Nyama Yaanza Kutengenezwa Maabara,Inafanana na Nyama ya Ng'ombe Hadi ladha..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


DUNIA inabadilika kwa haraka kutokana na maendeleo katika sekta mbalimbali. Teknalojia nayo inakua kwa kasi huku ikitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya binadamu. Siku hizi Dunia inashuhudia uvumbuzi wa teknalojia za kisasa katika nyanja za kilimo, afya, nishati na nyingine nyingi.

Leo katika safu hii, nitajadili namna ambavyo wanasayansi walivyofanya jitihada za kutengeneza nyama katika maabara. Ndiyo, sasa si lazima kuhangaika kufuga na kupata usumbufu wa kutunza wanyama ili uweze kupata nyama.

Wote mtakubaliana na mimi kuwa, aina zote za vyakula vinavyotumiwa na binadamu inatokana na mimea na wanyama. Mamilioni ya wanyama huchinjwa kila siku duniani kwa ajili ya kupata kitoweo. 

Uchinjaji wa wanyama umekuwa mkubwa kuliko uzalishaji jambo ambalo limewafanya wanasayansi kufikiri namna ya kutengeneza kitoweo hiki muhimu pasipo kuhusisha kuchinja mnyama.

Rasilimali nyingi zimekuwa zikitumika kulisha wanyama, kuwachinja na kusafirisha, pia kumekuwapo upotevu mkubwa wa maji na nishati katika mzunguko mzima wa kupata kitoweo hiki. 

Ufugaji wa wanyama ambao hutupatia nyama unazalisha gesi ya methane ambayo inamchangio mkubwa katika mabadiliko ya tabianchi, wanasayansi wanataka kuondokana na haya yote kwa kutafuta mbinu mbadala ya kuzalisha nyama.

Kwa upande mwingine, wanyama hufungiwa ndani kwa maisha yao yote. Wanyama pia huchinjwa kikatili ili kuweza kupata nyama. Pamoja na haya yote, ni vigumu kufikiri maisha ya binadamu bila kula nyama. 

Utamaduni wa kula nyama ni mkongwe duniani na kwa vyovyote vile haitakuwa rahisi kuufuta. Kwa kutambua ukweli huu, wanasayansi wameaanza kutengeneza nyama maabara waliyoipa jina la nyama ya Vitro au Vitro meat kwa kimombo.

Nyama ya Vitro huzalishwa maabara. Kwa kawaida nyama hutengenezwa kutokana na kemikali ndogo inayojulikana kitaalamu atoms. Kama unaweza kutengeneza atoms kwa njia tofauti na ya kawaida, basi pia unaweza kutengeneza nyama. 

Ukipewa vipande viwili vya nyama kimoja kilichotokana na mnyama aliyechinjwa na nyingine aina ya Vitro ambayo hutengenezwa maabara ni vigumu kuelezea tofauti yake kutokana na kufanana kwa muonekano na hata ladha.

Maabara sasa inafanya kazi ya kutengeneza nyama ambayo ni sawa na nyama uliyozoea kununua buchani. Profesa wa Molecular Biology, katika Chuo Kikuu cha Stanford, alinukuliwa na gazeti la The Gurdian la Uingereza akisema inawezekana kuondokana na usumbufu wa kufuga na kuchinja wanyama kwa kuwa nyama sasa inaweza kutengenezwa maabara.

“Sina nia ya kutengeneza vyakula vipya kwa watu wasiokula nyama. Natengeneza chakula kwa ajili ya wanaokula nyama na ambao wana nia ya kula nyama. Hii itawasaidia kupata nyama bila shurba.

“Nyama ya Vitro haitokani na kiumbe hai hivyo haiwezi kufa na hii naletea tofauti kubwa katika upatikanaji wake. Kiuchumi, gharama za uzalishaji wake ni kubwa na hivyo kufanya uzalishaji mkubwa kuwa changamoto. 

Pia kutokana na ushawishi wa wafugaji wakubwa Marekani na sehemu nyingine duniani, inawezekana kuwa na vikwazo vya kisheria,” anasema Profesa huyo.

Gharama kubwa za uzalishaji wa nyama ya Vitro inaweza kuwa ndiyo kikwazo kikubwa katika uzalishaji wake. Hata hivyo, ugunduzi zaidi kwenye teknalojia ya uzalishaji wake itaweza kupunguza gharama. 

Kampuni kubwa ikiwamo New Harvest na Modern Meadow zinafanya kazi kuhakikisha kuwa nyama hii inazalishwa kwa wingi na kuwafikia walaji wengi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad