Breaking News...Makonda Afunguka Kuhusu Elimu Yake,Atoa Majibu Haya Kwa Wanaoshinda Mitandaoni Wakimsema..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KUHUSU ELIMU YAKE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefunguka tuhuma zinazozushwa kupitia mitandao ya kijamii na watu mbalimbali kuhusu elimu yake na zinazoeleza kuwa amefoji cheti cha mtu mwingine.

Akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri wa Mkoa (RCC) RC Makonda ameeleza kuwa kinachogombaniwa siyo Makonda bali ni kiti alichokalia (UKUU WA MKOA), hivyo ameeleza kuwa nafasi yake ya ukuu wa Mkoa amepewa na Mungu.

Na kufafanua kuwa hatakama angepata sifuri au daraja la kwanza katika masomo yake, Mungu angetaka awe Mkuu wa Mkoa angekuwa tu, kwani Mungu ndiye anapanga kila kitu na kuongeza kuwa yupo imara kuliko alivyokuwa jana.

KUTISHWA KWA WAZAZI WAKE

Pia RC Makonda amefunguka kuhusu kutishwa kwa baba yake mzazi, pia kuna watu walikwenda eneo analoishi baba yake na mama yake mzazi na kupiga picha, ili wakaoneshe nyumba anayoishi mzazi wake.

KUHUSU KUITWA SHOGA NA MGUMBA

RC Makonda ameeleza kuwa watu wamekuwa wakimtolea lugha chafu kuhusu uzazi wake na kumuita mgumba kwa kuwa hana mtoto na wengine wamekuwa wakimuita shoga, amefunguka na kusema kuwa haoni tusi jipya.

RC Makonda amesema ipo siku watu wataulizwa kuhusu matendo wanayoyafanya duniani kilasiku, hawana budi kuwa makini na matendo yao.

KUHUSU DAWA ZA KULEVYA

RC Makonda ameeleza kuwa tangu aianze vita ya dawa za kulevya yameibuka mengi na kusisitiza kuwa hatoacha ataendelea kwani wapo wanaoshukuru kuanza kwa vita hiyo na kuhoji kwanini haikuanza mapema kwani imeokoa maisha ya wengi, kuhusu maendeleo ya vita hiyo RC Makonda amesema kuwa mashamba ya bangi yanateketezwa kila uchwao, siku mbili zilizopita wamekamatwa watu 100 na kete 400 za dawa hizo pia zimekamatwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

19 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ili kumaliza utata aoneshe vyeti ili kujisafisha maana washamtia doa na atopata heshima Kama hapo mwanzo....ushsuri tu

    ReplyDelete
  2. Hivi elimu kwanini inadaiwwa sasa baada ya kuwaumbua wenye madawa ya kulevya. Unayedai elimu sasa ni mmoja wa walevi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa issue ya vita ya madawa ya kulevya wote tunaunga mkono na kwa kweli nampongeza Mh. Makonda sababu amekuwa wa kwanza kuthubutu hadharani na kwa uwazi ingawa njia aliyotumia ina ulakini kidogo ila angalau sasa vita inaendelea. Big up kwa hilo. Lakini suala la vyeti nalo limejitokeza kwa ujasiri ule ule anapaswa kulitolea ufafanuzi ili wananchi wake tujue ukweli nao ukweli pia utamuweka yeye mwenyewe huru. Ushauri wangu ni kwamba asilumbane, asijitetee ila aeleze ukweli wa mambo ili kuondoa hilo doa linalozidi kusambaa lakini endapo ni kweli vyeti vyake ni feki basi awe gentleman ajiuzuru tu ili pia kuendelea kuunga mkono Mh Rais ktk vita dhidi ya vyeti feki nayo itakuwa heshima kwake.

      Delete
    2. Nampongeza Mh.Makonda kwa udhubutu wake katika kuanzisha vita dhidi ya madawa ya kulevya. Wazazi wengi tumeguswa na madawa haya. Kama halijakufika huwezi kuelewa namna ambavyo ndugu wa vijana walioathirika na madawa ya kulevya wanavyohangaika kuwarudisha watoto wao katika hali yao ya bila madawa; namna ambavyo resources nyingi za familia zimetumika katika kuhudumia waadhirika. Hili la vyeti vya Mheshimiwa lisiingizwe katika vita hii. Si wakati muafaka kabisa.Lisionyeshwe kama.linalumbana na dhana nzima ya vita ya madawa ya kulevya. Tutapoteza mwelekeo katika vita hii.

      Delete
  3. Hata wasemeje lakini wauza ngada Hamna chenu tafuteni cha kufanya tu mana raslimali nyingi

    ReplyDelete
  4. Nafikiri kinachihitajika zaidi ni uwezo ktk kuimudu kazi na amshaonyesha umahiri. Kwa nafasi yake sidhani km wakato wote inahitajika shahada ya juu sana

    ReplyDelete
  5. Kwanini mkuu wa kaya aliagiza uhamiki wa vyeti mbona wengine wamebajia

    ReplyDelete
  6. Mkuu wa kaya aliekeza vizuri kuhusu umuhimu wa kuhakiki vyeti ili kilaza asipewe nafasi je zoezi lilikuwa batili

    ReplyDelete
  7. Mkuu wa kaya aliekeza vizuri kuhusu umuhimu wa kuhakiki vyeti ili kilaza asipewe nafasi je zoezi lilikuwa batili

    ReplyDelete
  8. Ameelezea vzuri. Ila kwa vile wakati huu ni wakati kuondoa walaghai wa vyeti Waliopo maofisini, ni vyema na yeye akaondoa utata uliopo juu yake na kusonga mbele.

