20 Mar 2017

Imevuja Shilole na Nuh Hawawezi Kuachana,Waonekana Hotelini Wakipeana Malove kwa Siri...!!!!


Wanaubuyu wanakuambia kuwa kuendelea kuwasiliana mambo ya malavidavi na ‘eksi’ wako ni sawa na kutembelea muwa kama fi mbo kwani ipo siku utautafuna! Hicho ndicho kinachodaiwa kuendelea kati ya mastaa wawili Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ na Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.

Ubuyu unadai kuwa, Shilole au Shishi na Nuh wanaendeleza libeneke la kukwichikwichi na kwamba hawawezi kuachana, licha ya Nuh kufunga ndoa na Nawal na kujaliwa mtoto wa kike hivi karibuni.

Chanzo makini kilinyetisha kuwa, tangu Shishi na Nuh wamwagane umepita muda mrefu, lakini kuna ubuyu wa kunyapianyapia kwamba wamekuwa wakimtesa Nawal kwani anaweza kukata hata mwezi mzima bila kumtia machoni mumewe huyo.

CHANZO CHATHIBITISHA

Chanzo hicho ambacho ni rafi ki wa karibu wa ‘kapo’ hiyo kilidai kuwa kina uthibitisho usiokuwa na shaka kwamba Shishi na Nuh wamekuwa wakikutana kwenye hoteli moja iliyopo Sinza, Dar (jina tunalo) ambapo wanadaiwa kuitumia kula bata na kumbonji mara kwa mara

WALALA HOTELINI

“Hivi mna ubuyu kuwa Shishi Trump na Nuh hawajawahi kuachana? Kwa taarifa yenu huwa wanatoka ‘out’ na kulala pamoja pale…(kinataja jina la hoteli hiyo).

“Kiukweli hawa watu hawawezi kuachana na naionea huruma sana ndoa ya huyo Nawal kwani siyo siri inaelekea pabaya maana Shishi naye si mtu wa mchezomchezo linapokuja suala la malavidavi anapokuwa kwenye kumi na nane,” kilisema chanzo.

Chanzo hicho kiliendelea kufunguka kuwa, shosti wake, Shishi ana imani ipo siku Nuh atamwagana na Nawal kisha ataolewa yeye maana anampenda jamaa huyo kinoma na hakuna anayeweza kuwaachanisha.

WIKIENDA LACHIMBA

Baada ya ubuyu huo kutua kwenye meza ya Wikienda, wanahabari wetu walianza kuichimba ambapo walikutana na Shishi uso kwa uso ili azungumzie ishu hiyo ambapo mahojiano yalikuwa hivi; Wikienda: Kwanza Shilole unazungumziaje Nuh kupata mtoto wa kike?

Shilole: Nimefurahi sana…tumepata mtoto… hahahaaa…

Wikienda: Kwani mtoto wa Nuh ni wako pia?

Shilole: Si aliwahi kuwa hivyo? Nuh akipata mtoto mimi nafurahi kama mtoto wangu.

Wikienda: Je, hutamani nafasi hiyo ingekuwa yako? Shilole: Hapana.

Ningetaka kuzaa na Nuh ningezaa naye na si mtoto mmoja hata watatu, lakini haikuwa hivyo.

Wikienda: Hata hivyo, kilichotuleta kwako si mambo ya mtoto bali ni ubuyu tuliofi kishiwa kuwa huwezi kumuacha Nuh na mmekuwa mkijifungia hotelini Sinza kisha mnafanya yenu, je, hili likoje?

Shilole: Hahahaaa…mbona mnapenda kuniuliza swali hilo? Niseme mara ngapi? Nuh ana familia yake jamani! Kama ndivyo itafi kia time (wakati) nitaacha kuongea kuhusu ishu hiyo.

Wikienda: Wewe unachotakiwa kujibu ni kweli au si kweli kwani watu wakiachana kurudiana inawezekana hata ndani ya siku mbili tu.

Shilole: Kiukweli siwezi kuliongelea suala hilo, kama mmesikia basi lifanyieni kazi, kama mambo yapo yataonekana tu lakini ninachojua Nuh ana mkewe na wamepata mtoto hivyo wana furaha sasa.

HUYU HAPA NUH.

Nuh alipoulizwa aliendelea kusisitiza kuwa, yeye na Shilole ni washkaji tu na anamheshimu mkewe. “Mimi na mke wangu tunapendana, huyo Shilole atabaki kuwa zilipendwa tu, mimi sina uhusiano naye kwa sasa,” alisema Nuh.

KUTOKA KWA MHARIRI.

Kama kweli lisemwalo lipo, Shilole atakuwa anamkosea Nawal na kwa upande wa Nuh anapaswa kuheshimu ndoa yake.


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment


Popular Posts

Matangazo

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger