Ivo Mapunda Izzo Business Jack Chuzi Jack Cliff Jack Maisha Jack Pemba Jack Pentezel Jack Wolper Jackie Chandiru Jacob Steven Jacob Zuma Jaden Smith Jaguar Jagwani Jaji Ramadhani Jakaya kikwete Jamal Malinzi Jambo Leo James Bond James Cosmetics James Lembeli James Mbatia James Tupa Jamii Forums Janet Magufuli January Makamba Jay Z JB jela Jenerali Godefroid Niyombare Jeneza Jeneza la Lady Jay Dee Jengo Refu Africa Mashariki Jenista Mhagama Jennifer Lopez Jerry Muro Jeshi la kenya Jeshi la Kujenga Taifa Jeshi la Polisi Jestina George Jihad John Jiji la Dar Jike Shupa Jimbo la Bunda Jini Kabula JK JKT JNIA Job Ndugai Job Opportunity Job Vacancy Joh Makini Johari John Dillinga John Heche John Magufuli John Mnyika John Terry Johnson Minja jokate Jokate Afunguka Jokate Atia Aibu Jokate na Ali Kiba Jokes Jose Chameleone Jose Kusaga Jose Mourinho Joseph Butiku Joseph Mbilinyi aka Sugu Josephat Gwajima Josephine Mushumbusi Joshua Nasssari Joti Joyce Kiria Jude Okoye Juliana Kanyomozi Juliet Kairuki Julius Mtatiro Juma Abdul Juma Duni Juma Jux Juma Mwapachu Juma Nature Juma Nkamia Juma Nyosso Justin Bieber Jux Jwtz K-lyin Kabali EFM Kadi za CCM kafulila KAGERA Kahaba Kahama Kajala Masanja Kaka yake Zari Kakobe Kala Jeremiah Kalapina Kamanda Kova Kamanda mkoa wa Arusha Kamatia Chini Kamikaze Kamishina Mkuu Kanye West Kariakoo Karrueche Karume Kasi ya Magufuli Kasoro DART Kassim Mganga Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Katibu Mkuu wa Chadema Katunzi Kauli ya Shilole Kayumba Kcee Kenya Kenya Airways Kenyan Member of Parliament Kenyan News Kesi KEYSHA Kibaki kidoa Kifo Kigaidi Kigamboni KIGOMA Kilimanjaro Kill Music Awards Kim Kardashian Kinana King Crazy GK King Lawrenc Kingereza Kingunge Kingunge Ngombale Mwiru Kingwendu Kinje Kinondoni Kinyume na Maumbile Kipaji Kipindupindu Kipondo Kisumu Kiswahili Kitandani Kitila Mkumbo kituo cha Azam TV kituo cha Polisi Kiuno bila Mfupa Kizimbani Kobe Kocha Koffi Olomode Komedi KOVA KTMA Kubaka Kubemenda Mtoto Kubenea Kucheza Filamu Kufika Kileleni kufumaniwa kufunga ndoa Kujichubua Ngozi Kukandamiza Uhuru wa Habari Kumpa Raha kupaka poda kupendwa na wadada Kupima DNA Kura za Maoni Kurefusha Nywele Kutongoza Wanawake Walioolewa ni Rahisi Kuliko Wasioolewa.. Kuwa Original Kuwachinja Mateka Kuwait Bombing kwenda Bara yenye mabehewa 22 imeanza safari kwenda Kigoma Kyela Kylie Lady Jay Dee Lamar Odom Latiffah Naseeb Abdul Lawrence Masha Lema Lemutuz Leonardo DiCaprio Lesbians Liberatusi Sabas Lil Wayne Linah Sanga Linex Lionel Messi Lipumba Listzetu.com London Lost Generation Love Love Advise Love Boat Lowassa Lubuva Lucy Komba Lucy Mayenga Ludewa Luis Luku Lukuvi Lulu Diva Lulu Michael Lupita Nyong'o Lusinde Luten Karama Maafa Maajabu Maajabu ya Lowassa Maalim Seif Maandamano Maarufu Peter Maaskofu Wamjibu Rais Kikwete Mabasi ya Mwendo Kasi Mabasi ya UDA Mabeste Mabibo Hostel Mabomu ya Machozi Mabula Mad Ice Madam Rita Madawa ya Kulevya Madee madereva madereva wavyombo vya usafiri Madini ya Almasi Madness Mafikizolo Mafinga Mafuriko mafuriko dar Mafuriko ya Lowassa Magaidi Magari ya Kifahari Magazeti ya Leo Mahakama Kisutu Mahakama mkoani Dodoma Mahakama ya Kazi Mahakama ya Kimataifa ICC Mahindi Mabichi Mahips Mahojiano baina ya Jeshi la Polisi Mahusiano Maimartha Jesse Mainda Maiti Majaliwa Kassim Majambazi Majanga Majengo Marefu makahaba Sinza Makalio Makalio Fake Makamba Makanisa ya Kiroho Makapi Make me Sing Makerere University Makongoro Nyerere Makontena Makosa ya Mtandao Malaika Mali Asili Malia malkiawaisnta Mama Diamond Mama Kanumba Mama Lulu Mama Nyerere Mama Ongea na Mwanao Manaiki Sanga Mange Kimambi Mangula Manji Manyaunyau Manyika JR Mapaja Mapanga Mapenzi Mapenzi Raha mapenzi ya Jinsi Moja Marando Marekani Maria Nyerere Mark Mwandosya MARKSON BEAUTY PRODUCTS Marlaw Mart Nooij Martin Kadinda Mary Nagu Masanja Masanja Mkandamizaji Mashehe Masheikh Mashine za BVR Mashoga Maskini Jeuri Masogange Masoud Kipanya Mastaa Bongo Mastaa Hodari Kuficha Mimba Master J Mateso Mathias Chikawe Matokeo Kidato cha Nne Matokeo ya Darasa la Nne Matokeo ya Darasa la Saba Matokeo ya Kidato cha Nne Matokeo ya Kidato cha Sita Matokeo ya Uchaguzi Matokeo ya Urais Matokeo ya Wabunge Matonya Matusi Mtandaoni Mauaji Mauaji ya Albino Mauaji ya Kimbari Mauji Mawazo Mawio Max Rioba Mayai ya Kware Mayweather Maziwa Mtindi Mb Dog Mbao FC MBDog Mbeya Mbio za Mwenge Mbio za Ubunge Mbio za Urais Mboni Show Mbowe Mbunge Mbunge Shyrose Bhanji Afunguka Ugonjwa Unaomsumbua Mbunge wa Mbeya Mbuta Nanga Mbwana Samatta Mc Pilipili Mch. Gwajima Amgomea Makonda Mchepuko Mchungaji Mwingira Mchungaji Peter Msigwa Mdahalo Mduara Meck Sadick Media Bar Meek Mill Meji Alabi Mengi Meninah Meno ya Tembo Meya Dar Mez B Mfalme wa Qatar Mfanyabiashara Mganga Mgao wa Umeme Mgombea Urais Mgomo Mgomo wa Madereva Mhe. Balozi Ombeni Sefue Mheshimiwa Ndugai Micah Johnson Miche Michepuko Michezo Midahalo Migiro Mikoa Duni milion 13 Millard Ayo Millen Magese Mimba Mimba ya Zari Mipasho Bungeni Mirrow Miss Tanzania Miss Universe Miss World Miss World 2015 Mita za Luku Mitandao ya Kijamii Mitumba Mizengo Pinda Mizinga Mke wa Dada Mke wa Dr Slaa Mke wa Lowassa Mke wa Mtu Mke wa Mtu Afumaniwa Mke wa Rafiki Yangu Mkemia mkuu Tanzania Mkito Mkude Nsiba Mkutano wa CCM Mkuu Mkoa Mkuu wa Jeshi Mkwasa Mlima Kilimanjaro Mnyika Mo Dewji Mo Music Mohamed Ali Mohammed Dewji Mombasa Monalisa Monduli Moses Iyobo Moza Mpoto Mr Blue Mr Bond Mr Nice Mramba Mrema Mrembo mrembo afia china Mrisho Mpoto Mrisho Ngasa Msaga Sumu MSD Mshipa wa Aibu Msiba Msichana Mtanzania Akamatwa kwa Ugaidi Kenya Msuva Mtabiri Mtandao wa Instagram Mtangazaji Charles Hillary Mtanzania Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo Mtikila Mtoto Auwawa na Mbwa mtuhumiwa Mtuhumiwa wa Mauji MTV Base MTV Mama Mtwara. Muadhama Polycarp Kardinali Pengo Mugabe Muhimbili Muhongo Muigizaji wa filamu Mukeyamuganda MultiChoice Africa Muonekano wa Kupendeza museven Music Muswada wa Sheria ya Mtandao 2015 Muuguzi Muungano Muungwana Blog Mvua ya Mawe Mwadhama Polycarp Kardinari Pengo Mwakyembe Mwalimu Mwalimu Nyerere Mwami Radjabu Mwamvita Makamba Mwana FA Mwanafunzi Mwanafunzi wa Chuo Mwanahalisi Mwanamke Bikira Mwanamuziki Suma Lee Mwananyamala Mwanasheria Mkuu Mwanaume sahihi Mwanza Mwendokasi Mwenyekiti CCM Akutwa na Fuvu la Kichwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mwenyewe Akiri Kuishi kwa Hofu Mwigizaji Lulu Michael Apachikwa Ujauzito Mwigulu Nchemba Mwimba Injili Flora Mbasha na mumewe Mwinyi Mwisho Mwampamba Mwizi Mzee Majuto Mzee wa Swaga Mzee wa Ubuyu Mzee wa Upako Mzee Yusuph Mzungu Kichaa Na Yule Nafasi za Kazi Nahreel Naibu Spika Naima Nairobi Naj Nakaya Nakosa Raha Nana Nancy Sumari Nani Mkali Naomba Wema Sepetu Umsamehe Kajala Naombeni Msinilaumu Nape Nape Nnauye nasema nawe Natamani Kufanya Mapenzi Nauli za Mabasi Navio Navy Kenzo Nay wa Nay wa Mitego Nazizi NCCR-Mageuzi Ndikumana ndoa kubuma Ndoa ya Wema Sepetu Ne-yo Nec Necta Neema Herbalist Nehemiah Mchechu Nelly Kamwelu New Video Ney wa Mitego Neyo ngono Nguo fupi Nguvu na ushawishi wa Lowassa waongezeka maradufu Nguvu za Kiume NHC Nick Minaj Nick wa Pili Nida Nigeria Niki wa Pili NIMR Nisha Nisher Niva Nizar Khalfan Nora Nssf Nuh Mziwanda Nuhu Mziwanda Nusu Utupu Nyalandu Nyama ya Binadamu Nyanyasaji Nyayo Estate Nyimbo Mpya Nyoka Nyumba ya Diamond Obama Odama Ole Sendeka Omba Omba Ombeni Sefue Ommy Dimpoz Omotola Opareshi Tokomeza Open Letter Orijino Komedi Osama Bin Laden Oscar Oscar Pistorius P Square P-Square Pacquiao Padri Panya Road Papa Francis Papa Msoffe Papa Wemba Paul James Paul Kagame Paul Makonda Paul Pogba Paula Pembe za Ndovu Penny Penny: Huu Usista Duu Utatumaliza Wasichana Bongo Pete ya Uchumba Peter Kuga Mziray Peter Msigwa Peter Serukamba Petitman Phina Mango picha Picha Chafu Picha za Nusu Utupu Picha za Uchi Picha za Utupu Picha Zingine za Wema Sepetu na Idriss PINGU NA DESO Pipi Pius Msekwa Planet Bongo PNC Polisi Pombe Pope Francis Portugal Precision Air Service President Museveni Prodyuza wa Bongo Fleva Prof. Beno Ndulu Prof. Ndalichako Profesa Ibrahim Lipumba Profesa Muhongo Profesa Mwesiga Baregu Professor Jay Promosheni Promotion Pwani Q-Chilla Qeen Susy Quick Rocka Radio5 Rah P Raha ya Mapenzi Rahco Raila Odinga Rais Kikwete Rais Maskini Rais Nkurunziza Rais wa Burundi Rais wa Rwanda Ramada Hotel Tanzania Ramadhani Mungi Ramadhani Singano Rambo Ramesh Patel Rammy Rammy Gallis Rashid Charles Mberesero Ray Ray C Ray Kigosi Raymond Rayuu Rayvanny Red Bull Regina Lowassa Richard Kasesela Richi Mavoko Richmond Ridhiwani Kikwete Rihanna Riri Rished Bade Risper Faith Riyama Ally Robert Mugabe Rockstar4000 Roma Rommy Jones Roper Rosa Ree Rose Mhando Rose Migiro Rose Ndauka Rostam Aziz Royal Regency Rubega.com Ruby Ruge Rugemarila Rushwa Russia Ruto Rwanda sababu za Kutokuoa Sabby Angel Sabuni Express Saed Kubenea Safari Lager Safari za Nje Safina Said Fella Said Lugumi Saida Karoli Sajuki Sakata la Kumtukana Sakata la Operation Tokomeza Salama Condoms Salama Jabiri Salima Salma Said Salma Salmini Salome Sam Mahela Sam Misago Samantha Samia Hassan Suluhu Samson Mwigamba Samweli Sitta Sanchoka Sarafu ya Shillingi Mia Sauti Sol Sayansi SBL Seck Sehemu za Siri Selcom Seline Sepp Blatter Serena Hotel Serena Williams Serengeti Serengeti Boy Serikali Shaa Shaban Kado Shaffih Dauda Shambulio la Garissa Shamsa Ford Sheddy Clever Sheikh Ponda Issa Ponda Shetta shibuda Shida Gari Shika Adabu yako Shilole Shilole Akiri Shinda Gari Shinyanga Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Shopping sias Siasa Siasa Huru Siha Siku 100 za Rais Ikulu Simba Simbachawene Simon Msuva Simu Feki Singano SINGIDA Single Mtambalike Sintah Siri Imefichuka Siri yafichuka Siri Yafichuka Kumbe Wasanii Wengi wa Bongo Hawampendi Wame Sepetu Sitta Sitti Mtemvu Siwema Siyo siri Skendo Slider Slim Snura Snura Mushi Socialite Solo Thing Somalia Sonko Sonkoro Soudy Brown South Africa Spa and Beauty Parlour Spika wa Bunge Sporah Show Staa Staa Mrembo staa wa sinema Bongo Stamina Stan Bakora Stara Thomas Startimes Stella Tillya Steve Nyerere Steve Wasira Stories Strabag Sugu Sukari Suleiman Kova Sumaye Sunday Mangu ‘Linex Supu ya Pweza Taadhari Taarifa Kwa Umma TABORA Tabwe TACCEO Taifa Stars Taifa ya Uchaguzi Takururu Tambua Aina ya Wanaume wenye Mvuto zaidi kwa Wanawake Tamisemi Tamko la Al-shabaab Tanapa Tanesco Tanga Tangazo Tanzania Tanzania Bloggers Network (TBN) Tanzia Tarime Tasaf Tazara TB Joshua TBC TBC1 TCRA TCU Team Kiba Team Wema Team Wema Wakwera na Tabia ya Watu Kumzushia Wema Technology Tecno Tekno Miles Temba Tendo la Ndoa Tendwa Tetemeko Tevez TFDA TFF The guy who sat on nothing The Industry The Mboni Show The Most Beautiful Policewoman in Kenya Thereza May Thomas Ulimwengu Tiara Tiba Mbadala TID Tigo Tiko Tip Top Connection Tishio la Ugaidi Toyota TPL TRA Trace TV Treni Treni ya kisasa (Delux) Trust Divas TTCL Tuhuma Tukio la Ujambazi Tulia Ackson Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tunda Tundu Lissu VS Zitto Kabwe Tundu Lisu Tusker Fanya Kweli Tuzo za Watu Tyga TZA u-turn UAP Ubakaji Ubunge Ubungo Uchaguzi Mkuu Uchaguzi Zanzibar Uchawi Uchumi UDA Udaku Udaku App Udaku Leo Udaku Spe Udaku Special Udaku Speshi Udaku Spesho Udaku TV Udaku_special udsm ufasaha Ufisadi Ugaidi Uganda Ugandan News Uhuru Kenyatta Ujambazi Ujangili Ujauzito Ujauzito wa Aunty Ujauzito wa Zari UK ukatili Ukawa Ukuta Ukwepaji wa Kodi Ulanga Goodluck Mlinga Ulikuwa Wapi Ulinzi Umalaya Umeme Umoja wa Mataifa Unyama Unyanyasaji Upaja Upinzani Urafiki Urais 2015 Urembo USA Usagaji Ushauri Ushirikina Ushoga Ushuru Usicheze Mbali Ustadh Juma na Musoma Utafiti Utafiti wa Gesi Utajiri wa Kutisha utamaduni wa kiafrica Utangazaji Utapeli UVCCM Uvumi Uwanja wa Maigizo Van Gaal Van Vicker Vanessa Mdee Vera Sidika Video chafu Video Mpya Video Qeen Video ya Davido akimponda Diamond Vigodoro Vigogo TRA Vigogo TRL Vincent Kigos Vipodozi Viroba Virusi vya Ukimwi Vitambi Viungo vya Albino Viwanda vya Mikorogo Vikizimwa VJ Penny Vodacom Vurugu Vurugu Burundi Vyeti Feki Vyombo Vya Habari Wabogojo Wabunge Wabunge wa Upinzani Wachaga Wafuasi wa Gwajima Wafuasi wa Lowassa Wafunga Doa.Diamond Platnumz waganga Wahalifu wa Mitandao Waislam Waitara Wakili Awadh Ali Wakuu wa Wilaya Walemavu Walinzi wa Chadema Wame Sepetu Wamsindikize Wanafunzi Wa Vyuo Vikuu Jijini Mwanza Wanaigeria Wafanya Kweli Wakipiga Chini Chama Tawala Wanaijeria Wanajeshi Wanakea Wanakwaya Wanamgambo wa Kislam Wanaume Ndani ya Ndoa Wanaume Walevi Rombo Wanaume Warefu Wanawake Bikira Wanawake Mabubu na Magogo Wanawake Ukawa Wang Xin Hua Wanjera Warembo Warioba Wasafi Records Wasambaza Picha za Utupu na Ngono na Wasambaza Uongo Mitandaoni Kwenda Jela Miaka 10 ama Faini Mil 50 Wasanii Wasira Wassira Wastara Watuhumiwa Waume za Watu Wayne Rooney Waziri Abdalah Kigoda Waziri Maghembe Waziri Mkuu Wazo Huru wellu Sengo Wem Sepe Wema Aonyesha Pete Yake ya Uchumba Wema Daily Wema na Diamond Wema Sepetu Wema Sepetu amefunguka Wema Sepetu na Idris Wenje Wezi wikii hii alipokua Kenya. William Lukuvi William Malecela William Mhando Wimbo Mpya Wivu wa Mapenzi Wizara ya Afya Wizara ya mambo ya nje Wizkid xenophobic attack Ya moto Band Yabainiki Kwake ulinzi ni Sifuri Yagongwa Yamoto Band yanga Yaua Askari Polisi Wawili Kwa Kutumia Panga Yaya Toure Yemi Alade Yound D Young D Young Dee Yussuf Manji Yusuph Mlela Z Anto Z ANTON na Nk Zacharia Express Zamaradi Zamaradi Mketema Zamaradi na Ray C Zanzibar Zari All White Party Zari Hassan Zari is far away from Wema Zari The Lady Boss Zari Vs Wema Zari White Party Zawadi ZEC Zitto aichokoza Chadema na kuwapa somo wanachama wake Zitto Kabwe Zitto Kabwe Ameshinda Nafasi ya Kiongozi Mkuu wa- ACT Wazalendo Ziwa Victoria Zungu

AWALI ya yote, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda, kutupa uhai na afya njema hadi leo. Yote yamewezekana kwa kuwa amependa sisi wajoli wake tuwe hai na wenye afya.

Wako wenzetu wakati huu wako hospitali au vitandani kutokana na maradhi mbalimbali. Tuwaombee wote walio wagonjwa.

Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kujua kwanini wengine kawapa afya njema na wengine kawapa maradhi ya aina mbalimbali. Inawezekana kati ya mnaosoma makala hii sasa, wengine hamtaweza kuuona mwaka 2018.

Ndugu zangu Watanzania, ili tuweze kuwa na matumaini ya mwaka mpya wa 2017 tuliouanza, ni vema takatafakari mwaka tunaouaga wa 2016.

Huu ni mwaka wa kwanza tangu Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, ambapo tulimpata Rais mpya, John Magufuli na kuunda serikali yake. Ni dhahiri kila tunapoingia kwenye uchaguzi, kila mmoja wetu huwa na matumaini ya matokeo ya uchaguzi kuleta unafuu katika maisha yetu ya kila siku.

Ndio maana wakati wa kampeni, tunasikiliza kwa umakini sera mbalimbali zinazoletwa kwetu. Hatimaye tunapiga kura kuichagua ile sera ambayo kila mmoja kwenye nafsi yake anaamini itamletea unafuu, itamtoa pale alipo kuelekea kwenye maisha bora.

Kwa wengine ni matumaini ya kutoka kwenye maumivu ya maisha kwenda kwenye unafuu. Kwa uzoefu wangu wa ubunge wa miaka 15 na miaka 20 kwenye siasa( active politics), ninaelewa kabisa kuwa wako ambao siku ya pili baada ya uchaguzi wanataka kuona kero zao zimeondoka.

Kama tatizo lilikuwa maji safi na salama, hawaelewi, baada ya kumpata kiongozi kwanini siku ya pili, ya tatu, mwezi na hata mwaka baadaye hakuna maji!

Hii ni hali ya kawaida kwa binadamu. Mimi nilichaguliwa na watu wa Karatu kutokana na kero kubwa ya maji wilayani Karatu. Maji yalidhalilisha utu wa binadamu hasa akinamama.

Maji yalifanya watoto wadogo kubakwa kwenye vituo vichache vya maji vilivyokuwepo. Maji yalifanya mahudhurio ya watoto shule za msingi yadorore kwa kuwa watoto walikesha usiku kucha kusubiri maji kwenye vituo vichache vya maji.

Nakumbuka kila nikipita mitaani, nilianza kuitwa tapeli kwa kuwa miezi sita baadaye, na kisha mwaka mmoja baadaye, maji yalikuwa hayajaonekana kwao. Mwananchi wa kawaida yeye hajui jitihada unazofanya kuleta maji.

Yeye kazi yake ilikuwa kupiga kura, mengine hayamhusu. Hajui kuwa maadui zako wanakuhujumu na kukuvuta chini ili usifanikiwe, kwani kufanikiwa kwako ni kuonyesha udhaifu wao.

Mwananchi haelewi kuwa mikakati ya utekelezaji wa mradi wowote haina budi kuandaliwa kwa umakini, fedha zitafutwe, kazi ya usanifu lazima ifanyike.

