Huu Ndio Umafia Unaofanywa Nyuma ya Pazia Kuhakikisha Makonda Anatumbuliwa Ukuu wa Mkoa......!!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Imebainika kuwa njama za kumtoa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda zilianza Bungeni kwa kuratibiwa na baadhi ya wabunge wanaohusishwa na mtandao wa dawa za kulevya.

Katika kudhibitisha hili, walifanya kikao Dodoma kilichohusisha baadhi ya wabunge na kukubaliana kuunganisha nguvu na wafanyabiashara na Viongozi wa Dini waliohusishwa na biashara ya Dawa za kulevya.

UTEKELEZAJI WAKE :-
1. Walikubaliana kuungana na baadhi ya viongozi wa ukawa ambao hapo awali walikuwa mahasimu wao kisiasa, zoezi lililoratibiwa na mbunge mmoja ambae ni mtoto wa kiongozi mstaafu, rejea picha za matukio mbalimbali wakati wa mechi ya simba na yanga (zoezi lilifanikiwa)

2. Kuwaunganisha kwenye mtandao wafanyabiashara wakubwa waliotajwa na Makonda pamoja na kumuunganisha Askofu mmoja alietuhumiwa kujihusisha na mtandao wa dawa za kulevya, lengo la kuwaunganisha hawa ni kupata ufadhili wa fedha za kutosha, rejea kauli za baba askofu akidhibitisha kujizatiti kumuondoa Makonda Dar (zoezi lilikamilika)

3. Kushawishi marafiki wakubwa wa makonda ambao walikuwa wakimsaidia Makonda katika vita ya dawa za kulevya kwa kuwarubuni kumgeuka makonda na kuungana katika kambi yao kwa makubaliano kuwa makonda akiondoka Dar watashinikiza kupatikana kwa mkuu wa mkoa ambae atakuwa hana purukushani za dawa za kulevya, udhibitisho wa hili ni RUGE KUMGEUKA MAKONDA(zoezi limefanikiwa)

4. Kutumia baadhi ya mawaziri ambao watu wao walijeruhiwa kwenye kampeni za uchaguzi na kuwaingiza kwenye mtandao wa kumtoa Makonda Dar, ushahidi wa hili ni alliance ya Mgombea wa Urais kutoka Lindi, mahusiano yake na waziri ambae amejitoa Muhanga kumpinga Makonda hadharani.(zoezi lilikamilika tangu dodoma)

5. Kutengeneza tukio ambalo litamfanya makonda apate aibu mjini, kisha wamtake makonda aaibike, wakishapanga mtego mmoja makonda akaujuaga mida ya nyuna akukwepa, sasa hili tatizo la makonda kwenda CLOUDS usiku lilivyotokea wakaamua KUKANYAGIA HAPO HAPO.

6. Kuwashawishi baadhi ya wabunge wa chama tawala kutoa vitisho kama Makonda hataondolewa kwenye ukuu wa mkoa basi watajiuzulu , ushahidi wa hili ni post ya face book ya mhe Kingu(zoezi lilifanikiwa)

HITIMISHO
-Jiulize tangu lini clouds na mmiliki wa ipp walishakuwa na mahusiano ya karibu kama juz?

- Jiulize tangu lini EFM na CLOUDS walishakuwa marafiki?

- Jiulize tangu lini Askofu alishawai kukaa karibu na CLOUDS?

- Jiulize tukio linalotajwa la uvamizi limetokea ijumaa, kelele zimeanza kupigwa Jumatatu hii ni baada ya hawa mabwana kukutana jumamosi na kufanya kikao cha pamoja jumaosi na jumapili hela ikatoka kanisani kwa askofu kwa kazi maalum Jumatatu.

-Jiulize hiyo jumatatu jamaa kafanya mahijiano live asubuhi, kisha saa nne asubuhi Mhe waziri anatinga CLOUDS akiwa na mzee wa ipp, na hapo hapo kamati ya huduma za bunge inakwenda CLOUDS mchana huo huo? 

-Jiulize kwa nini wote wameshinikiza Makonda aondolewe Dar?
Na mwisho kabisa, baada ya Mhe Rais Dkt. John Magufuli kustukia njama zao kutokana na kuwa na kikosi imara cha ujasusi katika maeneo mbalimbali akawabomoa LIVE bila chenga pale ubungo wakati wa uzinduzi wa mradi wa flyover.

TUKIDHANI WATAMUELEWA MHE RAIS WAMEGOMA NA KUMSHAWISHI MHE WAZIRI KUUNDA KAMATI WAKATI WANAJUA MHE RAIS AKISHAONGEA MJADALA UMEKWISHA, LAKINI WAO WAMEAMUA SASA KUPAMBANA NA NGUVU ZA MHE RAIS KWA KUSHINIKIZA BAADHI YA WABUNGE WAJIONDOE KWENYE NYADHIFA ZAO.

NB:Hayo ni Maoni ya Mmoja wa Msomaji Wetu na Wla Si Msimamo wa Blog Hii,Sisi Kazi Yetu ni Kufikisha Taarifa Tu,na Hata Wewe  Unaweza Kuwasiliana nasi kuweza Kuandika  Makala ya Maoni Yako Hapa

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukisikia 'MTANDAO WA MADAWA YA KULEVYA' sio watu wa MCHEZO-MCHEZO!!

    ReplyDelete
  2. Lakini kweli, Clouds ndio 'mashoga-zake-vipenzi' iliwezekana kuyamaliza kimya-kimya....ANYWAY, ASO'MTU ANA MUNGU.........

