Alichosema Rais Magufuli Kuhusu Paul Makonda Leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Tofauti na kile ambacho watanzania wengi leo walikuwa wakitarajia kuona Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli akichukua uamuzi mgumu dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, mkuu huyo wa nchi amemuelezea Makonda kuchapa kazi.

Makonda anakabiliwa na kashfa lukuki ikiwemo ile ya kudaiwa kughushi vyeti na kwamba jina lake halisi ni Daudi Bashite, kutumia vibaya madaraka yake ikiwemo tukio la juzi la kuvamia studio za Clouds Media Group akiwa na wanajeshi wenye silaha akilamizimisha kurushwa kwa kipindi na zingine. Tukio hilo limelaaniwa vikali.

Akizungumza Jumatatu hii kwenye uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa barabara za juu (Flyovers) Ubungo, Dar, Rais Magufuli amesema, “Mimi ndio najua mwenyewe nani anatakiwa kuwa wapi akae wapi, ni mimi ninayepanga. Ninajua wamenielewa. Kwahiyo Makonda wewe chapakazi, nasema chapa kazi.”

“Suala la kuandikwa kwenye mitandao sio tija kwangu, hata mimi ninaandikwa kwenye mitandao kwahiyo nijiuzulu urais? Chapa kazi, hapa kazi tu.”

Rais amesema Watanzania wanapoteza muda mwingi kwa mambo yasiyo ya msingi.

“Tumepoteza direction tumeanza kujadili personalities,” aliongeza.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hahahaaaaaaaaaa wamenywea nywiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  2. Itakuwa ni Nchi ya kwanza kabisa Duniani kuongozwa na vijimaneno vijimaneno vya mitandaoni. Hii itakuwa ni ajabu katika Dunia hii haijapata kutokea. Yani Nchi iongozwe na vijimaneno vya mitandao??? Kwa kweli Mheshimiwa hapo umenena. Na ni ukweli usio na shaka kuwa sisi Watanzania tuna tabia chafu sana za kupoteza muda wetu kwa kushughulika na mambo mengi yasiyokuwa na maana kabisa katika maisha yetu. Kwa tabia za aina hii kwa kweli maendeleo yetu sisi Watanzania kwa kuanzia mtu mmoja mmoja mpaka Taifa kwa ujumla itabakia ndoto.

    ReplyDelete
  3. chezea mke wewe!

    ReplyDelete
  4. Tanzania inamaraisi wawili JPM na raisi Makonda.

    ReplyDelete

Top Post Ad