Kwa Karatu, maji yalianza kutoka kwenye mabomba mwaka 2000, wakati uchaguzi ulikuwa 1995. Tone la kwanza la maji lilipotoka, wananchi hata waliokata tamaa, waliodhani wametapeliwa walilipuka kwa furaha ya ajabu.

Walisahau matusi yote waliyokuwa wamenishushia. Sasa wakaanza kubaini kwamba kumbe hawakuwa wakidanganywa. Waliokuwa wavumilivu waliona na kushuhudia hatua zote za utekelezaji wa mradi.

Waliokuwa wepesi kukata tamaa nusura watukatishe tamaa sisi watekelezaji kwa kejeli, kebehi, matusi tuliyokuwa tukimwagiwa mitaani.

Uvumilivu ulizaa matunda. Wananchi takribani 30,000 walipata maji ya uhakika ndani ya nyumba zao, wengine katikati ya kitongoji chao, vitongoji vingine vilikuwa na DP ( Distribution Points) zaidi ya mbili au tatu.

Hivyo mama anaenda na sufuria na akirudi anabandika jikoni. Hili ni tunda la uvumilivu. Ndugu zangu nimeeleza kidogo kwa kirefu hadithi hii ambayo ilinipata mimi na wananchi wangu wa Karatu.

Ninafahamu pia kwamba mara baada ya ushindi wa Magufuli, makundi tofauti ya wananchi yatakuwa na matumaini tofauti kuhusu matarajio ya nini watakachokipata.

Wamachinga walijua mikopo midogo midogo itapatikana kwa urahisi, na hawatakimbizwa tena mitaani kama mbwa. Bodaboda waliozuiliwa kuingia katikati ya miji walijua sasa wamefunguliwa milango na hivyo biashara yao itakuwa rahisi.

Hali hii iko hivyo kwa takribani makundi yote ya kijamii. Kwa miaka mingi, wananchi wetu wameaminishwa kuwa nchi yetu ni tajiri na hivyo wana matarajio makubwa kwa viongozi wao.

Tuna rasilimali za kila aina kuanzia rasilimali chini ya bahari na maziwa yetu, magogo kwenye misitu yetu, rasilimali wanyamapori, ikiwa ni pamoja na “twiga wetu” aliyekunjwa shingo na kuingizwa kwenye ndege kutoroshwa.

Kuna kero nyingine pia kama vile maelfu ya tembo na faru waliokuwa wakiuawa bila huruma na majangili kwa manufaa yao binafsi, fedha zetu kwenye benki kuibiwa hovyo nakadhalika.

Wananchi haohao wamesahau kuwa mara baada ya uchaguzi, kazi kubwa ni mapambano dhidi ya “ wahujumu hao”. Kwa bahati mbaya “mpira usiocheza hujui si rahisi kujua ugumu wake. Kumbe hata ukiachiwa peke yako ufunge bao kwenye goli lililo wazi, unaweza kuupaisha juu kwa mshangao wa wengi!”

Hivi ndivyo ilivyo kwa serikali. Natambua kabisa watumishi wa umma walitegemea mishahara itapanda na kukidhi mahitaji yao, wanafunzi wa vyuo walijua mikopo sasa itakuwa rahisi na itatoka kwa wakati.

Wazazi walijua “ elimu itakuwa bure hadi kidato cha nne” na hawatasumbuliwa tena, hata kero ya madawati itatatuliwa bila mwananchi kuguswa kabisa! Natambua kuwa matamanio hayo si tu hayakutekelezwa bali maumivu yalikuwa makubwa zaidi kwa mwaka wote wa 2016.

Mitaji imepotea, mabenki hayakukopesha kwa hofu mbalimbali, mzunguko wa fedha ulikauka, hata wenye mitaji yao midogo ikaliwa. Hoteli nyingi kufungwa kwa kushindwa kulipa mikopo kutokana na kutokupata wateja.

Watumishi wa umma hawakupewa mishahara iliyotangazwa kupanda. Hii ni hali ngumu na ninatoa pole sana kwa wale wote, kwa makundi yao, walioumia kwa namna moja au nyingine.

Kazi ya kwanza ya kiongozi yeyote makini anaposhika dola ni kuangalia mianya mbalimbali ya wizi na uozo wowote katika usimamizi wa rasilimali za umma. Nadhani wote tunakiri serikali hii ilipoingia tu madarakani, jambo la kwanza lilikuwa kubaini wafanyakazi hewa.

Leo tunazungumzia wafanyakazi hewa takribani 20,000. Fikiria ni mabilioni mangapi kwa mwezi yalienda kwa wafanyakazi hewa? Ni dhahiri fedha hizi zingelitengeneza mzunguko wa fedha kama zingelikuwa kwenye mkondo sahihi. Hakuna shaka kwenye hilo.

Lakini ni wafanyikazi hewa, hivyo taifa halikuzalisha kutokana na wafanyakazi hao hewa. Ghafla uhakiki unaonyesha kuwa kuna siyo tu waalimu hewa, lakini wanafunzi hewa zaidi ya 60,000. Mungu atusamehe!

Sijui tumelogwa! Taifa la ajabu. Watu “wanatumbua” bila aibu. Hawa walikuwa wakitumbua fedha zetu kwa manufaa ya “ matumbo yao” na familia zao.

Hatujakaa sawa tukaambiwa kuwa hata fedha za TASAF zilizolenga kusaidia kaya maskini sana nazo zimeliwa. Kaya takribani 55,000 zilizokuwa zinufaike zimekosa huku baadhi ya viongozi wa serikali wa ngazi mbalimbali, wakiwemo maofisa wa TASAF wenyewe wakidaiwa kuhusika na wizi huo.

Hatujatulia mara maelfu ya wanafunzi ambao hawakuwa na sifa za kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu walipewa nafasi! Ni dhahiri kuwa wazazi wa watoto waliofukuzwa wameumizwa na hatua hii.

Lakini ipi nafuu kuendelea kuwa nao na kuathiri ubora wa elimu hasa katika dunia ya leo ya ushindani. Wenzetu kila siku wanapambana na ugunduzi wa mipango ya kwenda kwenye sayari mbalimbali kwa lengo la kutafuta sayari yenye kufaa kwa maisha ya binadamu.

Sisi tutaendelea kuwa na mijadala ya kutafuta fefha kwa matundu ya choo. Hadi lini! Najua lilikuwa uamuzi Mgumu sana Mhe. Rais na Waziri wako wa Elimu. Lakini hapakuwa na njia.

Nashukuru kama wazazi mlifanya jitihada za kuwaelekezea vijana hao penginepo ili rasilimali watu za Taifa zisipotee na wao pia wanufaike na rasilimali za Taifa lao. Ni haki yao.

Haikuishia tu kwenye fedha. Bandarini Kontainer zaidi ya 11,000 zinaingizwa bila kulipiwa kodi na ushuru mbalimbali. Hii ikasababisha milango na mirija ya ukwepaji kodi kufungwa.

Na dhihiri waliokuwa wakinufaika na kupata “ super profit” kwa kukwepa kodi wataikimbia Bandari yetu. Kitendo cha kuikimbia Bandari, kwa muda athari yake ni kuwa bidhaa zitapungua, na makusanyo ya kodi za Serikali pia yatapotea.

Mzunguko wa fedha katika ujumla wako nao utapungua. Na hivyo hali ya maisha kuwa ngumu kwa kila kundi.

Ndugu zangu, kwa kiongozi yeyote jasiri, mwadilifu, mpenda Taifa lake anakutana na mtihani mkubwa sana. Aidha ni uchaguzi mgumu. Au aache uozo huo wote kuanzia “ hewa” hadi “ ukwepaji kodi uendelee au audhibiti kwa njia zote zinazowezekana.

Akiuruhusu maana yake nimkuwa mzunguko bandia wa fedha utaendelea kuwepo na kundi dogo linalofikiwa na mzunguko huo litaendelea kunufaika lakini umma mpana utaendelea kuumia, kama tulivyokuwa tukiumia kabla ya uchaguzi.

Kwa bahati mbaya walio wengi ambao walikuwa hawanufaiki na uozo uliokuwa ukiendelea hawakuwa na pa kusemea. Leo angalau wamempata Rais anayewasemea wao. Rais amekuwa akitumia neno “wapiga dili”.

Ni kweli waliokuwa wakinufaika ni hao wapiga dili waliotengeneza “ wafanyikazi hewa, hewa, hewa, kila sekta”.

Lakini kwa bahati mbaya wanaoathirika ni pamoja na mama lishe, na wafanyibiashara ndogo ndogo ambao kimsingi hawahusiki kwa lolote lile na kupiga dili.

Wao wanafanya biashara wakati hao wachache wakipiga dili. Lakini hapa ndipo palipo na msemo, “mtego wa panya kuwakamata wahusika na wasiohusika”. Hii ndio inayoitwa “Dilemma”.

Unachagua kipi? Uache uozo na ufisadi/ huu mkubwa uliofilisi nchi nzima uendelee kwa ajili ya kuwasaidia wenye biashara ndogondogo au funga njia, kwa muda tutaumia, rudisha nchi kwenye reli na baada ya muda fungua milango kwa biashara halali.

Kweli kwa uamuzi huu liko kundi litaumia sana. Lakini taifa likirudi kwenye reli, kundi hilo na wote tutanufaika. Taifa zima litanufaika.