    ReplyDelete
  9. unapenda mziki? basi acha maneno onesha vyettii

    ReplyDelete
  10. Ndg Mkuu wa Mkoa, Mungu akubariki na kuktia nguvu, wewe ni striker hatari kuishambulia timu ya uovu hasa ulw wa madawa ya kulevya. Sasa ile timu ina mabeki wanaoshambulia kutoka kila kona wakiwa na lengo la kukupotezea target yako ya kusafisha maovu katika jiji hili. Ni kwako tu mtu anaweza akataja mhalifu bila kujulikana. Wengine wakiambiwa wanaenda kusema ni fulani kakutaja.Tayari unakuwa katika kuwindwa na wa tu wabaya.
    Kuhusu elimu, kazi uliyoifanya ya utafiti wa madawa ya kulevya, nikazi ya umakini tena usipozimia moyo watu watakuja kujifunza kwako. Elimu uliyotumia katika utafiti ni ya kiwango cha Doctorate, jitahidi uandike kitabu watu watakuja jifunza kwako.
    Jinsi ulivyopambana na ukahaba " you are the icon' watwala wengine miaka ijayo watajifunza kwako. Pata mwandishi mzuri to compile 'all of your work'. Nakuombea umetenda mema kwa taifa lako, Bwana Yesu akutendee mema wewe na familia yako. Kwa jina la Yesu .Amen

    ReplyDelete
  11. Onyesha Vyeti endelea kupiga kazi. Jiamini baba, ulisema uko tayari kufa sasa vyeti tu? Kuliko drug dillers?

    ReplyDelete
  12. Mungu Skype moyo huo huo ea ujasiri na ushuoavu. Utuokolee watoto wetu. Malipo yako kwa mungu.. Biashara inazidi kukusa wateja..itanidi tuzibiti sehemu zote za uingizaji.na uuzaji. KAZA BUTI KAMA BABA JPJM UNYOOSHE HAWA WAHARIBIFU WASIO MUOGOPA MUNGU WALA KULIOENDA TAIGA LETU..kazi yako Ni nzuri HONGERA

    ReplyDelete
  13. Hawa ndio wale wale waliotaka JPJM aoneshe Salary slip yake. Sasa wanaomba cheti.. Unawapotezea tu.
    jina lolote uwaruhusu ila wasitukane tu wakosefu wa haya na ustaarabu. TANZANIA BILA YA MADAWA TWAWEZA. na Dar yetu mpya Chini ya Kijana Shupavu na Jasiri madawa yameanza kupotea na Watoto Zetu wana Anza kupata afya njema japo Ulezi wake na Huruma tunaiona. LAKINI CHONDE CHONDE HII VITA ENDELEVU UIZIDISHIE NGUVU NA MUNYE NDIE ATAKUPA MALIPO YAKO KUTUOKOLEA WAATHIRIKA. MENGINE NI YANA LENGO YA KUKUONDOLEA MWELEKEO. FUMBA MACHO NA ZIBA MASIKIO. BIASHARA YAKO HAINA WATEJA KAMA HAPO AWALI.... HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  14. Hawa ndio wale wale waliotaka JPJM aoneshe Salary slip yake. Sasa wanaomba cheti.. Unawapotezea tu.
    jina lolote uwaruhusu ila wasitukane tu wakosefu wa haya na ustaarabu. TANZANIA BILA YA MADAWA TWAWEZA. na Dar yetu mpya Chini ya Kijana Shupavu na Jasiri madawa yameanza kupotea na Watoto Zetu wana Anza kupata afya njema japo Ulezi wake na Huruma tunaiona. LAKINI CHONDE CHONDE HII VITA ENDELEVU UIZIDISHIE NGUVU NA MUNYE NDIE ATAKUPA MALIPO YAKO KUTUOKOLEA WAATHIRIKA. MENGINE NI YANA LENGO YA KUKUONDOLEA MWELEKEO. FUMBA MACHO NA ZIBA MASIKIO. BIASHARA YAKO HAINA WATEJA KAMA HAPO AWALI.... HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  15. Waliosema vyeti vya Makonda siyo kwamba hakusoma shule ila alirudia darasa la saba baada ya kufeli mara ya kwanza. Jamani kwa watu waliowengi mbona hizo zimetumika na wakafaulu na wengine sasa hivi ni maprofesa na ndo maana waliweka kuapa ili uweze kubadili jina. Tatizo ni kama hakusoma na anavyeti vya kugushi lakini kama shule ameenda kwa kutumia jina la mtu siyo shida ndo ulikuwa mfumo wa hapo nyumba.

    ReplyDelete
  16. Hoja kuchapa kazi tu. Unaweza kuwa daktari bila yakuwa na taalima nayo. kutokana na hayo ile tabia ya kuhakiki vyeti ambayo ilisababisha wengi kuzikimbia kazi zao au kufukuzwa na huku wakiwa wafanya kazi mahiri. mii naona hata ikiwa mtu hana cheti lakini anajuwa kazi basi inatosha na waliofukuzwa au wenyewe kuzikimbia kai zao kwa hofu ya kukamatwa warejeshwe pindi kama walikuwa wanazijuwa kazi zao

    ReplyDelete

Top Post Ad