ZITTO Kabwe Azidi Kuibana Serikali Kuhusu ufisadi wa IPTL....Amtaka Rais Magufuli Achukue Hatua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameendelea kumtaka Rais Magufuli kuchukua hatua dhidi ya anachokiita ufisadi katika kampuni ya uzalishaji umeme ya IPTL, inayomilikiwa na Kampuni wa PAP.

Tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani mwezi Novemba mwaka 2015, Zitto amekuwa mstari wa mbele kumsihi na kumuomba Rais Magufuli afanye maamuzi juu ya kampuni hiyo ambayo imekuwa ikilipwa milioni 300 kila siku bila kujali kama inazalisha umeme au la.

Kupitia mitandao ya kijamii, Zitto ameandika "Rais John Magufuli ana fursa ya kihistoria kumaliza kabisa huu mtandao wa wizi na utapeli uliodumu toka mwaka 1995. watanzania masikini na wanyonge tutakuwa nyuma yake kwenye hili. Atende sasa."

Mnamo tarehe 21, Septemba 2016 Mhe. Zitto Kabwe alimtaka tena Rais Magufuli aoneshe hasira zake dhidi ya hicho anachokiita ufisadi mkongwe wa IPTL huku akieleza masikitiko yake juu ya kutochukuliwa kwa hatua zozote hadi sasa.

Mhe. Zitto Kabwe ambaye amekuwa hachoki kulizungumzia sakata hilo la IPTL amehoji ni nini kipo nyuma ya pazia, na ni nani mfaidika hadi hatua zisichukuliwe, huku akitoa ushauri wa hatua zinazoweza kuchukuliwa na mahakama kwa sasa.

"Mahakama Ina uwezo wa kurejea maamuzi yake kwa kuitisha upya kesi zilizoamuliwa. Hivi hii Mahakama haioni suala la PAP kumiliki IPTL na kuchota mabilioni ya fedha zilizokuwa Benki Kuu na kuendelea kulipwa tshs 300m kila siku izalishe au isizalishe umeme? Ushahidi wote ulionyesha utapeli wa Kimataifa uliofanywa na Harbinder Singh Seth lakini kivuli cha uamuzi wa Mahakama umefanya matapeli hawa kuendelea kunyonya fedha kutoka TANESCO. Huu mrija wa PAP/IPTL upo kinywani mwa The Chato Inc? Ama ni jipu la mgongoni?". Alihoji Mhe. Zitto Kabwe
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Vizuri.
    Kazia na ESCROW.
    Tanzania turudishe sheria, kwa kuwadhibiti wabadhilifu wa mali za umma.
    Ni hapo tu, Tutaweza kusonga mbele. Sasa Wapinzani ingawa silipendi hili jina, unganeni na Muikomboe nchi. Rudisheni sheria, Katiba, na usawa na haki kwa Watanzania wote bila kujali cheo, dini, kabila, rangi na uwezo kipesa. Sheria imlinde, imheshimu, na kumtumilia kila mtu sawa na kwa haki.

    ReplyDelete

Top Post Ad