    ReplyDelete
  3. Weka vyeti hapo

    ReplyDelete
  4. Mmh! Mbona kama haya maneno yanaendana na yale aloyasema Steve Nyerere kwenye ile clip yake na Mama'ke Wema?? Maana alisema Mh. Nape wanapanga bonge la mkakati kwa siri, lakini Wema asiambiwe maana ni LopoLopo......sasa naanza kupata picha ya yale mazungumzo ya Mama Wema na Steve Nyerere......ANYWAY, sterling hauwawi!!

    ReplyDelete
  5. ALAH KUMBEEEEEEEEEE..SASANDO PICHA KAMILI NIMEIPATA..NAKUKUBALI KWA ASILIMIA MIA ZOOOTE.. ITS AGAINST DRUGS THATS SO..

    ReplyDelete
  6. Hata nyie kuchapisha hii taarifa tu, mnaonekana hamna fikra pevu. Upuuzi mtupu umeandikwa hapa. Namuuliza tu huyo mwandishi, je, kwenda clouds na askari wenye silaha na kufanya fujo ilikuwa sahihi!? Au kuonekana na magari ambayo inasemekana ni ya watu aliowatuhumu kuhusika na madawa ya kulevya ni sahihi!? Msitufanye wapumbavu aisee

    ReplyDelete
  7. tuko pamoja MAKONDA-na MUNGU ATAKULINDA- BABA WA WATU ,MAGU OYEEEEEEEEE MAKO OYEEEEEEEEEEEEE ..ASANTE KWA KULITAMBUA HILO..

    ReplyDelete
  8. Mpaka global publisher mlivyotumbuliwa ndo mnaza kumsakam makonda

    ReplyDelete
  9. Hamna cha vyeti walaa nini? Mbona huko nyuma yote hayakulizwa hayo. Hangoki mtu Hapa. Makonda chapa kazi. Nchi hii imezoea maovu na mabaya. Mazuri hwayapendi kwa kuwa ni hao hao walioko huko. Sasa wanaona wamebanwa pa kushika hawapaoni, mwendo mdundo tu si utawala wa kuchekeana huku, huku wanaoaribikiwa ni kundi la walala hoi.

    ReplyDelete
  10. Hawa Madrag deler wasicheze na akili zetu, watacheza na akili za wajinga wajinga tu. Mwenye akili anaelewa Kila kitu kinachoendelea dhidi ya viongozi waminifu wanapokuja kukemea hili swala la hili Janga au tatizo, wao si wamezoea kuona mijihela ya halamu ikimiminika tu bila kuipatia jasho, basi watafanya Kila njia ya kuwalaghai watu. Mmmmh ni shida

    ReplyDelete
  11. Unajaribu kupotosha uma , na leo itakua mwisho kusoma ki blog chako uchwara ,habari yako haijabalance imekaa kinafiki na inaonekana umelipwa .Hivi mtu kwenda kuvamia kituo cha radio na kulazimisha habari ya uongo itangazwe kwa nia ya kuchafua tu hiyo ni vita ya madawa ? Hilo hulioni ? Hivi unamtajaje mtu anafanya madawa na magari yake wewe ndo unatumia hilo nalo hujaliona ? Hivi sisi watanzania tumelongwa na nani ? Kweli Njaa hii itatumaliza

    ReplyDelete
  12. Baadhi ya watu bwana wanajidai wanajua sana sheria wakati nao hawana lolote, hivi mnajua maana ya silaha, tafuteni definition ya hili neno, je mnajua maana ya kuvamia? ukielezwa benki imevamiwa na majambazi au watu wenye silaha za moto maana bunduki unaelewa nini? kwani mmeambiwa mlango wa studio za Clouds umevunjwa? nani kaumia katika sakata hilo? nani anajua kabla tukio wao studio na RC walikubaliana nini? kuna mchezo ulichezwa hapo kwa vijana wa kipindi husika kuwa double agent kucheza Gwajima na Rc , kuna maoni gani kuhusu kipindi chenyewe cha SHELAWADU? kina manufaa gani kwa jamii ya watanzania?tuache siasa tufanye kazi tusonge mbele.

    ReplyDelete
  13. kuishi mjini na kujimix na watu pamoja na kujisomea sana kunanifanya muelewa wa mambo hata kwa kumtazama mtu bila ya kumsikiliza na ntacho extract toka kwake haita pingana na uhalisia wenyewe. Hili movie la kiutu-uzima yatakiwa uwe mtu wa dimension nyingine ndio linasomeka tena wala halihitaji nguvu nyingi ya meditation. poleni msioelewa ila hamjachelewa yawabidi kuitafuta elimu ya vitabuni na wala havipotei tena haichukui muda kuwa elevated hapo ndipo mtapojua kupima mizani ya parables za namna hii wepi wanaeleza ukweli na wepi wanaongopa maana tofauti ya perfect-imperfection na perfect perfection ni ndogo sana yani (3x6x37) na (3x7x37). kazi kwenu

    ReplyDelete
  14. KIKUBWA HAPA NI KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA TU, MENGINE BAADAE. NA MKAE MKIJUA HAKUNA SIRI DUNIANI KWANI MNAVYOPANGA MAMBO YA AJABU AJABU, HAPO HAPO WAPO MAMLUKI MTAUMBUKA HADI MUWE KWENYE MSTARI. MAKONDA PAMBANA WALA USIJALI. MUNGU ATAKULINDA.

    ReplyDelete
  15. magu na makonda nyie kazeni tu wenyewe watalegeza na kuachia ...

    ReplyDelete

Top Post Ad