Mwenyekiti wa Chadema Mbowe Aifagilia Mahakama Arusha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kunyimwa dhamana na kukaa gerezani kwa zaidi ya miezi mine sasa.

Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe akiwa nje ya mahakama mjini Arusha baada ya mahakama ya rufaa kufuta rufaa za upande wa Jamhuri, amesema kitendo hicho kiliwafanya waichukie mahakama kuona inapewa maelekezo na serikali, kumbe siyo kweli bali ni mchezo mchafu wa ofisi ya DPP.

“Leo mahakama imetufariji sana na kuturudishia imani yetu kwao kuwa ni chombo kilichosimama kwa miguu yake kama Mhimili wake na haipokei maagizo ya serikali” Amesema Mbowe.

 Amesema sakata hilo linawasababisha kupeleka hoja katika bunge lijalo kuwa waangalie wafungwa na mahabusu walio mo ndani, kwani siyo wote waliokaa kwa sababu za kuhusika na makosa, bali wanaonewa.

Aidha amewapongeza majaji kwa kuitaka ofisi ya DPP kushikilia watu kwa misingi ya sheria na badala ya kuitia najisi mhimili huo kwa sababu ya michezo ya kisiasa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wee nawe hao si ndiyo walikutupia nguo nje au.Unajipendekeza nini mbona ueleweki? au watu wa hukondivyo mlivyo na uenda hamuaminiki nadiyo maana mnafukuzwa kila mnapoenda, maana naona hata hasimu wako mkubwa karejea CHADEMA, hebu kuweni na msimamo hili litawa-cost na ndiyo itakuwa mwisho wenu kisiasa. Acheni kujikweza fanyeni kazi kwa kujiamini na siyo kuwa ndumila kuwili unanufaisha wa njee wakati wa ndani kwako analala na njaa, akili mitope au nyie ni upande mwingine? maaana atuwaelewi kabisaaa.

    ReplyDelete

Top Post Ad