4 Jan 2017

Jike Shupa Awaanika Mastaa Anaowauza Kwa Vigogo, Yumo Wolper, Masogange


DAR ES SALAAM: Imefichuka! Wakati mastaa mbalimbali wakijinasibu mara kwa mara kupitia vyombo vya habari kuwa hawafanyi biashara ya kuuza miili yao kama inavyodaiwa na baadhi ya watu, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ amekiri kuwauza wenzake kibao kwa vigogo, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukujulisha.

Jike Shupa ambaye ni ‘video queen’ kwenye nyimbo mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, bila kujijua, amejikuta akiingia kwenye mtego wa kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers na kutaja idadi ya mastaa huku akieleza kila msanii ana dau lake tofauti, hakuna bei maalum.

ILIKUWA HIVI

Baada ya OFM kupata habari kutoka kwa vyanzo vyake mbalimbali kwamba mwanamama huyo anawauza wenzake, wakiwemo mastaa na kudaiwa kuwa ni kinara mkubwa wa biashara hiyo, OFM iliingia mzigoni na kupata majibu chanya.AANZA KUINGIZWA KINGI

Makachero wa OFM waliwasiliana na Jike Shupa na mmoja wao akamuomba waonane ili aweze kupata huduma ya kuunganishwa na msanii atakayepatiana kwa bei ya wastani.

Jike Shupa baada ya kuelezwa hivyo alimuomba kachero huyo aliyejitambulisha kwake kama mfanyabiashara kuwa wakutane maeneo ya Kinondoni kwenye mgahawa mmoja maarufu majira ya saa moja usiku ili waweze kuzungumza vizuri kuhusu dili hilo.

OFM YAWAHI KUFIKA MGAHAWANI

Saa moja usiku kachero wa OFM alikuwa katika eneo la tukio, alipofika kwenye mgahawa huo alikaa na kumsubiri Jike Shupa ambaye aliingia na vijana wawili aliowatambulisha kuwa ni wadogo zake, ikiwa ni dakika 15 zaidi ya muda wa makubaliano.

OFM: Karibu sana Jike Shupa.

Jike Shupa: Asante, umenisubiri sana eeeh?

OFM: Yeah, lakini siyo tatizo.

Jike Shupa: Pole sana.


Baada ya Jike Shupa kukaa na mhudumu kumsikiliza anachohitaji (OFM ililipia bili yote), mazungumzo kati yake na OFM yalipamba moto na baada ya muda, alielezwa moja kwa moja kuwa dili alilotaka kumpa lilikuwa ni kumpata Amber Lulu ili awe naye kimapenzi, jambo ambalo lilionekana kuwa jepesi mno kwa Jike Shupa.

ATANGAZA DAU

Jike Shupa alimhoji OFM kama alikuwa na fedha za kutosha maana kazi yake yeye ‘anadili’ na watu wenye fedha tu na kwa kumuuza Amber Lulu, alisema atachukua shilingi milioni moja na nusu ikiwa ni nje ya fedha ambazo Amber Lulu atataka kulipwa.

‘MFANYABIASHARA’ FEDHA SI TATIZO

Kuonesha kwamba fedha si chochote, kachero wa OFM hakubisha juu ya hilo, alichofanya ni kumwambia kuwa nusu ya fedha alizokuwa anahitaji  angemlipa muda mchache wakati wakiendelea na mazungumzo, lakini akataka kujua kutoka kwa mwanamke huyo kama amewahi kuwauza mastaa wengine kama anavyofanya kwa Amber Lulu?


Jike Shupa: Wako wengi tu, ambao huwa ‘ninawa-connect’ (kuwaunganisha) na mabwana, mfano, (akataja jina la msanii mkubwa ambaye tunahifadhi jina lake kwa sababu hatukumpata), Tunda, Masogange, Wolper na wengine wengi.

ETI HAKUNA ANAYEMCHOMOLEA

“Hakuna staa wa kike ambaye simfikii, ni wewe tu kusema unamtaka yupi, unatoa pesa halafu mimi namaliza mchezo wote.

“Unawaona hata hao vijana niliokuja nao (anawanyooshea kidole walipokuwa wamekaa)? Hao ni mashoga, huwa nawaunganishia watu (wanaume) wanaowataka kufanya nao mapenzi.”


OFM YAMMWAGA KIAINA

Baada ya OFM kukamilisha upelelezi wake na kujiridhisha kuwa kweli Jike Shupa ni kuwadi na anawauza wasanii wenzake wa kike pamoja na mashoga kwa mapedeshee, ilimtoka ‘kisanii’ mwanadada huyo huku ikiwa na ushahidi wa kutosha.

WATUHUMIWA WAFUNGUKA

Alipotafutwa Masogange na kusomewa mashitaka yake, awali alianza kwa kusema hana urafiki kivile na Jike Shupa na kwamba waliwahi kukutana naye mara moja tu.


“Sina urafiki kivile, nachukia sana mtu kuzungumza kitu ambacho sijafanya, kwanza huyo Jike Shupa mwenyewe hana mtu wa kuniunganisha naye. Hebu ngoja nimpigie sasa hivi nimpe vidonge vyake, sipendagi ujinga mimi,” alisema Masogange na baada ya kumpigia na kumkosa, alimuandikia meseji ndefu Jike Shupa ya kumsuta ambayo aliikopi na kuipiga picha kisha kumtumia mwandishi wetu.