Nina hakika tukiisha kurudi kwenye mstari ajira zitatoka kwa utaratibu unaotakiwa, fedha za miradi zitatoka na mzunguko wa fedha utarudi kama kawaida. Maamuzi magumu yanahitaji kushirikiana lakini pia uvumilivu mkubwa. Hakuna jambo jema linapatikana kirahisi.

Najua kuwa kuna wengi wanalalamika. Wako wasomi kati yao. Lakini kama wasomi hao wana dhamira njema, miaka yote nchi ilipokuwa inatopea kwenye dimbwi la ufisadi, uwizi huu; mbona walikaa kimya?

Mbona hatujusikia sauti yao. Wasomi hao wengine wao si ndio walikuwa pia wakikusanya mamilioni wakati mwingine kwa “Dola Za Marekani” kwa kilichokuwa kikiitwa kazi za kiushauri yaani Consultancies?

Wengine walikuwa wakiandika rasimu za sheria mbovu lakini wakiishia kujikusanyia mamilioni ya fedha. Kwa bahati nzuri sizungumzii nadharia. Ninayafahamu yote ninayosema kwa undani.

Mambo ya “ Watumishi hewa”, wanafunzi hewa Kamati ya Bunge ya Hesabu ya Serikali za Mitaa tulianza kuyazungumzia mwaka 2007. Mbona tangu wakati huo wakati huo hatukumwona msomi yeyote akifanyia utafiti ( hata baada ya kuwarahisishia kwa taarifa za LAAC).

Tuache kudanganyana. Hawa wasomi wetu hawakuona huo ufisadi , wizi na uozo huu wakati ulipoanza ? Leo ndiyo wanaona uchungu au kwa sababu kwa namna moja au nyingine na wao pia wameguswa? Japo si wasomi wote.

Watu wanalalamikia safari za nje kuzuiwa. Tena wanaihusisha na mgawanyo wa mamlaka na kuwa Rais anaingilia mamlaka zingine. Hivi mwaka 2014 nilipotaka Bunge kufanyiwa “Special Audit” kwa ziara za kibunge zilizokuwa zikitumbua fedha bila manufaa kwa taifa walikuwa wapi?

Ni sekta ipi katika nchi yetu ambayo haikuguswa na Ufisadi? Hatimaye mwajibikaji mkuu wa fedha za Umma ni Rais kwa mujibu wa Katiba. Iweje basi akichukua hatua ionekane kuwa ameingilia mamlaka zao?

Ni kweli siyo kila kitu cha Serikali ya Awamu ya Tano mimi naunga mkono. Mimi siungi mkono kujenga reli kwa fedha nyingi kwa Standard Gauge. Labda tuambiwe kuwa wakati inajengwa kwa Standard Gauge wanazungumzia pia Electrification.

Nilikwishasema “ we do not have to re- invent the wheel”. Leo unatoka Hamburg kwenda Munich Ujerumani takribani umbali wa kilomita 1500 kwa muda wa saa 3 tu. Sisi tunakwenda Dar- Mwanza na treni inachukua siku tatu hadi nne.

Hii ni karne ya sayansi, hatuhitaji kuwekeza fedha kama hatutaenda kisasa. Inatakiwa mtu alalale nyumbani kwake Mwanza anaenda kufanya kazi Dar na kinyume chake.

Tunataka bidhaa za viwanda na za kilimo zizalishwe kwa wingi Mwanza, Mbeya na Kigoma na zifike katika Bandari ya Dar es Salaam kwa muda usiozidi saa tatu na si baada ya wiki.

Nchi hii haiwezi kuendelea kwa namna ya kufikiri ya mwaka 1947. Wasomi wetu wana jukumu la kujitafakari na kubadilisha namna yao ya kufikiri na kutoa mchango kwa taifa kama wanahitaji tuwatambue kwa usomi wao.

Wanasiasa wetu nao ajenda isiwe kuingia Ikulu pekee. Ajenda iwe namna ya kuliondoa taifa kwenye “ mduara” ( Vicious Circle) tulioko na mkakati walio nao wa kulipeleka taifa tunakotaka.

Kwa ujumla nchi ilikosa mtu wa kusimamia rasilimali. Nchi ilikosa mtu wa kutoa maagizo na maamuzi. Nchi ilikosa usimamizi na mtu wa kukemea. Rais JPM amejidhihirisha kuwa anayo nia, anayo dhamira na anao ujasiri na uwezo wa kufanya.

Chanzo: Gazeti la Raia Mwema, JAN 05, 2017.

Mwandishi wa makala hii aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Karatu kupitia chama hicho.

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa


Labels:

Post a Comment

  1. Tawile baba........kwa sasa mafisadi 'wanakodo-kodo' ...HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete


Author Name

Formulir Kontak

Name

Email *

Message *

Template images by i-bob. Powered by Blogger.