Mwimbaji Billnass Amtetea Petit Man Issue ya Madawa ya Kulevya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baada ya meneja wa label ya LFLG, Petit Man kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya, masanii wa label hiyo Billnass amefunguka na kuzungumzia sakata hilo ambalo lilipelekea bosi wake huyo kukaa ndani zaidi ya wiki mbili kabla ya kuachiwa na mahakama.

Akizungumza na Bongo5 wiki hii, Billnass alidai yeye alikuwa anajua bosi wake huyo hajihusishi na biashara ya dawa za kulevya.

“Uzuri ni mtu ambaye namfahamu kwa hiyo nilikuwa naamini hausiki kwa namna yoyote na nilikuwa naamini siku yoyote anaweza kuachiwa,” alisema Billnass.

Aliongeza,”Kingine pia mimi nimekulia mtaani, ishu za kusikia mtu amekamatwa tumeshasikia sana mpaka ndugu zetu, kwahiyo ni vitu ambavyo vipo na vinatokea. Vingine vinatendeka kwa haki vingine ndio hivyo unaweza kusikia hata kesho Billnass amekamatwa kwa tuhuma fulani kwahiyo haya mambo yapo,”

Rapper huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Mazoea’ ambao amemshirikisha Mwana FA.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad