Baada ya Wafanyakazi wa Manji Kukamatwa,Ubalozi wa India Waibuka na Tamko Hili Zito kwa Serikali ya JPM..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


SIKU chache baada ya Idara ya Uhamiaji kukamata raia wa India kwa madai ya kufanya kazi bila vibali, Balozi wa India nchini, Sandeep Arya, ameingilia kati suala hilo na kusema tatizo lilikuwa mawasiliano kati ya mwajiri na Uhamiaji.

Akizungumza jana , Balozi Arya alisema anaendelea kufuatilia kwa karibu suala hilo na kudokeza kuwa jitihada za kumaliza sintofahamu hiyo, zinaendelea kwa njia ya mazungumzo kati ya mwajiri na Idara hiyo.

Akifafanua baada kumaliza kikao chake na wawakilishi wa kampuni 30 za kutengeneza dawa kutoka India zinazojiandaa kuwekeza nchini, Balozi Arya alisema baada ya kubaini tatizo kuwa mkanganyiko wa mawasiliano, ndiyo maana wameruhusu kampuni hizo kuwekeza nchini.

“Unajua zipo ajira za muda, zingine miaka miwili, hivyo udhaifu wa mawasiliano ulisababisha sintofahamu, hivyo taratibu za kufanya ukaguzi zinapaswa kuchukuliwa na vibali vitolewe maisha yaendelee,” alisema.

Balozi Arya alisisitiza kuwa jitihada za kumaliza sintofahamu hiyo, zinaendelea kwa njia ya mazungumzo na ofisi yake kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, watahakikisha suala hilo linamalizika kidiplomasia bila kuathiri ushirikiano uliopo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jamani tupeni kazi fukuza wageni wote tunataka kazi mheshimiwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na ugenini kuna wa-TZ wengi wako huko na wanafanya kazi,je utapenda kusikia wamefukuzwa kulinda ajira kwa raia wao?

      Delete

Top Post Ad