Jike Shupa hakujibu ujumbe huo wa kichambo ambao ulionesha umefika kwenye simu yake.

AMBER LULU NAYE ANENA

Kwa upande wake Amber alikanusha vilivyo madai hayo ya kuuzwa na kama haitoshi, alisema hana hata urafiki naye.

“Huyo labda anatafuta kiki, sina hata urafiki naye ataniuza kivipi? Sinaga hizo habari,” alisema Amber.


WOLPER NAYE AMKANA

Alipotafutwa Wolper na kuelezwa kama amewahi kupigwa bei na Jike Shupa, alimkana kuwa hamtambui na kusema anaomba atumiwe picha ili japo amuone anafananaje, kwani watu wa aina hiyo anashindwa kuwaelewa awaweke kwenye kundi gani.

“Unajua kama ana akili timamu si mwezi mchanga, inabidi nidili naye na ikiwezekana nimshtaki maana atakuwa amenizushia jambo ambalo sijawahi kulifanya lakini kama ni mwezi mchanga (hajakamilika kiakili), naweza nikamsamehe,” alisema Wolper.

MASTAA ZAIDI WAFUNGUKA

Mastaa wa kike mbalimbali walipotafutwa na kuelezwa habari hizo kila mmoja alionesha kukasirika na kuzungumza lake.


BABY MADAHA

“Huyo Jike Shupa hawezi kuniuza mimi labda hao anaoonana nao na suala la kuuzwa ni la mtu binafsi huwezi kuuzwa kama ng’ombe.

“Huyo msanii ana uwezo wa kuwauza wale anaowamudu kwangu atagonga mwamba kwani hatuongei lugha moja, yaani viwanja ninavyoenda ni tofauti na vyake, wanaume anaokutana nao ni tofauti na wale nitakaokutana nao mimi, kwanza Kinondoni na Mbezi ni wapi na wapi?”

SHAMSA FORD

“Mimi nimeolewa hilo haliwezi kunitokea kabisa waulizeni hao ambao hawaeleweki nina mume ndani tayari.”

ISABELA MPANDA

“Huyo Jike Shupa hawezi kuniuza kwa sababu ninajitambua labda hao wengine na sina shida na siwezi kuuzwa kama karanga, huwa naenda kwa mwanaume ninayemtaka.”

ROSE NDAUKA

“Jamani hivyo ni vitu vya kipumbavu siwezi kuvizungumzia wala kumzungumzia mtu kama huyo.”

NENO LA MHARIRI

Kwa kuwa OFM imemnasa Jike Shupa ‘live’ akithibitisha madai ya kuwa anawauza wenzake, anapaswa kuachana na vitendo hivyo mara moja kwani vinakwenda kinyume na mila na desturi za Kitanzania.

Ni tabia ambazo zinakwenda kinyume na mafundisho ya imani za dini zote, ni wakati wa Jike Shupa na mastaa wenzake wote wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kikahaba kuachana navyo na kutafuta mkate wa kila siku kwa njia halali.

Stori: waandishi Wetu, Risasi Mchanganyiko, Jan 4-6, 2017, Toleo 1388

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share:
Weka Maoni yako Hapa

6 comments:

 1. MMMMMmmmmmmm anatafuta kiki!!!???

  ReplyDelete
 2. mashoga pia wanauzwa sana na huyo huyo fanyeni operesheni mtawajua wengi sana nalo ni tatizo sugu sana hapa jijini sasa ivi. kuna shoga maarufu sana anaitwa Davito mtu wa songea huyo ndiye kinara wao pia anawauza sana hao mastar.

  ReplyDelete
 3. Na mimi ningekana kwani baby madaha aliwahi kunaswa kwenye gazeti lenu akijiuza mpaka akaomba msamaha kuwa harudii tena

  ReplyDelete
 4. Na wewe achana na umbea umepitwa na wakati,shwain!

  ReplyDelete
 5. wewe jike shupa kwa nini unawaaibisha wenzako hujui kama wenzako wana wazazi na ndugu kama mmekubaliana uwatafutie mabwana inabidi uwe makini siyo kuongea na kila mtu unayemuona sababu unajua OFM wapo, mwenzako sijui anaitwa Lungi aliongelea kuhusu biashara hiyo lakini hakumtaja msanii yeyote ona sasa umejiumbua mwenyewe, kwanza wewe ni msanii umeonekana kwenye video sasa kwa nini unaropoka hovyo na watu bila ya kuwa makini

  ReplyDelete
 6. Watu hamjifunzi tu kuwa OFM wako kila kona si muda mrefu JB maovu yake yalifichuka kuwa anaishi pia na Miss Kiama mpaka OFM waliongea nae akiwa nyumbani kwa Kiama Jb akaingia ndani kwa Kiama kuwachukulia maji OFM hapo ukawa ushahidi tosha kuwa pia anaishi pale, Jb huwa anamuaga mke wake kuwa anaenda location kushoot video kumbe ni uwongo kumbe anaenda kuishi kwa Ester Kiama, sasa hivi mke wa Jb atakuwa ameshafahamu siri ya mume wake

  ReplyDelete

Total Pageviews


Popular Posts

Matangazo

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger